Tulieni, Lissu sio Roma akirudi atazungumza kila kitu

Yaan aje huku ndio aongee??aongelee huko huko ,,huku atazuiwa kuongea
 
Tukimjua tutamgawana kama mkate uliopakwa asali, na kama ana madarakani makubwa tutamuombea kwa Mungu ampe adhabu Kali na kumletea aibu kubwa yeye na familia yake
Miujiza iliyotokea kupona kwake ni Mungu tu ni kama nusu kufa (half dead) so he has nothing to lose hata kama akimtaja yeyote.
 
Ni kweli inabidi "WatuWasiojulikana" watulie sana tena sana..
Badala ya kulaani tukio wao wanajitetea kwa kauli tata..!!
Kadri wanavyojitetea ndivyo tunavyoendelea kuwafahamu..!!
 
Mungu alivyomkubwa akawaponya TL na Dereva wake. Aibu sana kwa wauwaji. Ashukururiwe Mungu kuwa na wauwaji wajinga kiasi hiki. Very inefficient killers
 
Atakuwa anatuongopea, siku zote hizo ICU atakuwa anajua nini, huyo hivi sasa ni kama msukule tu
 
Atakuwa anatuongopea, siku zote hizo ICU atakuwa anajua nini, huyo hivi sasa ni kama msukule tu
Najua akija kuongea utaifuta hii post.

Ukija kuifuta quote yangu bado itakuwa shahidi.

Mark your word and my word!!
 
Na dereva angebaki wasingekosa la kusema. Kwanza wangeanza kuchambua dini yake; wangechambua kabila lake; wangechambua kanda yake; wangechambua nafasi yake kisiasa; wangechambua umasikini wake; wangechambua rangi yake; wangechambua ufupi wake; wangechambua jinsia yake; wangechambua kila aina ya upuuzi wanaoujua wao halafu wangekuja na conclusion - CHADEMA ni WABAGUZI.

Ona! Wamempeleka Lissu hospitali ya kifahari huku wakimtelekeza dereva wake kama mbwa; dereva aliyefanya kila jitihada kuokoa maisha yake. Wangeendelea kujibizana kipumbavu, "isingekuwa weledi wa dereva, Lissu angekufa; walaaniwe". Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana!
Km Wamendoa CCTV Dereva Wa nini
 
R
Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kumlinda Mh. Tundu Lissu huko aliko kwenye hospitali ya Aga Khan Nairobi, tumuombee ampone haraka arudi tuungane tena kwenye harakati za kutetea raslimali zetu.

Pili niwaombe wote kwa ujumla 'mnaojihisi' mmehusika mtulie hofu ya nini, kama maji yameshamwagika kuyazoa ni kazi sana mwisho mtazoa na tope. Hakuna haja ya ku panic, niwahakikishie tu kuwa Mh. Lissu ambaye ndiye mhanga wa tukio hili kwa jinsi alivyo, atakaporudi atasema kila kitu hatoacha jiwe juu ya jiwe.

Najua wengi wenu mlitegemea Lissu hatopona ili mtumie tukio hili kwa faida yenu kisiasa kuichafua CHADEMA na viongozi wake, Mungu hakutaka iwe hivyo bado ana mpango naye. Baada ya kuona uwezekano huo ni mdogo mkahamishia majeshi kwa dereva kuzusha kuwa kakimbia, mkaambiwa dereva hajakimbia anatibiwa Nairobi, halafu tena ni binamu mtoto wa dada yake.

Mlipoona hilo limeshindikana, mkahamia kwenye rangi ya shati, mkaulizwa, hivi mkiambiwa rangi ya shati ndiyo itafawafanya mjue Lissu amepigwa risasi? Hata hivyo nani kawaambia vitambaa alivyoshikilia dereva ni shati, badala ya kuhoji ilikuwaje gari isiyokuwa na plate number iliruhusiwe kupita geti la viongozi Area D, nyie mnahoji rangi ya shati, tuwasamehe.

Baada ya rangi ya shati kupuuzwa, mmehamia kwenye issue ya kwa nini nguo za Lissu ashikilie dereva na si mke wake, vihoja vya kitoto kabisa, zingeweza kushikiliwa hata na nesi, je mngesema nesi ni mke wa Lissu?, vingeweza hata kuwekwa kabatini au kwenye mfuko. Mnahoji bila kujiuliza mke wa Lissu alifika hospitalini muda gani baada ya tukio na je alikuwa Dodoma kwa siku hiyo?

Mbona suala hili lipo wazi sana, Lissu na dereva wake sio wajinga bado wapo hai speculations hazisaidii, walijua muda mrefu (more than a month) kuwa wanafuatiliwa kwahiyo walikuwa wamejiandaa kwa kiasi chake.

Lakini ninachotaka kuwaambia ni kuwa, kila kitu kitawekwa wazi, msiwe na hofu labda kama mnahusika.

Sina bullet proof.
Roma huzungumza kwa mashairi!
 
Back
Top Bottom