Tulianzia hapa Ugomvi wangu na Mwenye Nyumba mpaka kufika mwishoni hali ilikuwa mbaya

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
742
1,000
Miaka hiyo nimetoka chuo tu nikapata kazi sehemu fulani bado nikiwa home. Nilijiwekea tu malengo kuwa kuepuka usumbufu wa usafiri in a year lazima niwe na gari.

Nilinunua gari nikiwa home then nikanza mchakato wa kuanza maisha binafsi. Nikatafuta nyumba ya kuanzia maisha. Nilipata vyumba viwili kimoja master, sebule, jiko na public toilet.

Tulikuwa tunaishi compound moja na mwenye nyumba, limama moja jeupe halina mume but linapendeza na halitaki kuzeeka.

Siku ya kwanza alikuja akitaka nimpeleke salon mvua ilikuwa inanyesha. Nilishtuka kidogo but nikajizoa zoa toka chumbani nikampeleka salon. Kufika akataka nikawasalimie wadogo zake mle ndani. Nikaenda nikarudi zangu kwenye gari, alinambia 30 mins tu tunaondoka. Baada ya saa akaja akasema now turudi home Ikapita.

Mara ya pili akanifuata siku hiyo Jumamosi eti nimpeleke kwenye shughuli ya wenzie Kinondoni, nilimkatalia tu nikamwambia leo napumzika sijisikii vizuri. Akanambia basi nimpatie funguo za gari, nilimwambia hapana huwa siazimishi gari akaongea mwishowe akaondoka.

Mara ya tatu siku hiyo asubuhi naenda job naye akawa ananisubiri getini, natoka akaja akasimamisha akapanda kushoto mbele nikamsalimia. Basi mimi nafuata njia ya mwenda job tumefika sehemu ananambia niingie kulia nimpitishe kwa shoga yake wanaenda jiandaa kuna function.

Nlimwambia nachelewa kazini, siku hiyo akanitolea uvivu kuwa aliniona mimi mstaarabu kumbe bure kabisa. Simheshimu na simjali kila kitu namkatalia tu hayo magari ni sawa na kutembea na jeneza tu anytime naweza vuta nalo gari hata kwa ajali. Niishi vizuri na watu nivae viatu.

Nlishangaa sababu mpaka hapo nilikuwa na viatu si chini ya pair 7 sikununuliwa na mtu hata mmoja. So sikuelewa dhana yake ya kuishi na watu ili nivae viatu.

Tukaachana hapo nilimpa 6000 achukue bajaji akapokea. Jioni akaleta barua kodi imepanda kwa tsh 120,000 nzima katk ile ya kwanza. Bahati nzuri nlilipa mwaka na mpaka that time nilikuwa nimekaa miezi 3. Nilipokea barua nikasema sawa.

Baada ya siku tatu ananifuata kuwa nimlipe hiyo iliyozidi. Nilimweleza kwa sasa tunaishi na mkataba wa kwanza mpaka kodi ikiisha ndo tutaanza upya ikiwa nitataka kuendelea kukaa pale.

Yule mama alinisema sana kuwa aliona mimi nitakuwa kijana mstaarabu tena msomi ila nimemwonesha mhuni na mswahili sana. Akataka twende kwa mjumbe, nilimwambia aende halafu nije kuitwa akanishtaki.

Akatoka hakuja niiita week, ikafuatia sasa anataka nami nifagie uwanja mle ndani kulikuwa na mpangaji mwingine ana house girl nikamwambia afagie nitampatia 10,000 kila mwisho wa mwezi. Yule binti alifurahi sana.

Mama mwenye nyumba kusikia hivyo alinifuata siku hiyo amekasirika, kama nina hela sana ningempa yeye. Why nilipe 10,000 kwa kufagia tu? Akasema nina ujeuri sana.

Baadaye visa vikawa vingi mara aje na khanga tu home kuuliza kama naweza mwelekeza kutumia laptop, mara aje nimsetie simu yake. Mara aje na hili, mara lile.

Nikaanza kuwa narudi late, naondoka early. Baadaye nikaona isiwe shida nikaanza mleta girlfriend wangu mwanachuo sometimes analala, nongwa ikawa kubwa.

Mama mswahili anampiga vijembe yule binti mpaka basi. Yakaendelea mpaka kodi inakaribia kuisha mimi nikatafuta nyumba nyingine. Siku nahama hakujua. Tulikuja onana nimehamisha kila kitu saa 3 usiku nikagonga mlango kwake kumkabidhi funguo.

Yule mama alisema sana. But akitaka niendelee kukaa pale tusameheane. Sikuwahi onana naye tena. Mpaka jana nimekutana naye amechoka sana. Zaidi ya miaka 15 sasa. Amenikumbusha mbali sana.
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,469
2,000
Baada ya kukutana naye hiyo miaka 15 kukutana tena, ungemwambia unaishi kwako sio pale ulipohamia, naona angeanguka, ila aliondoka kwa jeuri akijua unapanga bado.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom