Tulimkosoa Hayati Magufuli na sasa tutamkosoa Rais Samia. Kama mtaumia poleni sana Tanzania Kwanza

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Kuna watu wanataka kuuaminisha Umma kuwa Rais Samia Suluhu hakosei.

Hawa watu kwa kuendelea na upuuzi ule ule kwa waliokuwa wanazi na mashabiki wa Magufuli ambao nao walikuwa wanataka kuuaminisha Umma kuwa hakuwa akikosea.

Watanzania wengi wanajikita katika Ushabiki, Mahaba, Jazba, Mihemko na Ashki hata katika mambo ya msingi ya Kitaifa.

Kwa sasa limeibuka kundi la watu ambalo ukimkosoa tu Rais Samia unaonekana ulifaidika na utawala wa Magufuli. To hell.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO

Ni muendelezo wa kutumia matumbo kufikiri toka miaka na miaka tunaposhindwa kukemea ubovu kwa kuamua ku side na waovu kwa kuangalia kabila,dini,chama,jinsia,dhehebu n.k

Mimi nitasimama kama Mtanzania hawa wote watapita Tanzania itabaki. Tutamkosoa Samia na akija Mwingine akakosea tutamkosoa kama ambavyo tulimkosoa Kikwete na Magufuli pia.

Na atakayefanya vizuri tutampongeza kwa mazuri yake.
 
Wengine pia muwe tayari kusema fitina kwangu mbelee, mengine yanafuata.
 
Kukosoana kunaleta tija hasa ikiwa kukosoa kunapokuwa sahihi, kutoka kwa mtu sahihi, kuhusu jambo sahihi kwa mtu sahihi. Tatizo linakuja sio kila kitu kinakosolewa.

Ndio maana Hayati hakupenda kukosolewa kwa sababu waliokosoa hawakukosoa kwa murua na heshima bali vilikosolewa hata visivyohitaji kukosolewa.

Mama kama kiongozi wa serikali anaweza akakosoa hivyo kukosolewa kunatarajiwa, lakini tukosoe kwa adabu, heshima na kuzingatia hadhi ya cheo chake. Na pia tukosoe vyenye tija..
 
Nikajua katika maelezo yako chini kuna point ulizogusia mapungufu ya Samia ambayo umelenga kukosoa

Kumbe unatupa taarifa tu kuwa utamkosoa bila ya kuainisha mapungufu ambayo utayakosoa

Kwa mantiki hiyo mpaka sasa hauna la kumkosoa ila umekamia kumkosoa basi wewe ni MKOSOFU
 
Duh, limekuja Gang lingine tena. Tutakuwa na Gangs ngapi?
Wakulaumiwa ni mwendawazimu na wapambe wake, ndio wameifikisha CCM hapa. Tuliposema Mwendawazimu ni mbaguzi na anapandikiza chuki, tuliitwa wasaliti sio wazalendo, na tulichezea risasi, na mateso makubwa.

Sasa MaCCM yakulana yenyewe kwa yenyewe.😂😂
 
Wakulaumiwa ni mwendawazimu na wapambe wake, ndio wameifikisha CCM hapa. Tuliposema Mwendawazimu ni mbaguzi na anapandikiza chuki, tuliitwa wasaliti sio wazalendo, na tulichezea risasi, na mateso makubwa.
Sasa MaCCM yakulana yenyewe kwa yenyewe.😂😂
Well said Mkuu sasa wanaparuana wenyewe kwa wenyewe....
 
kukosoa kwa nia ya kujenga ni jambo muhimu zaidi kuliko kusifia kwa kujipendekeza. ogopa sana kusifiwa sana!!! wala kiongozi makini hapendi kusifiwa sana.

kwa viongozi wetu kumbukeni kuwa ukiona unasifiwa sana kupita kiasi ufahamu kuwa kuna watu wanakupumbaza kwa kulinda masilahi yao hivyo shituka haraka, epuka sifa zisizo na maaana.
 
Wala usiache kukosoa ndo wajibu wako kama mwananchi na ukiacha hayo majukumu yako basi subiri kupokea usivyopenda.
 
Hiyo ni tabia za baadhi ya watu. Siku mama akimaliza muda wake wanamgeuka na kuanza kuongea against her....yaani Tanzania kuna rangi na drama kibao za kisiasa na kishabiki.
 
Huyu mwenye Bandiko ni Mataga pure nilipo weka neno HAKI amefura kweli kweli kama anauchungu akamsaidie mwenzawake kule Kisongo...
Mwendawazimu kawavurugia sana CCM, Samia kazi anayo..
Wameparaganyika sana, kumtuliza mwanaccm kwa sasa lazima umuonge teuzi. yetu macho😂😂😂
 
Back
Top Bottom