Tulifurika uwanjani kujua utata kuhusu RICHMOND, si kwamba tunampenda Lowassa

Bora hata wewe unajua kuhusu utajiri wake ulitokana na nini. Wengi wansomtetea humu ndani wakiulizwa amepata wapi utajiri wake wanaishia kutukana na kusema ni wivu. Wewe kwa kweli unaonyesha una busara, hebu tuambie kaupata wapi?

Hahaha salute kwako dah
 
Sasa mbona mlikuwa mnamshangilia tena kwa kishindo kikuu. Kama kweli mlitaka kujua ataongea nini na wala hamko nae mngebaki nyumbani mkacheki kwa luninga au kusikiliza redio.
 
Mungu wetu ni wa ajabu sana, alimzuia asidanganye Watanzania ndiyo maana alikuwa haeleweki hata alichokuwa akikizungumza.


Like a Robot....

Upo makini sana! Kasumbua wenzie wakati hana jipya.
 
Ni mbinu tu ya wanasiasa kuvuta watu ili adhaniwe kukubalika. Si kila aliyehudhuria mkutano ni mfuasi wa EL! Kila mtu huenda kwenye mkutano kwa madhumuni yake maalum!
Nashangaa pia swala la Richmond bado analipiga danadana! Wahusika ni akina nani basi?
 
KWANI HATA ANGELIZUNGUMZIA RICHMOND

ANGELIWEZAJE KUJISAFISHA

HILI NI KAMA HESABU LA ALJEBRA

AU NI FUMBO X =Y AND Y=X

FIKIRISHENI VICHWA VENU

***UKUBWA HEKMA NA TAFAKURI***

YAANI MPAKA MBWAGIWE MEZANI/ jr
 
jamani pamoja na kupingaaaaa wagombea urais...sasa ni vema tukapendekeza anayefaa kwani iwe isiwe lazima rais apatikane
 
Swala LA msingi alilotakiwa kwanza ni kijisafisha watanzania tunataka kujua kwanini anahusishwa na Richmond. Jana ametushangaza saana anakuja kutusomea vitu vya kuandikiwa tu. .watanzania tunamsubiri asidanganyike na hao aliowanunua
 
Mungu wetu ni wa ajabu sana, alimzuia asidanganye Watanzania ndiyo maana alikuwa haeleweki hata alichokuwa akikizungumza.


Like a Robot....

Yani sina kumbukumbu yule jamaa aliongea nini hahahah
 
mm mwenyewe nimekasirika sana nimepoteza muda kusubiri majibu ya richmond halafu analeta usanii tu
 
TUTAANZISHA SIKU YA WAMBEYA DUNIANI!! Wape taarifa mashosti wenzio! Nendeni mkale MTAMA uko!!

Mkuu umajua tafsiri ya umbea kimtaa??
Maranyingi huwa ni ukweli unaosemwa kabla ya muda wake kufika. Kwahiyo hiyo siku inaweza kua na mantiki kidunia. Mi nipo kuungana na wewe katika hili hiyo siku ianzishwe.
 
Wakuu kwanza salaam!! Nawasalimu nyotee....
Jana Jumamosi bwana Lowassa alitangaza nia, tena si nia tuu bali kampeni ya kugombania urais katika nchi hii. Sina tatizo nae, ni haki yake kikatiba.

Tatizo ni kwamba kile alichokiahidi kukizungumzia kuhusu kashfa yake ya RICHMOND. Watu tulifurika uwanjani tukisubiri habari hiyo mpya, lakini hatukuona jipya hata kidogo. Kauli zote alizoziongea jana si mpya kwetu kwani ahadi za CCM tumezizoea.

Hoja ya msingi inabidi atueleze habari ya RICHMOND kwani ndio habari ya mjini na ndio tunaisubiri,
hatutaki bla bla hapa, atueleze kwa kina alihusika vipi na kashfa hiyo na kama hakuusika alihusika nani!!!

Asanteni

Sasa mabango ya kuonyesha mnapenda mlibeba ya nini? Hebu acheni siasa zenu chafu. Kila uchao mnatumwa na kina Membe kuanzisha threads za kumkashifu Lowassa badala ya kujenga hoja za msingi! Na kusema mtaifanyia nchi....
 
Kumbe maamuzi magumu ni pamoja na kunyamazia uozo? maccm yanasifiana kwa kuficha uovu, Sasa huu mzigo ataubeba badala ya maccm wenzake, ngoja apitishwe moto tutakaompelekea ataufyata, kizota mpitisheni mleteni tunamsuhiria kwa haku.
 
Bado lowassa ni mtuhumiea wa Richmond naishangaa kwa nini Takukuru haijamtia Pingu huyu mgawaji rushwa na jana kagawa tena.
 
Hamjaelewa anachokwepa Lowasa, anachokwepa kukiongea ni kwa sababu bado hajapitishwa kuwa mgombea uraisi kwa kuwa wanaompitisha miongoni mwao kuna mafisadi wa kutupwa na wengine wanahusika na kashfa hizo, sasa akiwalipua mapema kuna KUPITISHWA HAPO? Pengine hiyo ndiyo hofu yake.
 
Mimi binafsi nilienda uwanjani nikitegemea kumwona Lowasa akibadilisha hali ya hewa kwa kuliweka sawa sakata la Richmond ila kwakuwa aliamua kulipigia kimya ni wazi Dr. Mwakembe alikuwa sahihi na mkweli.

Pia nawashukuru wakazi wa Arusha kwani walijitokeza kwa wingi ila walipoona Blabla zimekua nyingi walianza kujiondokea na kuwaacha wale wa mikoani waliosombwa kwa mabasi na malori.

Hakika niliwasikitikia sana jamimi ya wafugaji (wamasai) waliosombwa kwa malori huku wakiwa hawana ufahamu na kazi yao ni kushabikia tu.

Kiukweli jana niligundua ni kwanini Lowasa anaiongoza Munduli kwa kipindi kirefu na jibu ni aina ya watu anaowaongoza.

Nilishia kuona wamasai wakisema yero huyo ni rais amewapa watu elimu dunia nsima!!!!
 
Back
Top Bottom