MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,757
- 48,403
Naona MaCCM humu yamechachamaa kufungua nyuzi ili kutafuta mbinu za kupaka tope uchaguzi uliofanyika Kenya, yanajaribu kutumia hizo mbinu kuficha aibu ya dhuluma zao kwao huko Tanzania.
Ifahamike kawaida baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu kura, huwa hatukimbilii kumtangaza mshindi na kumuapisha kama kwenu huko, huwa lazima kura zihakikiwe kwa mbinu zinazokubalika na wagombea wote, tena mbele ya waangalizi wa kimataifa na vyombo vya habari, ili kuhakikisha anayeshindwa hata akienda mahakamani hatakua na sababu zozote au hoja zozote zenye mashiko.
Kingine, katiba inahitaji mshindi lazima awe aliyekubalika na Wakenya, maana kwamba lazima ashinde kwa asilimia 50%+1 na mpaka sasa hakuna aliyekidhi hicho kigezo, hivyo kuna uwezekano tukarudia zoezi la ushindani baina ya wagombea namba moja na mbili, wengine watoswe.
Hii yote ni kwa ajili ya kuhakikisha tunampata kiongozi anayekubaliwa na wananchi, sio kulazimishiwa mtu. Kwa hivyo tulizeni nyuzi zenu hizo kila mara ooh "Kenya kimenuka", "Kenya kitawaka", "Kenya kitaiva", "Kenya watakatana mapanga".....mumekaa kama mafisi yenye njaa mnasubiri mkono udondoke hamuna hata aibu....ha ha ha!!!