Tulikotoka: 'Marais wastaafu wanavyoifilisi nchi yetu'


M

mwanaizaya

Senior Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
134
Likes
0
Points
0
M

mwanaizaya

Senior Member
Joined Apr 26, 2008
134 0 0
Tulikotoka: 'Marais wastaafu wanaifilisi nchi'

*Watumia mamilioni kila mwaka
*Salim Ahmed Salim naye atengewa zake

Dodoma, Agosti 4, 1998

MARAIS wastaafu ni miongoni mwa viongozi ambao wameelezwa kutumia fedha nyingi za walipa kodi hali inayotishia kufilisi nchi na kuzorotesha huduma muhimu za jamii.

Akichangia hotuba ya makadirio ya matumi ya fedha ya Waziri Nchi Ofisi ya Rais Utumishi ya mwaka 1998/99 bungeni jana, Waziri Kivuli wa Utumishi, Bw. Seif Mohamed Azzani, alitaka Serikali kupunguza gharama za kuwakirimu viongozi hao kulingana na hali ya uchumi wa Tanzania.

Bw. Azzani aliainisha gharama hizo kuwa ni kwa ajili ya matumizi ya simu, samani, maji na matengenezo ya magari kwa marais na makamu wa Rais wastaafu.

Aliongeza kuwa kila Rais Mstaafu anagharimiwa na Serikali sh. milioni 7.2 kwa ajili ya simu, sh. milioni 14.4 za kwa ajili ya matengenezo ya magari na sh. milioni 1.2 kwa gharama za maji kwa mwaka.

Alisema kuwa kila Makamu wa Rais Mstaafu analipwa sh. milioni 4.8 kwa ajili ya simu, na kutoa mfano wa sh. milioni 1.5 kwa simu za Dkt. Salim Ahamed Salim, ambaye ni Katibu Mkuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (OAU) ambazo ni kubwa mno kulingana na uchumi wa Tanzania.

Alihoji inakuwaje Dkt. Salim ambaye anatumikia OAU kulipwa gharama hizo na Serikali wakati angeweza kulipwa na mwajiri wake?
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,407
Likes
5,796
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,407 5,796 280
Du hapo ndipo wabunge wetu walipochemka sana kwa kweli...ingekuwa bora walipwe zote in lump sum...one and for all....maana hivyo ni balaa baada miaka 10 wanazidi kuongezeka na mzigo mkubwa sana kwa serikali...ila wabunge wana ubavu huo wa kubadilisha pensheni kwa wakuu wa nchi wastaafu?
 

Forum statistics

Threads 1,238,346
Members 475,888
Posts 29,317,597