Tulichojifunza kutoka kwa watu wa Vietnam

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg
View attachment 328602

Wale wa umri wangu ukiitaja Vietnam basi unakuwa unaelezea zile "movie" za mapigano kati ya majeshi ya Vietnam na nchi adui.Enzi zetu tulikuwa tunaoana "movie" kiasi cha kuamini Wavietinam wana jeshi lenye askari wasioisha,maana ilikuwa kila wakipigwa risasi na kufa wanaibuka wengine.Hii ndio ilikuwa taswira ya utoto juu ya Vietnam.

Hatimaye tulikuwa na kuijuwa Vietnam,ziara ya Rais wa Vietnam ilianza na mjadala wa "Tanzania-Vietnam Business Forum" ambao waongozaji walikuwa Waziri mkuu na Rais wa Vietnam.Safari ya Rais huu inaanza Tanzania baade Msumbiji na kumalizia nchini Iran,ni ziara itakayomuweka Rais wa nchi hiyo ugeninj kuanzia 09/03-15/03/2016.Rais huyo ameambatana na mawaziri nane na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 50.Mjadala wa leo uliwahusisha Tanzania Investment Centre,Tanzania Private Sector Foundation na Vietnam Chamber of Commerce.

Kwetu sisi Watanzania tuna mengi sana ya kujifunza kutoka Vietnam,mpaka mwaka 1970's Tanzania na Vietnam ilikuwa ni nchi sawa kwa kiwango cha maendeleo,zikijulikana kama nchi za kipato cha chini.Mwaka 1974 nchi ya Vietnam ilituma vijana kadhaa kuja kujifunza mbinu za "seddling" ,walitembelea kwenye vyuo vya Kilimo vya Naliendele n.k,huko walijifunza jinsi ya kuandaa miche na jinsi ya kuanza kilimo cha korosho,mwaka mmoja baadae yaani 1975 walikuja kujifunza ktk viwanda vyetu jinsi ya kupangua korosho.Elimu hii ilitolewa na wataalamu wa kitanzania kwa vijana wa Vietnam ambao walirudi kwao na kusambaza elimu hiyo kwa nchi yao.Leo mwaka 2016 Vietnam ndio nchi ya pili duniani kwa "export" ya korosho katika soko la dunia,jeuri hii wameipata kwa kuchukua ujuzi wa kupanda na kubangua korosho toka Tanzania,wakati huku kwetu Bodi ya Korosho ndio moja ya bodi zinazolalamikiwa kwa ufisadi mkubwa na huku mkulima wa korosha akilalamika na kero ya stakabadhi ghalani.

Licha ya kuwa Vietnam inaingia mara tatu kwa ukubwa ktk nchi ya Tanzania, lakini inazalisha mchele mara tatu kwa mwaka,wakati sisi tukiwa na mabonde makubwa kama Kilombero,Mbarali,Rufiji na Bonde la Ruaha tunazalisha mchele mara moja kwa mwaka.Eneo la kilimo cha Mpunga Vietnam inalingana na bonde la Mkomazi lililopo mpakani mwa Korogwe na Tanga,na mchele huo huko Vietnam unauzwa dunia nzima.Pia Vietnam inazalisha pilipili manga kwa wingi na ndio inaongoza kuuza ktk soko la dunia.

Zaidi ya Kilimo,Vietnm imejiingiza katika biashara ya mawasiliano,kwa kutumia kampuni yake ya Viattel Group inayomilikiwa na Wizara ya Ulinzi na kuwekwa chini ya Jeshi la Vietnam,Vietnam wamefungua kampuni dada ya Halotel katika nchi za Tanzania na Msumbiji,Halotel Tanzania wamewekeza dola milioni 700 na kutawanyika zaidi maeneo ya vijijini.Kampuni hii ipo chini ya jeshi na inasimamiwa na jeshi la watu wa Vietnam.Wamejiimalisha ktk technolojia ya mafuta na gas na hii ndio inampeleka Rais wa Vietnam nchini Iran.

Hawa ndio Vietnam,ambao miaka ya 1970 walikuja Tanzania na kujifunza mbinu za kilimo cha Korosho,hawa ndio miaka ya '70 tulikuwa nao sawa ktk kiwango cha maendeleo na ukuwaji wa uchumi,lkn leo Vietnam imekuwa ya kutupa msaada sisi kama Taifa.Tujiangalie kama Taifa,tuweke mkakati wa pamoja na tutazame wapi tulipokosea na kunyanyuka.
 
Kwa nchi ambayo itikadi za vyama zinawekwa mbele na utaifa unawekwa nyuma au sometimes unakuta hamna kabisa tutabaki hivi hivi na hata somalia wakimaliza vita vyao watatupita na watakuja kwetu kufanya investments na tutasema mwaka x walikua kama sisi
 
Basi hapo jinsi tulivyokuwa hatupendi kusumbua akili zetu jibu letu rahisi tu,ni kusema kuwa ccm ndiyo iliyotufikisha hapa basi. Hivyo tukichagua upinzani ndio mambo yote yatakuwa sawa,japo hao viongozi waliyokuwepo upinzani wametoka hukohuko ccm.

Hizi siasa za vyama sijui zitaisha lini ili tujenge nchi yetu.
 
View attachment 328604 View attachment 328602

Walijua ubaya wa majipu wakaanza kuyatumbua toka zamani, kwetu sisi majipu yakiisha tutaamka tu. Mungu ibariki Tanzania
 
Mtoa post unania ya kuidhalilisha ccm na viongozi wake wakina napi,february,muongo,mafish,change,hela ya mboga,..tanzania kuifika vietnam haitawezekana
 
Basi hapo jinsi tulivyokuwa hatupendi kusumbua akili zetu jibu letu rahisi tu,ni kusema kuwa ccm ndiyo iliyotufikisha hapa basi. Hivyo tukichagua upinzani ndio mambo yote yatakuwa sawa,japo hao viongozi waliyokuwepo upinzani wametoka hukohuko ccm.

Hizi siasa za vyama sijui zitaisha lini ili tujenge nchi yetu.
Huo ndo ukweli japo mchungu!
 
barafu

Ziara hii ilianzia pale Kikwete alipotembelea Vietnam na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi. Immediately tukaona vielelezo wanaanzisha biashara yao Tanzania, remember halotel?

Hii ni moja ya tija ya safari za Kikwete.

Kudos Kikwete.
 
Kwa nchi ambayo itikadi za vyama zinawekwa mbele na utaifa unawekwa nyuma au sometimes unakuta hamna kabisa tutabaki hivi hivi na hata somalia wakimaliza vita vyao watatupita na watakuja kwetu kufanya investments na tutasema mwaka x walikua kama sisi
Kweli kabisa Mkuu! Rwanda si hawa wanatupita?
 
Basi hapo jinsi tulivyokuwa hatupendi kusumbua akili zetu jibu letu rahisi tu,ni kusema kuwa ccm ndiyo iliyotufikisha hapa basi. Hivyo tukichagua upinzani ndio mambo yote yatakuwa sawa,japo hao viongozi waliyokuwepo upinzani wametoka hukohuko ccm.

Hizi siasa za vyama sijui zitaisha lini ili tujenge nchi yetu.
Kumbuka tulianza na vyama vingi, nyerere nadhan aliwaza kama wewe akaviunganisha tukawa na kimoja! Nadhan tukatoka kapa then wakavirudisha!
 
Mkuu ahsante kwa habari njema. Angalau tumeanza vyema,haka kamagu chetu katatupeleka somewhere man. Ila mswahili inabidi tumpige ban kwenda ikulu maaana khaa!
 
Back
Top Bottom