Tulikuwa bado tunamhitaji BENJAMIN MKAPA kama Raisi wetu kwa maeneleo yetu

ni kweli kwa kuchechemea huku taifa letu linakopitia we still someone with a strong character like danger man, but what is gone is gone, we now need good governance for survival of our country so that we can be served from the state of death
 
ukiishi na watu, kuishi kwingi kuona mengi. Utagundua kwamba suala la uongozi thabiti, uwezo wa kupambanua darasani, na uwezo wa mtu ktk mambo mbalimbali hayana uhusiano wowote na utanashati au sura ya mtu. Watanzania wengi wanaponzwa na mvuto wa mtu pasipo kuangalia uwezo wa mtu! Inauma lakini ndio tumefika hapo!
Hata hivyo, kwa ujumla, katiba tunatakiwa tuiweke namna ambavyo itatufanya kiongozi aingie madarakani kwa uwezo wake si kwa uwezo wa kifedha. Maana kwa mfumo uliokuwepo ktk CCM, hata wasio na fedha walihitaji kupata support ya mafisadi, na bahati mbaya rushwa ya pesa na ngono ni vitu ambavyo vinaondoa sana 'independence' (hali ya mtu kufanya mambo kama yeye) ya mtu.
 
Mwizi tu huyu! Kule China kwa ufisadi alioufanya alipokuwa madarakani hata kizimbani wasingempandisha ili kutokupoteza muda. Ukiuliza alichokifanya ni kipi katika kuinua viwango vya maisha ya Watanzania watu wanaanza kung'aa macho. Mishahara haikuongezeka, Watanzania wengi walikuwa bado wanaishi maisha ya dhiki iliyokithiri, Mashule yetu mengi yalikuwa hayana hadhi ya kuitwa shule na wanafunzi wengi bado walikuwa wanakaa chini au kwenye matofali, hospitali nyingi zilikuwa hazina dawa, vitanda au vifaa muhimu vya kutendea kazi na hata wajawazito walikuwa wakilala chini au kushare kitanda wakati mwingine kitanda kimoja kwa wajawazito hata saba!

Alifanya biashara akiwa Ikulu pamoja na kuwa alikuwa na mshahara mkubwa pamoja na marupurupu chungu nzima, alifanya ufisadi katika kulazimisha kununua rada ya $42 million, alihusika na wizi wa EPA ($133 million) ambao ulitokea akiwa madarakani, alihusika pia na kagoda na meremeta maana alikuwa yuko madarakani, alilazimisha kwa mtutu wa bunduki kuwaingiza Net Group katika kuendesha TANESCO na kuwalipa mabilioni chungu nzima pamoja na kuwa walikuwa hawajui chochote kuhusu umeme, alishiriki katika kuuza mashirika yetu mengi kwa bei ya kurupa kwa kile alichokiita ubinafsishaji kwa mfani ile NBC ambayo ilikuwa na thamani kubwa aliiuza kwa shilingi 15 million tu wakati ilikuwa na thamani kubwa sana, alihusika na kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa uamuzi ambao umeshaingiza Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 200, alihusika kusaini mikataba ya kifisadi ya kuchimba madini yetu na kisha kuificha ili Watanzania tusijue details za mikataba hiyo ambayo tunapata 3% na wachukuaji wanachukua 97% wakati wale jirani zetu wa Botswana wanagawana sawa sawa na wawekezaji (50%). Aliongwza kwa kiwango kikubwa ukusanyaji wa kodi lakini asilimia kubwa aliitumia katika kulipa madeni ya nje badala ya kuboresha maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa. Aliiba Kiwira Coal Mining pamoja na kiwanda na shamba kule kilombero kwa kutumia wadhifa wake kama Rais.

Hahitaji kusifiwa kwa chochote huyu bali WIZI tu aliingia madarakani akiwa sio hata milionea lakini katika miaka 10 aliyokaa madarakani alikwapua mali nyingi za Watanzania na kuweza kuwa bilionea lakini bado baadhi ya Watanzania hawauoni ufisadi alioufanya Mkapa!!!! Kweli baadhi ya MIAFRIKA ndivyo ilivyo!!! itasifia hata kile kisichostahili kusifiwa!
 
its true ni kweli Mhe. Ben aliifanya Taasisi ya Urais iwe na heshim a ya dhati.

na kama alikuwa akilisimamia jambo basi lazima lifanyike.Infact kiuchumi aliiweka nchi mahali fulani pa kusimamia ithink he needed more time at least ten years more perhaps nchi hii ingekuja walau kuifikia KIDOGO HATA Botswana kimaendeleo.

Though kuna mambo yaweza kuwa aliboronga lkn to much extent aliutengemaza uchumi wa nchi
 
Hamna shaka watanzania badowana mapenzi ya dhatikwa raisi mstaafu Mkapa, pamoja na matatizo yake yote katika utawala wake ,alijipambanua kama kiongozi jasiri,sio mnafiki aliyekuwa na vision ya dhati ya kujenga Tanzania, tulikuwa bado tumhitaji MKAPA.

Yaani pamoja na kujimilikisha mgodi wa taifa na kufaya biashara ikulu wewe haujachoka tu!!!
 
Kinachotutesa hapa sio mtu au watu; ni mfumo uliochakaa wa CCM. Muhimu ni kwamba watanzania tulipaswa kuwa tumeshaifukuza CCM jana sio leo. [
 
Tatizo la ufisadi ni la kimfumo maana kila raisi wa Tanzania ni fisadi kianiana maana kuna ulazima wa kubadiki katiba ya taifa hili na kuona jinsi gani ya kufanya jinsi ya kufanya ili tuwe na rais accountability kwa watu
 
safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!public enemy no.1 miaka mitano ya mwanzo aaaaaaah,alifanya vizuri lakini ile mitano ya mwisho wenye akili za kifisadi walimvaa wakamsomesha wakimsadikisha kuwa atatoka masikini baada ya miaka yake mitano kumalizika akakubali tabia ikabadilika kabisa akawa mjeuri,kiburi kingi,majibai,mkaidi vitisho etc.Bora kama bado unamhitaji basi awe raisi wako nyumbani kwako.:dance:
Vonix nakupa 100% kaudokozi kamemshusha hadhi sana huyu chinga
 
Mkapa ndio source ya maovu nchini(ufisadi)
Mmesahau ANBEN?
Kufanya biashara IKULU,

Brainiwashing is not good at all
 
sio uzuri wa mkapa bali ni udhaifu wa ****** unaomfanya BWM aonekane bora. Fundisho la msingi hapa ni kwamba tuwe makini kabla ya kumpeleka mswahili yeyote ikulu kule magogoni
 
Hamna shaka watanzania badowana mapenzi ya dhatikwa raisi mstaafu Mkapa, pamoja na matatizo yake yote katika utawala wake ,alijipambanua kama kiongozi jasiri,sio mnafiki aliyekuwa na vision ya dhati ya kujenga Tanzania, tulikuwa bado tumhitaji MKAPA.

Don't be cheated, hawa jamaa hawako tofauti,wanapokezana vijiti.Kikwete anaendeleza agenda alizo acha Mkapa.
 
Alikuwepo Mzee Nyerere (miaka 24)...alipoondoka kuna wanazi wanaimba kwa sauti kwamba tulimhitaji wengine tukasema afadhali ameondoka na ujinga wake

Alikuwepo Mzee Mwinyi (miaka 10)... alipoondoka kuna wanazi wake wanaimba kwa sauti mzee huyu alikuwa bora sana muungwana wengine tukasema afdhali aondoke na upole wake tumechoka

Alikuwepo Mzee Mkapa (miaka 10)...alipoondoka wanazi wake wanaimba kuwa alikuwa na akili, mkali na rais bora wengine tukasema afadhali aondoke na uwizi wake, ubabe wa kijinga, akiwemo Ulimwengu ok..

Atakuwepo Mzee Kikwete (miaka 10 InshAllah).. ataondoka wanazi wake wataimba alikuwa msikivu, mpole na muungwana na wengine tutasema afdhali aondoe uwoga wake, upole wake n.k

Binadamu ndivyo walivyo wanapenda jua, baridi, mvua, kiangazi nk...
 
Kinachotutesa hapa sio mtu au watu; ni mfumo uliochakaa wa CCM. Muhimu ni kwamba watanzania tulipaswa kuwa tumeshaifukuza CCM jana sio leo. [

Kitila, mbola unashangaza sana, sasa kama CCM haikufukuzwa jana unataka leo pia isifukuzwe? Kumbuka kila jambo linawakati wake muafaka kufanyika. suala la kuifukuza CCM huu ndio wakati muafaka kabisa. naomba utambue hilo na kukubaliana na hali hii
 
Back
Top Bottom