Tulilaani ubaguzi, mauaji ya Sharpeville, Soweto; Iweje tukubali ubaguzi, mauaji ya Arusha, Songea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulilaani ubaguzi, mauaji ya Sharpeville, Soweto; Iweje tukubali ubaguzi, mauaji ya Arusha, Songea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Feb 23, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Ni jambo ambalo hadi leo linanikera, linaniudhi, na kunisikitisha sana. Tanzania katika miaka ya 1960 hadi 1990 ilikuwa mwanzilishi wa nchi tano zilizo mstari wa mbele katika ukombozi wa kusini mwa Afrika. Tulilaani kwa ngiuvu zote ubaguzi wa rangi. Tulilaani kwa nguvu zote ubabe wa polisi wa makaburu dhidi ya raia wasiokuwa na silaha walipoandamana kudai haki zao. Tulilaani haya yakitokea nje ya mipaka yetu.

  La ajabu sana, leo hii tunakubali ubaguzi na ubabe wa polisi ndani ya mipaka yetu wenyewe. Leo hii wazungu wengi wanaokuja katika nchi yetu kwa mlango wa uwekezaji wanawanyanyasa na kuwafanyia ubaguzi wa rangi raia na wazalendo kwa kiasi cha juu sana, na serikali yetu haitaki kusikiliza kilio cha wananchi kwa kuogopa kuwaudhi wawekezaji. Kuna baadhi ya wawekezaji toka South Afrika wanafanya vitendo vya kibaguzi kwa namna ambayo wasingethubutu hata kidogo kuvifanya huko kwao katika Afrika Kusini ya sasa. Viongozi wetu hawaoni shida juu ya hili, hawataki kuwasikiliza wananchi juu ya hili. Leo hii mtanzania mweusi hana haki katika sehemu kama migodi ya dhahabu, ananyanyaswa katika nchi yake mwenyewe, anadharauliwa na bosi wake mzungu na hana kwa kusemea kwa kuwa hakuna anayemsikiliza. Haya yote yanafanyika katika nchi iliyokuwa mstari wa mbele kulaani ubaguzi, na hata Watanzania wakapoteza maisha katika vita dhidi ya ubaguzi kusini mwa Afrika. Hata hao wageni wazungu katika nchi yetu wanatucheka na kutudharau sana, wanatukebehi wakisema kwa jinsi mlipovyopiga kelele juu ya ubaguzi wa rangi, tulidhani hapa Tanzania mtu angehukumiwa kifo kwa kufanya ubaguzi wa rangi, sasa iweje baadhi ya wenzetu wanawafanyia ubaguzi wa rangi na hakuna lolote serikali yenu inachofanya? Huu ni unafiki sana.

  Vipi ubabe na mauaji ya polisi ya raia wasio na silaha? Naam, tulilaani Sharpeville, pale polisi walipopiga raia risasi za moto migongoni. Hatukuuliza serikali ya makaburu kama wale raia walikuwa na kibali cha kuandamana, bali tulilaani tu, tukasema walikuwa na haki ya kudai haki zao kwa maandamano.

  Tulilaani mauaji ya Soweto polisi walipopiga na kuua wanafunzi wasio na silaha. Hatukuuliza kama wanafunzi waliomba kibali cha kuandamana. Tulisema wanafunzi walikuwa na madai ya msingi na ilaaniwe serikali ya makaburu kwa kuua raia wasio na silaha.

  Tuliaani ubagaguzi, ubabe wa polisi nje ya nchi yetu. Tulitoa hotuba kulaani, tulikatisha masomo na kazi na shughuli za shamba ili tuandamane na kulaani, tulitunga miziki kulaani, na hata tulipeleka jeshi letu kupigana - tukisema uhuru wetu hauwezi kuwa safi wakati ndugu zetu wanabaguliwa na kunyanyaswa na ubabe wa polisi. Tuliwaita watu wa Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini waje nchini kwetu wafungue kambi za mafunzo ya kijeshi ili wakapigane nchini kwao kuondoa ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa polisi. Tukasema tutapigana nao bega kwa bega hadi tone la mwisho la damu!

  Sasa ubaguzi, mauaji ya polisi yanatokea ndani ya mipaka yetu. Tunaona sawa inakubalika. Raia wanapigwa na polisi na tunaambiwa sababu ni kwamba raia waliandamana bila kibali tukawapiga risasi za moto. Tunaona sawa. Tuaangalia picha za polisi wakitumia mabavu dhidi ya wanafunzi chuo kikuu na kwingineko kwa udhalilishaji wa hali ya juu. Tunaona sawa.

  Tulilaani raia wazalendo wa Afrika kusini kuhamishwa toka makao yao ili kuwapisha wazungu. Leo mzalendo wa Kitanzania akihamishwa kwa mabavu na polisi ili wawapishe wawekezaji (wazungu) toka nje, na hata akiuwawa katika kuhamishwa huko, tunaona sawa.

  Kwa nini isiwe sawa kwetu kwa wananchi kubaguliwa na wazungu kule Msumbiji, Angola, Namibia, Afrika kusini lakini iwe sawa kwa wazalendo Watanzania kubaguliwa ndani ya mipaka ya nchi yao?

  Kwa nini isiwe sawa kwa polisi kuwapiga risasi za moto waandamanaji wasio na kibali kule Sharpeville, Soweto na mitaa mingi ya Afrika ya kusini lakini iwe sawa kwa polisi wetu wenyewe kufanya hivyo Mbeya, Arusha, Songea na kwingineko?

  Kwa nini tushindwe kuvumilia ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa polisi nje ya mipaka yetu na hata kujitoa muhanga kuwakomboa jirani zetu na baadaye tiyavumilie nmaovu hayo hayo yanapofanywa ndani ya mipaka yetu wenyewe?

  Lazima tuwaulize viongozi wetu watupe majibu.

  Lazima tuwaeleze wananchi kwamba haya yote hayakuwa sawa nje ya mipaka yetu, na si sawa ndani ya mipaka yetu

  Lazima tueneze ujumbe huu ili kuonyesha kwamba tuna viongozi ambao ni viongozi kwa maslahi yao wao binafsi.
   
 2. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Umeandika mambo makuu na ya msingi mno. Wananchi walio wengi wanasoma matukio haya ya kinyama kwenye magazeti tu na hiyo haitoshi kuwaamsha ili wapambane na udhalimu uliopo nchini.
  Video ni njia yenye nguvu sana kuweza ku-connect na hisia za mtu kwa sababu video inakuonyesha utendekaji wa kitendo kana kwamba wewe mtazamaji upo kwenye tukio lenyewe.
  Je, kuna uwezekano wa video za matukio haya kupatikana na kusambazwa kwa wananchi ili ziwachochee waamke na kuwatwanga polisi na viongozi wao washenzi? Dawa ya moto ni moto, naamini wananchi wakifanikiwa kuua polisi kadhaa adabu itaanza kupatikana.
   
 3. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Massenberg, nakuelewa hasira yako juu ya unyanyasaji unaofanyika ndani ya nchi yetu. Hata Nyerere na Mandela waliwahi kusema kwamba ikiwa njia za amani zinashindwa kuondoa unyanyasaji, basi wanaonyanyaswa wanakuwa na haki ya kutumia silaha.

  Ila siamini kwamba Tanzania tumefikia hatua ya moto kwa moto. Bado tuna namna nyingi tu za kumaliza unyanyasaji bila kutumia nguvu, japo nakiri kwamba suala la baadhi ya watu kupoteza maisha litatokea; iwe katika mambo ya kawaida ya kutumia nguvu ya sanduku la kura au kwa namna ya maandamano kama ya Songea. Katika suala la sanduku la kura kuna watu ambao wanajiona ni "wateule wa kuwa viongozi", ambao watafanya kila wawezazo kupata uongozi, kutia ndani na uuaji.
   
 4. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakupata vizuri, lakini kuna mambo mawili ya kuzingatia:
  1 - Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo hali inazidi kuwa mbaya na unyama unazidi, ni heri ufa ukazibwa kabla haujaangusha ukuta mzima.

  2 - Tofauti na binadamu wengine, Waafrika tumedhihirisha kuwa hatutawaliki kwa utaratibu wa demokrasia (kama ambavyo tunaelewa maana yake). Sisi ni watu wa kushurutishwa na kutwangana mangumi tu, hakuna lugha nyingine tunayoielewa.

  Hakuna uwezekano wa haki kutendeka Tanzania kwa kutegemea sanduku la kura au sijui upeo wa wananchi kukua. Katika masuala haya adui yetu ni muda, hatuna muda kusubiri wakati ushenzi unafanywa kwa makusudi.
   
 5. K

  Kibakamande Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ipo siku yatakwisha tu.
   
 6. d

  dav22 JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nadhani hili ni suala ambalo linakuwa ishu hapa kwetu maana kila siku polisi wanatumia extra power ...
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Synthesizer,
  Those were the days. Muhimu sasa hivi ni kuendeleza mapambano na baada ya ukombozi, wauaji wote hawa wafikishwe kwenye vyombo vya haki. Said Mwema na kampuni yake wanayo maswali mengi sana watakayotakiwa kujibu. Tusije ishia kuundiwa tume za maridhiano.
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu umegusa mahali muhimu sana watawala wetu wamesahau waliowachagua,na pia wamesahau kuwa wananchi wanaguvu kuliko wao.Tuendelee kupambana hadi wajue wananchi tumechoka,poleni sana wanaharakati wote waliokufa kwa risasi za moto ile hali wakidai haki za wengi,MUNGU atawalipa kwa sehemu mliyoichangia,hope mmekuwa mbegu muhimu ya mabadiliko katika nchi.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Yatakwisha lini wakati ndio kwanza yanaanza?
   
 10. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu natumia simu,ila nime like ili wazo
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  tupo kwenye kipindi cha mpito.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..mara nyingine watanzania tuna huruma sana na maisha ya watu wengine kuliko yetu wenyewe. mfano mzuri ni hii Jumuiya ya Afrika Mashariki[EAC] ambayo kwa kiwango kikubwa iko kuzifaidisha nchi nyingine kuliko Tanzania. Inawezekana pia tunapenda mno kusifiwa-sifiwa na wenzetu.
   
 13. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Ni kweli mie nasikia uchungu sana nikiona haya yakiendelea nchini mwetu. Hasa kwa Watanzania kufanyiwa ubaguzi wa rangi na wageni na sasa hili la Polisi kuua raia kwa risasi. Leo nimesikika kichefuchefu kusikia Polisi wanne wametiwa mbaroni Songea, wakati RPC ambaye alikuwa anatetea utumiaji wa risasi za moto yuko anapeta tu.

  Tunahitaji mabadiliko makubwa sana.
   
Loading...