Tulichambue Baraza la mawaziri la JK... Hili hapa toa maoni....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525

...TUNAPOELEKE UKINGONI MWA KIKAO CHA BUNGE LA BAJETI,NA KAMA UMEKUWA MFATILIAJI MZURI WA VIKAO VYA BUNGE HILI..NAOMBA MAONI YAKO KUHUSU MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI HAWA..................NANI KILAZA NA NANI MTENDAJI MZURI...


Orodha ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wa Wizara za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010 - 2015

1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora - Mathias Chikawe

2. Waziri wa Nchi, Mahusiano na Uratibu - Steven Wassira

3. Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia

4. Ofisi ya Makamu wa Rais Waziri anayeshughulikia Muungano - Samia Suluhu Hassan

5. Waziri wa Nchi Mazingira - Dk. Therezia Luoga-Kovisa

6. Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi wa Sera Uratibu na Bunge - William Lukuvi

7. Waziri wa Nchi, Uwekezaji na Uwezeshaji - Maria Nagu

8. Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - George Mkuchika

9. Naibu Waziri Tawala za Mikoa - Aggrey Mwanri

10. Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Masuala ya Elimu - Kassim Majaliwa

11. Waziri Wizara ya Fedha - Mustapha Mkullo

12. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (i) - Gregory Theu

13. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (ii) - Pereira Silima

14. Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Shamsi Vuai Nahodha

15. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch- Balozi Khamis Sued Kagasheki

16. Waziri wa Katiba na Sheria - Selina Kombani

17. Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Bernard Membe

18. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Mahadhi Juma Mahadhi

19. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi

20. Waziri Wizara yaMaendeleo ya Mifungo - Dk. Mathayo David Mathayo

21. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo - Benedict Ole Nangoro

22. Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Profesa Makame Mnyaa M'barawa

23. Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Charles Kitwanga (almaaruf Mawe Matatu)

24. Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Profesa Anna Kajumulo-Tibaijuka

25. Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Goodluck Ole Medeye

26. Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige

27. Waziri Wizara ya Nishati na Madini - William Mghanga Ngeleja

28. Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini - Adam Kighoma Ali Malima

29. Waziri Wizara ya wa Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) - John Pombe Magufuli

30. Naibu Waziri Waziri Wizara ya wa Ujenzi - Dk. Harrison Mwakyembe

31. Waziri Wizara ya Uchukuzi - (Reli, Bandari, Usafiri wa Majini) - Omary Nundu

32. Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi - Athuman Mfutakamba

33. Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara -Dk. Cyril Chami

34. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara - Lazaro Nyalandu

35. Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dk. Shukuru Kawambwa

36. Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Philipo Mulugo

37. Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Haji Hussein Mpanda

38. Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Lucy Nkya

39. Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka

40. Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Dk. Makongoro Mahanga

41. Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba

42. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Ummy Ali Mwalimu

43. Waziri Wizara ya Elimu, Habari, Vijana na Michezo - Emmanuel John Nchimbi

44. Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Habari, Vijana na Michezo - Dk. Phenela Mukangala

45. Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Samuel John Sitta

46. Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Abdallah Juma Abdallah

47. Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Profesa Jumanne Maghembe

48. Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Christopher Chizza

49. Waziri Wizara ya Maji - Profesa Mark James Mwandosya

50.Naibu Waziri Wizara ya Maji - Jerryson Lwenge

 

Ningetamani kuona wadau kutupa nyeti [Vimeo] vya kila mmoja
kama vipo,Mfano mmoja majuzi kaminywa na mama makinda akiomba muongozo akideclare interest issue ya UDA si mwingine bali Makongoro.
 
Kumbe ww mvivu umefuata nini huku JF?

16. Waziri wa Katiba na Sheria - Selina Kombani

Naanza na huyu:

Kazi yake so far zimemlemea- Kaanza tu na kufanya blunder - Kukataa kutupa katiba mpya - yalipomzidia kakubali ila katujia na Muswaada wa hovyo mpaka serikali ikabidi iuchomoe bungeni. Kaulizwa kasema 'alikuwaanatingisha kiberiti' (maneno ya dharau sana kwa watu wanaokulipa mshahara)Kakaa kimya na huo mswada naona anatuvizia tena kwa mara nyingine - Naona huyu shughuli inamelemea apishe.

nawahi nitarudi tena
 
Hili siyo baraza la Mawaziri aliloahidi watanzania katika ule Mdahalo siku chache kabla ya uchaguzi ambapo aliahidi watanzania atapunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kuteua mawaziri wachapakazi kwelikweli-so ili tulijadili tunakutuma ukajadiliane naye kwanza atekeleze ile ahadi yake then ndo tutajadili, otherwise watu watashuka na matusi hapa mtakuja lalamika na kuifungia thread bure! Mwambie kwa kifupi katika hili ukimtoa magufuli hakuna waziri mwingine ambaye ni mchapakazi, wote vilaza na hatuhitaji cheo kinachoitwa naibu waziri ambao infact si memba wa baraza la mawaziri! kazi yao nini?
 
Wafuatao hawafai because of non performance:-

Makongoro Mahanga

Ngeleja

Malima

Wassira

Kombani

Hussein Mwinyi
 
Kumbe ww mvivu umefuata nini huku JF?

16. Waziri wa Katiba na Sheria - Selina Kombani

Naanza na huyu:

Kazi yake so far zimemlemea- Kaanza tu na kufanya blunder - Kukataa kutupa katiba mpya - yalipomzidia kakubali ila katujia na Muswaada wa hovyo mpaka serikali ikabidi iuchomoe bungeni. Kaulizwa kasema 'alikuwaanatingisha kiberiti' (maneno ya dharau sana kwa watu wanaokulipa mshahara)Kakaa kimya na huo mswada naona anatuvizia tena kwa mara nyingine - Naona huyu shughuli inamelemea apishe.

nawahi nitarudi tena

Haya, just imagine kwa maneno hayo then bado mtu anaendelea kuwa waziri tu-tena ameandaa muswaada ambao kule mlikokufanya umamani watu wameuchana live bado tu hajaresign wala kutimuliwa sasa, bado mnataka tuwajadilie baraza lenu tu lipi?
 
Sioni wa kumsia hapo maana wote wamebebanabebana tu, na kufikishana hapo walipo, hlf ile falsafa yao ya collective responsibility (uwajibikaji wa pamoja), inanifanya niamini kuwa samaki mmoja akioza wote wameoza tupa wote jalalani.
Dk. Slaa aliwahi kusema hata uwe malaika ndani ya CCM huwezi kutenda haki.
Nimejaribu kuangalia kidogo hapa;
1. Magufuli, Mwanri, Tibaijuka nk, hawa wanabanwa sana na ile kanuni.
2. Sitta &Mwakyembe, hawa siasa zao ni za kinafikifiki.
3. Lukuvi, Sofia, ngeleja, Nahodha n.k, hawa ni vinara wa vilaza.
 
Maghembe - huyu ni Mbunge wa jimbo langu ambaye amechaguliwa na wanafunzi wa kidato cha nne na sita. Si mbunge wa wananchi wa Mwanga, by the way ni gamba, ni kilaza . Ni mbunge pekee aliyeulizwa kuhusu maji na wananchi wa Mwaniko akawaambia walete ng'ombe mweusi watambike ili maji yatoke kwenye mabomba kwani Mzimu unaoitwa VULUE umechukue maji yake.
Ni waziri ambaye uteuzi wake ni kizungumkuti. hakufanya vizuri wizara za kazi,maliasili na utalii na pia akatutumbukiza shimoni zaidi ya mungai kwenye elimu. anadai ni mtaalamu aliebobea wa kilimo lakini ziwa Jipe lililoko jmboni mwake limejaa magugumaji , maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai waliopo wapo karibuni kumalizika. kama mnamuamini kuwa atawafikisha kwenye kilimo imekula kwenu complete. Namfahamu vizuri sana huyu jamaa ana sifa ya ziada ya ushirikina
 
Maghembe - huyu ni Mbunge wa jimbo langu ambaye amechaguliwa na wanafunzi wa kidato cha nne na sita. Si mbunge wa wananchi wa Mwanga, by the way ni gamba, ni kilaza . Ni mbunge pekee aliyeulizwa kuhusu maji na wananchi wa Mwaniko akawaambia walete ng'ombe mweusi watambike ili maji yatoke kwenye mabomba kwani Mzimu unaoitwa VULUE umechukue maji yake.
Ni waziri ambaye uteuzi wake ni kizungumkuti. hakufanya vizuri wizara za kazi,maliasili na utalii na pia akatutumbukiza shimoni zaidi ya mungai kwenye elimu. anadai ni mtaalamu aliebobea wa kilimo lakini ziwa Jipe lililoko jmboni mwake limejaa magugumaji , maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai waliopo wapo karibuni kumalizika. kama mnamuamini kuwa atawafikisha kwenye kilimo imekula kwenu complete. Namfahamu vizuri sana huyu jamaa ana sifa ya ziada ya ushirikina

Kama hilyo sentensi ya juu alisema, bac hapo chini ni agreeable!
 
wote vilaza wakutupwa,nafuu ma'kufuli,hawana kitu kabisa,wanatupa mzigo tu!hata aliyewateua hamna kitu kabisa
 
Tulichambue au tulichambe??
Mkuu hakuna kitu! mimi sasa hivi najiongoza mwenyewe Rais mimi First lady Mke wangu, waziri mimi,Mbunge mimi, Katibu mkuu wa Nishati mimi, yaani ya Taifa langu ni Nyumba yangu. SIMTAMBUI RAIS WALA WATEULE WAKE WOTE kwni ndio wanazidi kunitia umaskini
 
  • Awali nilimwamini sana SS kuwa waziri bora sasa hapana,
  • Mwakyembe nilidhani ataonyesha umwamba sasa kimya
  • Tibaijuka alianza kwa kasi nzuri sasa sijui amehama nchi maana hasikiki
  • Lukuvi anajitahidi sana kuongea kwa mantiki lakini sometime anakuwa off
  • TUMAINI LANGU PEKEE LIPO KWA JOHN MAGUFURI
 
.............Huyu Hawa Ghasia vp? Sijaona mchango wa wanaJF kuhusu huyu waziri,kwa mawazo yangu ndio waziri kilaza zaidi akifatiwa na Ngeleja na Omari Nundu anafuatia.......
 
Mawaziri hawana book shelves ya kusoma vitabu majumbani mwao kila mara ili kupanua mawazo yao. Halafu, majimboni mwao hamna hata maktaba! wewe unategemea nini kama si kuwa kilaza. Waliziri wa ulinzi unaambiwa hata kitabu cha enetebe Raid hajakisoma, . Wewe unategemea nini kwa waziri huyo?
 
Back
Top Bottom