Tuliharibiwa: Madhara ya Ufisadi Yanaonekana katika Masalia ya Fikra Za Watu Wetu

Kwa maoni yako Ufisadi umeacha madhara makubwa kwa taifa hadi sasa?


  • Total voters
    58
  • Poll closed .
mmmh.. lazima usome picha usione tu JPM anakuchekea itakula kwako... hoja muona Rostam anaimba mwenyewe "kidumu chama cha mapinduzi"... yuko kwenye hali mbaya sana jamaa.. na siku akitiwa pingu msije kushangaa "mbona alikunywa naye chai"...
Ruksa kuota mchana.
Ufisadi upo tena sana tu. Rushwa ipo tena sana tu.
Kwanza inaonekana wewe huna uhusiano na hali halisi kwenye uwanja wa mapambano. Unaandika kutoka hewani.
Kwa walioajiriwa sekta ya umma, morali ya kazi imeshuka sana.
Rushwa ndani ya jeshi la polisi ipo pale pale au imeongezeka. (nimeshuhudia jamaa akitoa rushwa kituoni mbele ya maofisa zaidi ya wanne)
Jambo lingine la kukupa hint kwamba kuna ufisadi unaendelea nchi hii ni kupungua kwa demokrasi na transparency. Shetani hufurahia giza ili uovu wake usionekana kirahisi.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

View attachment 949427

Tulizaliwa katika mfumo wa kifisadi; tulikua na kuishi katika mfumo huo, na tulikufa tukiujua mfumo huo peke yake. Ndani ya mfumo tulienda na tukawa; watoto wetu na wajukuu wakaukuta mfumo na kuamini ndio maisha pekee wanayoweza kuishi. Ili mtu afanikiwe alitakiwa awe fisadi mwezeshaji au fisadi mwezaji.
Tulitengeneza taifa la mafisadi wakongwe na mafisadi vijana; mafisadi waliopo na mafisadi watarajiwa.

Ndugu zangu, madhara ya maisha haya sasa yanaonekana. Lakini tuweze kuelewa madhara yake ni vizuri kujua kabisa kuwa mfumo huu wa maisha uliwafanya watu waishi, jamii iende, nchi ionekane inakwenda n ahata pale ambapo haikwenda tulifisadiana katika kusaidiana kuifanya ionekane inaenda.

Ufisadi ulikuwa ni sehemu kubwa ya maisha kiasi kwamba watu walipanga bajeti za maisha na maendeleo na ndani yake waliweka bajeti ya ufisadi kukamilisha ndoto zao. Ukitaka kupata kibali cha shilingi 10,000 lazima utenge angalau 50,000 za kulainisha mikono ya watu. Ukitaka kujenga nyumba yako yenye gharama ya milioni mia moja gharama yake halisi ilikuwa kama milioni mia na hamsini – hamsini za kufanikisha mambo yako mbalimbali na yafanikiwe.

Hili lilikuwa kweli katika elimu, maji, afya, huduma mbalimbali na katika ngazi mbalimbali. Ufisadi ulikuwa ni sehemu ya maisha kuanzia kwenye kata vijiji hadi tarafa, wilaya hadi mikoa na tukaona ufisadi kutoka mikoa hadi taifa. Tukazoea kuishi kwenye maisha ya kashfa kubwa kubwa kama vile tunalazimishwa kuishi kwenye maji kama samaki; bila kashfa kubwa nchi ilikuwa haiendi. Kuanzia kashfa za kina Valambhia hadi kufika kina Rostam, kuanzia za kina Iddi Simba hadi Rugemalira Watanzania walizoea ufisadi na ufisadi uliwazoea Watanzania.

Tulicheka na kuchekeana katika ufisadi, tulizoea na kuzoeana , kubembeleza na kubembelezana huku tukisha na kushikana huku tukikodoleana na kutishana! Ufisadi ulikuwa kama dini iliyotuuunganisha, tukipiga magoti na kutoa dhabihu zetu za kushukuru mbele ya mafisadi katika madhabahu yao. Ukitaka kufanikiwa lazima umjue au umjue anayemjua anayejulikana. Ufisadi tungeweza kuuimbia nchi “ooh ufisadi wajenga nchi!” Na tuliamini ufisadi kweli kabisa unajenga nchi. Hata kama tuliulaani hadharani na kuwabeza mafisadi.

Uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni ni uchaguzi wa ama kuendelea na maisha yale au kubadilisha mwelekeo. Ulikuwa ni uchaguzi wa kati ya kutamalaki kwa ufisadi au kuvunjwa vunjwa kwa madhabahu ya dini hiyo yenye watu wenye dini zote! Imani ya dini hiyo ni tumbo na kitabu chake kimeandikwa kwa maandishi ya tamaa. Uchaguzi ule ulikuwa ni wa ama kuendelea na tulivyokuwa tukiishi huku tunafurahi katika ufisadi wetu; hakuna maamivu ya moja kwa moja kila mtu akiishi kwa kujifurahisha mwenyewe na familia yake.

Ulikuwa ni uchaguzi wa kuamua kama tunataka kuuvunja mfumo huo haramau au kuulea kidogo kwa sababu tumeuzoea.

Tuliokuwa tumedeka kwenye mfumo huo hatukuweza kufikiria namna nyingine yoyote ya kuishi. Ni kama mtoto anayetoka kwenye familia iliyomdekeza na siku moja anaambiwa hakuna vya bure tena shika jembe ukalime. Mtoto yule anapolima kidogo tu mikono yote inamuuma na kuanza kuchubuka huku ikitokea malengelenge! Machozi yatamlenga na kujiuliza kumbe “kilimo ni kigumu hivyo”.

Hili linanikumbusha nilipoenda kuanza shule ya Sekondari miaka mingi nyuma kwenye shule ya Wazazi ya Boza, Pangani Tanga. Nakumbuka mtoto mmoja binti wa familia ya kitajiri aliyeletwa bweni kuanza maisha na kupaona mahali penyewe palivyo (wakati ule). Binti yule aliangusha kilio gari la wazazi wale lilipoondoka kumuacha na kwa karibu wiki nzima alikuwa hana raha mtoto wa watu, akigoma kula na tunashukuru Mungu hakukuwa na Facebook wala Whatsapp enzi hizo, wala Instagram! Kilichomsaidia binti yule (msema kweli Mpenzi wa Mungu) – ni kuwa alijaliwa “Neema za Allah” na vijana wengi (mimi si mmoja wapo) walijitolea kumsaidia kwa kazi zake mbalimbali – hasa ilipofika zamu ya kwenda kubeba kuni!

Baada ya muda alizoea, akazoea maisha ya kule kwani asingeweza kuwapa vijana wote vile walivyohitaji bila ya kujichafua jina lake. Miaka minne baadaye alipohitimu binti yule alikuwa ni “mama” akiwasaidia mabinti wengine walioifika pale na baadaye akaja kuolewa na mlalahoi mmoja. Aliingia shule akiwa hajui jinsi ya kushika kijiko, alihitimu akijua kushika mwiko; aliingia akiwa na madaha, alitoka akiwa na staha.
Ndugu zangu, ufisadi ulikuwa ni kama dawa ya kulevya; taratibu taratiu watu wakauzoea na mwisho wa siku wakata arosto.

Uchumi wetu na maisha yetu kama taifa na kama mtu mmoja mmoja yalihitaji dozi ya dawa hii ya ufisadi ili mambo yaende. Alichofanya Magufuli na ambacho anaendelea kufanya (japo naona kama mwendo umepungua kidogo) ni kuwakatisha watu kupata dawa hii haramu. Matokeo yake watu sasa wako katika hali ya kuonesha withdrawal symptoms. Yaani, watu sasa wanagundua kuwa hawawezi kuishi bila kupata kitu kidogo kwenye damu zao. Kuna wengine ambao wanaona labda asingefanya kwa ukali hivi kwani wakati mwingine mtu anapokatishwa kutumia madawa kwa ghafla anaweza kuishia kuumwa sana na hata kufa! Je, Magufuli angefanya taratibu, abembeleze, asiguse sana uchumi na aachie achie kidogo ili watu wasiumie?

Ndugu zangu, leo hii wapo watu wanapata shida. Kuanza kumomonyolewa na kubanduliwa kwa mfumo wa utawala wa kifisadi kunawafanya watu wakose pa kushikilia. Wenye kulia wanalia, wenye kuumia wanaumia lakini nawaambia kwa uthabiti kabisa wa moyo kuwa hakuna wakati muhimu sana kwa historia ya Taifa letu kama wakati huu. Miaka hii mitatu ya mwanzo ya Rais Magufuli inanithibitishia kabisa kuwa tulichelewa sana na sasa maumivu tunayoyaona ni maumivu ya mtu aliyechelewa kupata tiba na sasa analazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa; si mchezo, si lele mama.

Miaka hii mitatu ya kujaribu kuvunja ufisadi, kujenga taifa la watu wanaojiamini na kujitegemea kifikra si jambo rahisi. Makosa yatafanyika, matatizo mengine yataibuliwa, vingine vitaharibiwa lakini kiujumla wake maisha yataenda tu ndugu zangu. Hata wagonjwa wanapofanyiwa upasuaji si wote wanapona na wakati mwingine kunatoke “complications” lakini nia na uthubutu wa madaktari hauwezi kupuuzwa au kubezwa.

Miaka mitatu baadaye ninapoangalia taifa letu linapokwenda sina sababu yoyote ya kujuta kukata marudio na mwendelezo wa mfumo wa utawala wa kifisadi. Sina majuto ya kuunyoshea kidole na kuukataa hata kama ungerudishwa kwa kisingizio cha “mabadiliko” ya kuzungusha mikono. Mambo yote leo yanafanyika nilivyotarajia? La hasha! Kuna vitu ambavyo ningependa vifanyike na havifanyiki au visifanyike na vinafanyika? Si kidogo! Lakini, kutengeneza nidhamu mpya, njia mpya na mwelekeo bora wa kitaifa linafanyika? Bila ya shaka!

Miaka miwili ijayo, itatupa mwanga zaidi; tutaona zaidi mafanikio ya utawala huu na nina uhakika Watanzania wengi zaidi – pamoja na maumivu na usumbufu wa sasa – watasimama na kusema tunahitaji miaka mingine mitano. Gharama ya kujenga mfumo wa maendeleo ni kubwa sana na tumeanza kuilipa. Nina uhakika yatafanyika masahihisho ya maeneo yanayosumbua sasa hivi. Tusije kuthubutu kuangalia nyuma na kutamani kule tulikotoka. Tukatae kabisa kuambiwa ati wakati wa Kikwete na Mkapa ulikuwa ni mzuri sana kwa sababu tulikula “nyama, matikiti maji na vitunguu saumu”.

Kwamba, kwa vile tuliishi katika Misri ya Ufisadi basi ilikuwa nzuri kwa sababu tulikuwa salama na wenye Amani. Tuwakatae na kuwapinga wanaotaka tukumbuke Misri ile ati tu kwa vile huku kwenye nchi ya ahadi kumbe tunatakiwa kufanya kazi, kuhenyeka na kufanya kazi kama uhai wetu unategemea.

Tusonge mbele kwa jitihada, ufanisi, na uwajibikaji. Tukifanya tunachopaswa kufanya basi kile tunachokifanya tutaona kweli kinatupasa!

Niandikie: klhnews@gmail.com
Aisee ni uongo, beurocracy imeongezeka sana, of coz in some area ambako interest za watu ni kwa uchache rushwa inaonekana kama imepungua, ila Rushwa ipo na bado mazingira yake yanapaliliwa vizuri kabisa, tungetengeneza mfumo mizuri na rahisi kufuata ofcoz ingekungua significantly
 
Sikiliza mkuu, hata kama tungesema kuwa Rais Magufuli amezitumia hizo fedha, wewe unafikiri zitakuwa zimeenda wapi? Au amezitumia kwenye madhumuni gani?

Ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba hata kama hizo hela amechukua basi nafikiri hata wewe utakubaliana na mimi kuwa anaweza akawa amezitumia katika miradi ambayo ina malengo ya kuwanufaisha watanzania kama; kufufua shirika la ndege Air Tanzania kwa kununua ndege mpya saba au baadhi ya pesa hizo labda kutumia katika kujenga na kuboresha kiwanja cha ndege cha Chato.

Sidhani kama kuna mtu ulimwengu huu anaweza lalamika kuwa Rais Magufuli hizo trilion moja point tano, kama kweli ziko, atakuwa amezitumia kwa manufaa yake binafsi, kama may be kuzichimbia kwenye mabank ya kigeni au katika miradi yake binafsi. Sijawahi sikia Rais Magufuli ana miliki kampuni au ana hisa za mabilion ya fedha katika mashirika na makampuni nchini na nje na kadhalika. Rais ambaye ameshindwa hata kumpeleka dada yake mpendwa Indian au Ulaya kwa matibabu mpaka amefariki, leo uje ummpe lawama ya kuwa amefanya ufisadi wa TSH 1.5 trilioni, hiyo sidhani kama ita kuwa imekaa sawa sawa. Tutakuwa tuna mwonea.

Tatizo letu watanzania wengi wetu tunakosa mawazo ya kufikiri nje ya Box. Serikali zote dunuani ambazo zina jali maendeleo ya wananchi wake, lazima zibuni miradi mbali mbali ili wananchi wake wapate ajira na kulifanya taifa lake liwe vibrant. Miradi kama ya SGR, Stiegler's Gorge, Upanuzi wa bandari na kuhamisha wizara za serikali kwenda Dodoma hizo zote ni mbinu moja wapo ambazo serikali ya Magufuli imebuni ili kuleta maendeleo ya nchi, badala ya kuwapa wananchi pesa za bure, kama serikali za awamu hizo nyingine zilizopita zilikuwa zikifanya, hii serikali imeamua kuchochea maendeleo yetu kwa ubunifu huo wa miradi mbali mbali.

Wote tunajua mtu ukimzowesha kumtengea chakula maisha yake yote matokeo yake huyo mtu hawezi kuwa creative. Anadumaa kiakili. Inaeleweka kuwa maendeleo ya binadamu yanaletwa kwa kupanuka kwa Ubongo. Ili ubongo uweze kupanuka unatakiwa uchemke kidogo, kwani hapo ndipo uwezekano wa ku-create new neurons unatokea. Creation of new neurons has an impact on forming of an integrated nerve system ambayo as a result ina mfanya binadam kuwa inquisitive na hivyo kupata uelewa mkubwa wa mambo mengi yanayo tokea kwenye environment ambayo inayo mzunguka na challenges anazo kabiliana nazo.

Juhudi hizi zote za kuchochea maendeleo ya binadam zinafanywa na watu wanao julikana kama Great Thinkers kama; Rais wetu wa sasa Dr John Pombe Joseph Magufuli na Hayati Mwalim Nyerere.
Hawa ndiyo wazalendo wa kweli.
Umeandika risala ndefu bila content ya maana.
Katika yote, Pombe sio great thinker. Hiyo sifa hana; hata kwa kusingiziwa tu. Ni mkurupukaji tu.
 
Msingi wake ni pale mheshimiwa hakuonesha kuguswa kwa namna yoyote na jaribio lile la mauaji na mpaka leo hakuna arrests wala uchunguzi wa maana ukiofanyika. Pili, msneno na matendo ya mh kabla ya tukio mfano "kumwita Lissu msaliti n.k." haya yote yanajenga msingi wa hoja kwamba anahusika kwa asilimia 90. Kama sio serikali yake basi alipaswa kuonesha na kudhibitisha hilo.
i
Unaandika ukiwa na assumptions kubwa sana ambayo sijui msingi wake ni nini...
 
Kwa akili zako Mzee Mwanakijiji Jiwe anapambana na ufisadi au anapambana na mahasimu wake wa kisiasa wanaotishia kukitwaa kiti alichokikalia?Akiwapachika Jina baya la mafisadi wanaotumiwa na mabeberu!
 
Hata magufuli aliishi katika mfumo huo naye ni ngumu kujinasua sababu anatabaka lake tayari la kina makonda ambao ni master mind wa mission to be possible by any means..imefika mizizi komavu imeingia mizizi king'ang'anizi hakuna rangi tutaacha ona ..safari ndo kwanza imeanza
Wamejificha kwenye jina lao pendwa la uzalendo
 
Matusi au kejeli haijawahi kujibu hoja zangu; inaonesha tu ama huna uwezo wa kujibu hoja au hoja zimekuzidi na badala yake unaongozwa na hasira na husuda... hoja hujibiwa kwa hoja.. unafikiri utawala wa Kikwete na Mkapa ulikuwa bora kuliko sasa?
Mkuu MKJJ, unashambuliwa kwa vile kile unachokiona wengine hawakioni.

Anyway, Lakini, kama lengo lako lilikuwa ni kuwalinganisha BM, JK na JPM na ulitaka watu wajadili hilo basi ungeweka hilo wazi. Maana tulikotoka Maraisi walikuwa ni zaidi ya hao, kulikuwa na JKN na AHM. Kwa hiyo kama unazungumzia kuziliwa, kukulia na kufia kwenye huo mfumo wa ufisadi, sioni ni kwa jinsi gani JKN na AHM wanakosekana kwenye mjadala!! Huo mfano ulioutoa kuhusu huyo binti, ni wa kizazi cha JKN ana AHM. Na wengi wao hawakuwa hivyo kwa sababu ya ufisadi wa wazazi wao bali kwa sababu ya malezi kutokana na vyeo vya wazazi wao. Enzi hizo pia niliona msichana anahama shule fulani ya serikali kwenda private school kwa ajili ya kuogopa kulima. Kuna watu walikuwa wanapewa na serikali almost everything na shuleni wanapelekwa na kuchukuliwa na gari la serikali.

Tukirudi kwenye point, ni lazima tukubali kuwa kila binadamu ana mazuri yake na mabaya yake iwe kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k. Tatizo langu ni kuwa mabadiliko mengi ya awamu hii hayaonekani kuwa na mafanikio makubwa endelevu (Sustainable). In a long run naona kama vile there in more damage done than gain ....... labda kwa sababu ya kila jambo linajaribu kutafutiwa short term solution. Kwa hiyo mambo mengi yanayopata solution leo kesho yakitokea tunarudi back to square one ......... mfano Korosho!!

Anyway, sioni unaonaje mabadiliko ya sasa ni bora wakati watu hawana ajira, wafanyakazi mishahara haipandi, wakulima mazao hayana soko n.k. Huko US data za ajira ni kitu muhimu sana kwa kuwa ni indicator mojawapo kwamba mambo yanakwenda vizuri kwenye nchi ......... hivi ushajiuliza kwa sasa unemployment rate Bongo iko kiasi gani kulinganisha na 2015. Kwa nini serikali hajawahi hata siku moja kutueleza ni jinsi gani ameongeza ajira au kipato cha watu tangu aingie madarakani zaidi ya kila siku kupewa data za Tshs ngapi zinatolewa kwenye elimu bure, Tshs ngapi kwenye mikopo vyuo vikuu as if tumepata uhuru miaka 10 iliyopita.
 
Ukitoa excuse kama hii basi kila utawala utakuja na maelezo mazuuuuri juu ya ufisadi uliofanyika katika tawala zao

Watakwambia EPA, Deep green, Meremeta, Ndege ya Raisi pesa zote zilizotumika huko zilitumika kwa nia njema!.

Nia njema lazima iendane na sheria, kanuni na taratibu ili isiwepo tapanyatapanya ya mali ya umma!
Pesa za umma si sawa na pesa za Jiwe kujiamulia tu azitumie vipi bila due process iliyowekwa kisheria!

JK alimkaanga Waziri wake mkuu kwa sababu Waziri Mkuu alifanya procurement ya mradi wa Richmond bila kufuata sheria ya manunuzi, Hii inatofauti gani na ununuzi wa Bombadia pesa kutolewa bila kuidhinishwa na bunge, bila taratibu za kawaida za procurement kufuatwa?

Unapohamia Dodoma, gharama za kuhamia Dodoma zilitengwa katika bajeti ipi?

Eti kashindwa kumpeleka dada yake nje kutibiwa, wewe vipi?. Hujasikia majuzi katoa milion 50 kumpa Ruge. Wewe unadhani alishindwa?

anyway, nia njema si hoja, Nia njema lazima iendane na sheria na nchi huongozwa kwa sheria si matakwa binafsi ya mtu!
Asante sana msomi wangu na mwana sheria wetu kwa mchango wako wa hoja.

Unajua mkuu ningependa kwanza kukusii kuwa ukisoma jambo usipende kukurupuka kwa kutoa majibu ambayo ni irrelevant. Katika hoja yangu niliyochangia nimeanza na conditonal sentences. Nilitegemea msomi kama wewe kulielewa hilo kuwa conditonal sentences hazileti implication kuwa action imetokea kweli au hapana. It is more like an imagination kuwa some thing might have or might have not happened! Ni kitu ambacho bado hakina Clues ambazo zinaeleweka.

Kwa maana hiyo mimi sijatoa excuse bali nimejaribu tu ku analyse ukweli wa mambo ambayo yanawezekana yakawa yapo au hayapo. Kwani nikiangalia na kulinganisha maisha ya Rais Magufuli na lawama ambazo anazipata kutokana na hela ambazo zina sadikika zimepotea, sioni kama kuna uwiano wowote ule. TZS 1.5 Trillion ni zaidi la pato la serikali kwa mwezi mzima, ni fedha nyingi sana kiasi kwamba imenifanya mimi kuhisi tu kuwa hizo hela, kama kweli zimepotea, zitakuwa zimetumika katika miradi niliyo itaja hapo juu na mingineyo, kitu ambacho mimi binafsi sioni kama ni kitu kibaya, kwani matokeo yake ni sisi wenyewe ndiyo tunao nufaika, na sio kwamba amejitajirisha yeye mwenyewe labda na familia yake. Sija justify kuwa sio kosa kwa majibu wa sheria. Nimeangalia tu umuhimu wa matokeo wa matumizi ya hizo hela.

Nilitegemea katika hoja yako ungekuja na maelezo ambayo ni relevant na issue UFISADI in conjunction na TZS 1.5 Trillion ambazo zina sadikiwa kuwa Rais Magufuli angekuwa amezitumia katika maswala ya matumizi yake binafsi kinyume na sheria, kama unavyodai.

Kabla sijaendelea na kujibu maswali yako mengine mkuu ningeomba fursa ya kupoteza mda wako kwa kuanza na swala la Definition of UFISADI. Kulingana na uelewa wangu Ufisadi ni kitendo cha ubadilifu au ufujaji wa mali ya umma katika matumizi ya mambo yasio leta tija kwa wananchi collectively, kama matumizi mabaya ya kihanatha ya kuishi maisha ya kifahari kana kwamba yeye ni mfalme na jilimbikizia assets kama majumba, magari na kadhalika na kujigamba kuwa yeye ni tajiri wakati hana utajiri huo.

Tumchukulie Mo kama mfano. Mo yeye ni Trillionare kwa Tanzania, ana kampuni yake ambayo inaendeshwa kwa misingi ya kisheria kama registration, kulipa kodi na kadhalika. Aneweza akaishi maisha ya kifahari anavyo weza hakuna mtu atakaye mwuuliza na kumbugudhi kuwa hizo hela amepata wapi na kadhalika.

Lakini unamwona mtu ambaye ni mtumishi wa serikali ambaye huko nyuma alikuwa anamiliki mali na mabilion ya fedha ambazo chanzo chake hakijulikani na hana kampuni ambayo inazalisha products au kufanya biashara, lakini anaishi maisha ya kifahari dhidi ya kipato chake na kuwa considered au regarded kama ni mtu tajiri, hiyo sio sahii. Kitu cha kwanza ambacho binadam mwenye akili timam cha kujiuliza ni ana mda kweli wa kufanya kazi yake aliyo ajiriwa ipasavyo? Watu kama hawa mkuu huko nyuma tulizoe kuwaona kila pembe ya nchi na wengine ni wajomba na shangazi zetu. Hata wazazi wetu nao walihusika basi tu tulikaa kimya.

Mtumishi wa serikali anatoka asubuhi kwenda kazini na saa nane nane hivi za alasiri unamkuta tayari yuko bar na milioni moja akifurahia maisha na wasichana warembo karibu kila siku, unategemea kweli nchi ita kuwa na maendeleo hapo mkuu?

Procurement kwa uelewa wangu sio utaratibu ambao unafuata sheria. Ni utaribu ambao ni wa kiutawala zaidi katika ofisi au mamlaka ambayo inahusika na manunuzi ya vifaa au dhana za kuendesha nchi, kitega uchumi, wizara au mahitaji ya vifaa na material ya projects. Ina fuata zaidi vigezo vya biashara na sio sheria. Sasa kama Rais Kikwete alimkaanga waziri wake mkuu kwa maswala hayo atakuwa na sababu zake, lakini taarifa ambayo ninaijua mimi ni kuwa mhusika mkuu wa scandal hiyo amekana. Sasa nani wa kumwamini?

Kama wewe una amini kuwa Lowassa ndiyo mhusika basi na Rais Kikwete naye alihusika kwani katika maamuzi hayo ya EPA na RICHMOND Rais ndiye mwenye final say, tukifuata utaratibu wa sheria na katiba. Na isitoshe mambo ya EPA na RICHMOND yalihusu energy si ndiyo? Swali langu kwako je, hiyo energy ilipatikana? Mimi nacho jua ni kuwa hela zilipotea na energy hatukupata badala yake tuliambulia magerator na pumps kibao kutoka China na India.

Hivi sasa nashangaa mnadai hela Magufuli kazifanyia Ufisadi lakini magenerator na pumps zimepungua, umeme na maji yako na miradi keme keme ya Flayovers, barabara, ujenzi wa miundo mbinu ya Afya na kadha wa kadha, watu wetu wanapata ajira. What is the moral of the story? A great thinker always remains a great thinker, whether you want to hear it or not.

Mkuu huyo jamaa unaye mwita mtu ningependa utambue kuwa yeye ni Rais wa nchi na anamamlaka ya kuongoza nchi kwa manufaa ya wananchi wake. Kuna maswala mengine yana ulazima wake. Na mamlaka yake yana mpa uwezo huo. Soma katiba yako tukufu utakutana nakipengee kinacho husiana na mamlaka ya Rais. Anaweza akatawala nchi kwa mujibu wa Decree! Jijuze kidogo msomi wangu na mwana sheria wetu.
 
Uchangiaji wa aina hii wa kukariri sijui mikakati, mara sijui dira, mara ooh sijui vitu gani..akili rojo rojo inafikiri umbali size ya pua! eti wizi uundiwe dira...akili za kitoto kitoto kurukia mambo zaidi ya uwezo wake..kazi ipo.
Kama hakuna maana ya kupanga, basi hakuna haja ya bajeti? Hakuna haja ya MPango wa maendeleo? halafu unajiita GT?
 
Ufisadi kwani umekwisha? Hela zinachotwa zinatumika bila budget, una uhakika gani hazipigwi. Sema wewe umeunga mknono yaliyopo, kwa hiyo huoni sasa.
 
Nyinyi ndio wale wajinga ambao mnashikwa akili na watu kiaa tu wanaandika porojo ndefu.Magu ni bonge ya mnafiku tu.

Unajua unachokiandika au unaandika tu?kabla ya lowassa kuhamia CDM,wewe ulikuwa mmoja wa watu wanaompondea humu,baada ya viongozi wako kumpokea ktk chama,wewe kama wewe umeshawi hata kuhoji humu kwanini kapokelewa kwenye chama,achilia mbali kumpondea tena lowassa?
Umeshawahi/unaweza kutupa sababu zako za msingi hapa zilizokufanya wewe kubadilisha mtazamo wako juu yake?
Kwasabu viongozi wako wamempokea nawewe umempokea si ndio maana yake?
Halafu bado unataka kuongea kuhusu kushikiwa akili,au haujui kushikiwa akili kupo vp?
 
Tumeacha kuchekeana na mafisadi?!

Mzee Mwanakijiji, you know better than this...

To every grand corruption, there will always be two sides of players; upande wa kwanza utahusisha, most likely business persons na upande wa pili utahusisha ama top government executives or high profile politician or both!

Tangu hizi drama za kupambana na ufisadi zianze, unakuta ni upande wa wafanya biashara tu ndio kwa mbaaaaaali unaguswa guswa wakati upande mwingine muhimu to keep corruption in equilibrium; hauguswi!

Mbaya zaidi, wale wanaoguswa wala hawawajibiki kwa Watanzania lakini wale wasioguswa, ndio tuliowapigia au kuwahi kuwapigia kura au ndio wanaoishio kwa kodi za wananchi!

Rugemalila kwa mfano, why should I be too concerned with Ruge mtu ambae hana wajibu wa kulinda maslahi yangu badala ya kuwa concerned na watu waliosababisha Ruge kuchota alizochota kwa sababu ni hawa watu ndio nina mkataba nao wa kuhakikisha wanalinda maslahi yangu na ya umma kwa ujumla!

Kwanini niwe concerned na yule mwenye madevu na kilemba wakati hata nikimwambia atamke jina langu kwa ufasaha huenda akashindwa lakini nijifanye kana kwamba huyo mwenye madevu alienda na vifaru pale BoT kiasi kwamba wale waliokuwa na wajibu wa kulinda maslahi yangu na ya taifa kwa ujumla; hawakuwa na jinsi zaidi ya kumwacha achote atakazo!

If am wrong, nitajie ONLY THREE high profile politicians and/or top government executives ambao wameguswa in the so called vita dhidi ya ufisadi! Kinyume chake, ningekushauri achana na hizo porojo kwa sababu bado mnacheka, kula, kunywa, kutembea na kupiga cheers na mafisadi na mengine yote ni porojo tu!

QN: Unadhani Said Lugumi alifanya ufisadi au alisingiziwa?
Umemaliza kila kitu Mkuu, MMK akikupinga hapa atakua amejidharirisha sana
 
Mwanakijiji anadai tunapambana na Ufisadi wakati Jiwe anatwambia tusiwamaindi sana Trafiki kwa sababu ya kututaka tuwape buku tano za kung'arishia viatu!.

Huyu mzee Mwanakijiji it seems yuko out of touch na kinachoendelea nchini!

Huku kuna ufisadi wa kutisha!
1. Kuna ufisadi wa kutoheshimu katiba
2.Kuna ufisadi wa ukanda na udini
3. Kuna ufisadi wa pesa za umma kutokutumiwa kwa kufuata sheria
4. Kuna ufisadi wa ulevi wa madaraka
5. Kuna ufisadi wa uonevu dhidi ya wapinzani
6. Trilion 1.5 mpaka leo hii haijulikani zilipo!
 
Back
Top Bottom