Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Mtu aliyepotea njia hajitendei haki kwa kuendelea na njia ile ile aliyopotea akitegemea kuwa kwa "bahati" ataweza kufika kule anakotaka kufika. Tanzania tuliyo nayo leo hii ni matokeo ya safari yetu tangu uhuru, safari ambayo bila ya shaka imetufikisha hapa.
Hata hivyo swali ambalo siku moja litahitaji kujibiwa ni kama hapa ndipo tulipotaka kufika? Je safari yetu ya miaka 45 na zaidi ilikuwa na lengo la kufika hapa au kuna mahali tumeenda pembeni?
Binafsi naamini kabisa kuwa kuna mahali tulikosea katika safari yetu na toka hapo tumekuwa tukienda tu "alimradi" tufike lakini hatujajiuliza "ni wapi tulikopaswa" kwenda na kama hapa tulipo ni sehemu ya mwelekeo wa huko tulikotaka kwenda.
Tulipotaka kujenga Taifa la "watu walio huru na sawa" na Taifa ambapo "kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" hiki tulichonacho leo ndilo Taifa lile tulilolitaka? Matukio ya Tabata siku chache zilizopita ambapo watawala kwa nguvu ambazo waliamini wanazo waliamuru na kwenda kuvunja nyumba za watu na baadaye kugeukana hayana budi kutuuliza kama hili ndilo Taifa tulilolitaka kulijenga?
Licha ya kuwa taifa linaadhimisha wiki ya maji lakini bado baadhi ya wananchi hawapati maji safi na salama, pichani ni mkazi wa kijiji cha Goba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Asma Ali akichota maji katika moja ya visima vilivyopo kijijini hapo jana kwa matumizi ya nyumbani. (Picha na Mroki Mroki)
Picha kama hiyo hapo juu inaelezea kwa kina mahali ambapo tulipo leo hii, hasa tukilinganisha na hii nyingine katika Jiji hilo hilo moja.
CENTER]
Kama hili ndilo Taifa tulilolitaka kwanini tusikubali yaishe tu na kufurahia "uzuri wa nchi yetu", kama silo lile hasa tulilolitamania kiasi cha kuamua kudai uhuru, tufanye nini basi kujenga Taifa tunalolitaka?