Tulidai Matokeo yalipochelewa kwa Kutanda Je na Taarifa nayo Tufanye Hivyo????


NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
1,675
Likes
6
Points
0
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
1,675 6 0
[FONT=&quot]Kama kuna kitu wana-CHADEMA ikiwa ni pamoja na wananchi wengine (labda na serikali ya JK) wamekingoja kwa hamu zote ni taarifa ya nini kimetokea wakati wa uchaguzi hata kumtangaza Kikwete kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania[/FONT]

[FONT=&quot]Hata kabla ya kutangazwa rasmi kuwa Raisi na tume ya uchaguzi, tayari katibu Mkuu wa CHADEMA (naomba nisiseme aliekuwa mgombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA) aliuambia umma kuwa kuna mapungufu makubwa ya matokeo ya uraisi yanayotangazwa na tume na hivyo kuitaka tume kusitisha matokeo mara moja.[/FONT]

[FONT=&quot]Hata hivyo tume kwa sababu wanazojua wenyewe hawakumsikiliza na waliendelea kuyatangaza mpaka walipomtangaza raisi bwana Kikwete huku Katibu Mkuu wa CHADEMA akisema wazi kuwa hayatambui matokeo hayo (yeye na chama chake) kwa kuwa yamejawa na mushkeli mwingi na raisi ametangazwa kwa matokeo yasiyo halali. Hakuishia tu hapo, lakini alitoa ahadi ambayo mpaka sasa inatutesa wengi ya kuwaambia watanzania ni kwa nini hawayatambui matokeo hayo na watatoa taarifa ni kwa nini hawayatambui.[/FONT]

[FONT=&quot]Ni muda sasa umepita hakuna taarifa yoyote huku itulazimisha wanachama na watanzania kuamini ya kuwa kuna mapungufu lakini hawayaweki wazi na uthibitisho wa mapungufu hayo. Labda wengine tunayajua lakini wengine hawayajui na wanaendelea kutuona wanaCHADEMA kama majuha tunaobisha huku hatujui tunachobishia. Hapa ndipo ninapopata taabu. Kibaya zaidi ni kuwa pako kimya na wala hakuna dalili wala fununu ya nini kinaendelea na ni lini tutapata taarifa. [/FONT]


[FONT=&quot]Nililazimika kuongea na rafiki yangu mmoja ambae kwa sehemu Fulani yuko karibu na makao makuu na nikamuuliza kwa nini hakuna taarifa yoyte mpaka sasa na tuliahidiwa itatoka karibu? Nilitaka kujua kama bado taarifa inatengezwa au imekwisha ila wakuu wanatafuta “pose” la kutokea. Kimsingi taarifa ambayo nimeipata (sitaki sana iwe ya uhakika 100%) inaonesha wazi ya kuwa taarifa hii iko tayari. Uthibitisho wake wa kwanza ni ahadi yao ya kutoa taarifa ndani ya muda mfupi. Kw aninavyowafahamu viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na katibu Mkuu wakisema hivi, hii inamaana ya kuwa kweli taaarifa iko karibu. Hata hivyo ukimya huu unatutia mashaka.[/FONT]

[FONT=&quot]Kutokana na haya nililazimika kuhoji je ni kwa nini taarifa haitoki?? Kati ya majibu niliyopewa ni kuwa taaarifa “imeiva” ila tatizo ni maombi ya viongozi wa dini waliomtembelea Katibu Mkuu na viongozi wengine na kuwaambia wakatishe kutoa taarifa hiyo ili kulinda amani ya Tanzania. Mimi sijui ni amani gain hii inayozungumzwa hapa. Naungana mkono na mtazamo wa Mtikila kwa ugeni huu wa viongozi hawa wa dini kwa Dr. Slaa na Chadema ya kuwa ni wa kinafiki. [/FONT]

[FONT=&quot]Kwa viongozi wa CHADEMA naomba tu niwafahamishe ya kuwa “you are driving us crazy” for not giving out the report. We want it out please before our patient run out of charge.[/FONT]

[FONT=&quot]Niwakumbushe tu ya kuwa wakati tume inachelewesha matokeo ya viongozi wetu tuliowachagua kwa imani kubwa tena bila sababu yoyote ya msingi, tulilazimika kulala kwenye majengo ya kuhesabia na kutangaza kura mpaka tukapata haki yetu. MATOKEO YALE NI HAKI YETU MAANA YALIBEBA HATIMA YETU, YALIBEBA IMANI YETU NA FURAHA YETU. Kucheleweshwa kwake ilikuwa ni maumivu makali kwetu. Mtambue ya kuwa kwa kuchelewesha huku tena bila taarifa inayoeleweka mnaanza kunitia wasiwasi wa kuwaona na nyie kuwa sawa na Mkurugenzi wa Shinyanga mjini kuchelewesha haki ya wananchi bila sababu ya msingi.[/FONT]

[FONT=&quot]JITOKEZENI, YOENI KAULI, TUAMBIENI LINI.[/FONT]

[FONT=&quot]KAMA TULIVYODAI MATOKEO YETU, TUKICHOKA TWAWEZA DAI NA TAARIFA YETU.[/FONT]

[FONT=&quot]HAKUNA MWENYE HAJA YA KUMWAGA DAMU, Tunachotaka ni taarifa, tujue ni kwa namna gain watawala wanachezea haki yetu, wanachezea hatma yetu, wanachezea uhuru wetu pamoja na maamuzi yetu kama wapiga kura. Nilichomwa na jua na kupata taabu nyingi wakati wa kupiga kura, TAARIFA TU PEKE YAKE ITATOSHA KUTULIZA MZUKA[/FONT]
 

Forum statistics

Threads 1,235,139
Members 474,353
Posts 29,213,133