Tulifanya utaifishaji, tukajuta. Tukaua Mashirika na makampuni, tukajuta. Sasa tunaua Demokrasia, hatutajuta?

road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
2,064
3,011
JK Nyerere kwa kinywa chake aliwahi kesema (baada ya kustaafu) kwamba alijutia kutaifisha baadhi ya mambo ikiwamo mashamba ya mkonge Sisal estates!!! Kiukweli ukifika kwenye hayo mashamba mfano Tanga, Mwanga, Same nk utaona kweli kuna kitu au uwekezaji ulifanyika hapo.

Ikaja awamu yingine makampuni na mashirika ya umma yakafa kifo cha mende. Inawezekana ilitokana na kubadilika kwa mifumo ya dunia Lakin tungekuwa na mtazamo sahihi tungeweza kuyanusuru baadhi ya haya makampuni kwa gharama au mfumo wowote ili yaendelee kuwa active tusingekuwa hapa tulipo!!

Nakumbuka baadhi ya hayo makampuni kama
Dowico (wine)
Tegry plastic
Textiles mutex,kilitex,sungura tex urafiki nk
Moro ceramic
Moro shoes
Canvas
Viwanda vya ngoz (tanneries) nk

Ilitupasa tuyanushuru hata kwa gahama yoyote Hali isingekuwa ilivyo sasa. Lakini hatukuijua kesho yetu. Sasa hali ni zaidi ya mbaya!!! Zikitoka nafasi 40 za kazi wanaomba watu 30,000 tena wana sifa.

Hilo hatukulijua sasa tunajuta!
Sasa imekuja awamu ya kuua mawazo huru na kuua demokrasia. Je, Hatutajuta? Kwanini watawala wanatumia nguvu kuuuubwa kuaminisha watu kuwa upinzani ni sumu kwa nchi Wakati Katiba inaruhudu upinzani.

Mfano ambao unaua uhuru wa mawazo, Mwenyekiti wa chama ambae ndie Rais wa nchi anaingilia maamuzi ya wanachama kwa kuondoa/kukata jina la mwanachama fulani na kuweka jina lingine ,hivi huyu aliyepewa lift au favour na Rais anaweza kujenga hoja bungeni dhidi ya Serikali ili hali akijua next round Rais ana mamlaka ya kuondoa jina!? Hivi hii sio hatari!? Hatutajuta baadae!?

Tulizoea kuona mijadala bungeni tukaona na bajeti mbadala tena zilikuwa zina facts nzuri tuuu kuliko hata za chama kikuuu!!! Sasa hazipo!!! Ndio maaana waliopewa dhamana wanamua kujikita kwenye Tozo Kwani wanakosa mawazo upande wa pili!!! Hatutajuta!??
 
Na ukikaa na kufikiri, unaona ni ufinyu wa akili na maarifa tu wa wanasiasa wa Tz.

Uchumi wa dunia unasababisha aje uuze au uue vyanzo vya mapato ya kila siku ya wananchi wako?

Hatuna jambo ambalo tumelisimamia kwa ufanisi kama WaTz tunaojitawala, ni uharibifu na ukosefu wa msimamo tu.
 
Na ukikaa na kufikiri, unaona ni ufinyu wa akili na maarifa tu wa wanasiasa wa Tz.

Uchumi wa dunia unasababisha aje uuze au uue vyanzo vya mapato ya kila siku ya wananchi wako?

Hatuna jambo ambalo tumelisimamia kwa ufanisi kama WaTz tunaojitawala, ni uharibifu na ukosefu wa msimamo tu.
Masharti ya IMF huyajui!?
 
Back
Top Bottom