Tulijuwa na kweli imekuwa, je itakuwaje 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulijuwa na kweli imekuwa, je itakuwaje 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TumainiEl, Oct 21, 2012.

 1. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,896
  Likes Received: 1,657
  Trophy Points: 280
  Tulijuwa na kweli imekuwa je tutegeme nini 2015 ni mawazo yangu binafsi nikiunganisha na mawazo ya wazee wetu waliokwisha tangulia mbele za haki. Taifa letu Tanzania ktk kipindi hiki linapita kipindi kigumu na cha dhiki ambacho uwenda hakijawah kutokea tangu kuzaliwa taifa hili 1961. Haya tunayo yaona na yale tutakayo yaona ni mwanzo wa utungu tu ila bado mtoto hajazaliwa, lakini kinachosikitisha sana viongozi waliopita waliyajuwa haya na uwenda yaliwasumbua sana mioyon mwao lakini at the last yametokea. Taifa hili leo linashuhudia idadi kubwa yawatu wasio kuwa na ajira na uwenda hata wale wana ajira zikawa matatani kutokana na uchumi ulioharibika chini ya mkuu wetu japo walijuwa na kweli imetokea. Taifa hili limepata mpasuko mkubwa ktk umoja wa kitaifa, vijana hawana uzalendo, pia muungano ndio kabisa wanataka kuuvunja hata leo lakini walijuwa na kweli imetokea. Taifa limekosa dira na mwelekeo na sasa tunashuhudia mvutano mkali kati ya wakristo na waislam ila embu jiulize hawakujuwa haya? Lahasha walijuwa na kweli imetoke. Sekta ya fedha imetoka ktk ma bank nakuwa ya makampuni ya simu wakati mabank yaki haha jinsi yakupata wateja na ukwasi? Je hawakujuwa haya? Walijuwa na kweli yametoke. Ktk kipindi ambacho sisi watanzania tukisubiri maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa maisha bora kwa kila alie na nafasi ndani ya serikali wakati wengi masikini wakiwa mafukara wakutupa. Je chama tawala na yale yanaendelea hawakujuwa? Bila shaka walijuwa ila nilazima watanzania wajuwe ipo siri nzito tusio ijuwa inaendelea ndani ya chama hiki ili kushika hatam 2015, je ni siri gani? Hiki ni kiza kinene kinacho endelea ila napenda kusema siri itafichuka 2014 kama sio 2013. Nilazima watanzania wajuwe hii nchi ipo chini ya Yeye alio ifanya na hakuna mpango wa mwanadam utafanikiwa, 2015 nilazima watanzania wajuwe jambo litatokea nalo litaleta ukimya mzito na watu watajuwa Mungu yupo. Thanks.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Thanks for sharing with us
   
 3. M

  MVENGEVENGE Senior Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mambo mazito umetamka katika jamv,i ili kuweka sawa thread yako tuweze kuchangia kwa unyofu funguka zaidi katika hiyo siri nzito.
   
Loading...