Tulifikia kuhitaji aina ya Rais tulienae

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
1,159
805
Habari wanajamvi,

Baada ya pilau langu la idd leo nimewaza jambo fulani, kwamba haya anayofanya rais wetu ni wakati muafaka, kuna watu tuliishi jehanam na wengine peponinhali ya kuwa sote ni raia wa nchi hii.

Namshauri Rais akaze buti maana hata usawa umeoneka kwenye hii sikukuu, wote tumeambulia pilau kama watoto wa uswahilini.Hiyo Demokrasia tunayotaka aifuate ndio imetufikisha pale tulipokuwa, kulikuwa na harufu ya ufisadi kila idara na huduma ziliendelea kuzorota siku hadi siku.

Ushauri wangu kwa rais;

1.Endelea na kasi hiihii, sisi walala hoi tuko pamoja na wewe.

2.Hawa UKAWA waachie platform yao wakushauri na hata kukuchallenge maana ndio kazi ya opposition.

3.Bunge liache lifanye kazi zake maana ndio chombo kitakachokusaidia kuisafisha system ambayo unaijenga.

4.Wabane wateule wako ili hii 40% ya fedha za maendeleo kwenye bajeti ikalete tija kwa wananchi huko vijijini.

5.Bado Naamini tuna rasilimali za kutosha kutuvusha hapa,tumia safu yako imara ya wachumi tulionao kuona namna hizi fursa zitakavyoinua maisha ya hawa walala hoi.

Asante
 
Anafanya kazi nzuri sana ktk kubana matumizi na kuziba mianya ya kukwepa kodi, wizi na rushwa. Ila akitaka awe kiongozi bora zaidi afuate katiba (uhuru wa habari, demokrasia n.k). Sawa katiba iliyopo ni imepitwa kwa wkt lkn sio kuikandamiza
 
Ila Chadema na Ukawa nao Wehu tu watu tumewabeba wakatuaminisha tuwe na Aman hakuna KURA itakayoibiwa, badae hata mrejesho haukurudi tuliona Mazingaombwe tu. SAIZ im fighting My own life, anaejali kizazi cha KESHO ndie namuunga Mkono. NAHTAJI KUIONA TANZANIA BORA kwaajili ya kizazi Changu kijacho
 
Hahahahaa unachekesha wewe, sio wote wenye hali nzuri ni mafisadi, wengine ni juhudi na ubunifu na usimamizi makini wa kazi zao ndio uliowaletea maisha ya peponi.
Haya bhana endelea kufurahia viporo vya Eid
 
Ha Ha Ha!!ni Kweli Lakini Hizo Juhudi Na Ubunifu Ulibebwa Na Ujanja Ujanja Mwingi Na loophole Ya Mfumo Tuliokuwa Nao, Kwa Hiyo Na Wao Ni Mafisadi Tu!!!ndg Kama Umevuliwa Nguo Chutama Tu, Acha Tujenge Nchi Mliyoifanya Shamba La Bibi
 
Alivyo hana soni anaweza kukuteua DED au DAS.. Sasa unaposema kuwa "wote tuliambulia pilau kama watoto wa uswahilini" unafurahia wenzako kupata shida au??? Muone sura kama mfalme wako mtukufu asiye na dhambi! Mnafanana sana mpaka akili!!
 
UKAWA watakunyonga wewe. Hawataki Rais mkali
Najua unazo akili tu lakini unajifyatua, natamani hata siku moja ujadili uzi nje ya siasa maana kwako majibu yote ni ya kikada zaidi
 
afuate katiba yetu aliyoapa kuilinda japo ina mapungufu yake. nje ya hapo vyote afanyavyo havitathaminika mbele ya umma.
 
Hahahahaa unachekesha wewe, sio wote wenye hali nzuri ni mafisadi, wengine ni juhudi na ubunifu na usimamizi makini wa kazi zao ndio uliowaletea maisha ya peponi.
Haya bhana endelea kufurahia viporo vya Eid
Ni kweli mkuu ulichosema. Kuna matajiri wengi tu ambao hawajaiba kitu cha mtu wala kuiba serikalini, ni juhudi zao wenyewe. Lakini sasa hivi tunakoelekea ni kwamba kuwa tajiri ni dhambi, kuwa na maisha mazuri ni ufisadi. Bado tuna safari ndefu..
 
Nkongu Ndasu Nchi Hii Tatizo Siyo Katiba Ingawa Ni Muhimu Kuiboresha, Nyerere JK Tunamlilia Kila Siku Alitumia Katiba Mbovu Kuliko Hii, Cha Msingi Ni Utashi Wa Kuamua Jambo Jema Kwa Raia Wako, JPM Ameamua Ndio Maana Nashauri Tumuunge Mkono, , Afterall Mambo Yatafanyika Kwa Awamu Kama Yalivyoharibiwa Kwa Awamu
 
Ni kweli mkuu ulichosema. Kuna matajiri wengi tu ambao hawajaiba kitu cha mtu wala kuiba serikalini, ni juhudi zao wenyewe. Lakini sasa hivi tunakoelekea ni kwamba kuwa tajiri ni dhambi, kuwa na maisha mazuri ni ufisadi. Bado tuna safari ndefu..
Ni kweli usemayo, basi kwa mtaji huo ni dhambi kutaka nchi ya viwanda labda serikali ijenge na sio watu au kampuni binafsi
 
Alivyo hana soni anaweza kukuteua DED au DAS.. Sasa unaposema kuwa "wote tuliambulia pilau kama watoto wa uswahilini" unafurahia wenzako kupata shida au??? Muone sura kama mfalme wako mtukufu asiye na dhambi! Mnafanana sana mpaka akili!!
Yaan Jpm wapo wengi mno hizo hasira dhidi ya waporaji ndo kwanza amelianzisha.

Watanyooka tu.

si kila mabadiliko watu wamwage damu Hata Democrasia inaweza amua.

Bandika bandua wakimbandua anabandikwa mwingine. Hadi heshima iwepo maana Kejeri zilizidi mno. Khaa!
 
Back
Top Bottom