Ngoja watakaosoma na kuelewa hii story yako waje watakushauri..
Mimi nimesoma nikaanza kuelewa, nilivyofika katikatika nikagundua sijalewa, nikaendelea kusoma mpaka mwisho nikagundua niko cofused.
Soma halafu unisimulieMh kwani anatatizo gani haswa? mie hata sijasoma
In short ni huyo binti ameanza biashara na mwenzake ila mwenzake ndo inaonyesha anachukua faida yote ya biashara bila kumgawia, anauliza AFANYEJE?
mi nimesomana kuelewa...hapo we kama vipi anza maisha yako achana naye maana akufukuzaye hakuambii toka...taayari kuna kulewa pesa hapo....tafuta kwako tuu uishikama weweMimi ninakaa kwa rafiki yangu ambae alishawahi kua wifi yangu i mean alikuwa mke wa kaka mtoto wa mama mkubwa but waliachana kitambo tangu nikiwa Mbeya kipindi hicho naishi na baba watoto wangu.Walipoachana nikawa nakaa nae kwangu yani tunalala kitanda kimoja na yeye na mume wangu kipindi hicho nina ujauzito na yeye alikuwa ana mtoto wa miaka kama miwili n kitu.
Nilikuwa nakaa nae tunachokula ndio anachokula yeye sikuwahi kumnyanyasa kwa namna yoyote ile, mpaka alipoamua mwenyewe kuondoka, siku zikaenda hatimae akapata mtu ambae ndio yuko nae mpaka sasa, ni mtu mzima huyo mumewe baada ya mimi kuachana na baba watoto wangu niliondoka Mbeya nikahamia Kibaha kwa mama mkubwa.
Nimekaa baadae nikajiunga na chuo kimoja nikasoma course ya counselling kwa ngazi ya cheti nilipomaliza nikajiendeleza na diploma miaka yangu miwili ilipoisha nikarudi Kibaha nikawa nafatilia ajira lakini mwisho wa siku nikakata tamaa sababu ya majaribu nilikua nakutana nayo kila sehemu niombayo kazi, unakuta intview napiga ila wanaatka hongo ya mapenzi nakimbia.
Basi nikawa niko zangu tu nyumbani.Huyu rafiki yangu alikua tayari yuko Dar kuna siku akaniita na kusema Khadija huko umekaa tu bora uje uku tufikirie kitu cha kufanya uwe unapata hata vimiambili maana pale nyumbani sikua na maelewano mazuri na mama mkubwa kwa kua nilikuwa nakaa bure pale kwake sichangii umeme wala maji.Basi nikaona sawa nikakaa kwa mda tena nikarudi Kibaha.
Ndio nikapata wazo la kumpigia simu mama mkwe wangu mana nao waligoma kumsaidia mwanangu akiwa chini yangu. Nilikua napika sambusa ndio mwanangu apate ada ya shule na chakula libaba mtu halina time. Niliumia nikaona sawa wacha nikubali aende Moshi ingawa sikupenda mwanangu akae mbali nami nilikuwa nataka nipate kuwa huru kutafuta kwani nisingeeza kumuacha mwanangu Kibaha mimi nikae mjini nikampeleka.
Nilipotulia ndio nikaja tena kwa rafiki yangu ambae niko nae mpaka leo tulikaa na akaniambia tuwe tunaenda kupiga picha kwenye maduka ya watu kama ni viatu au pochi then tunawarushia watu tunaowajua wakipenda tukaombe tuuziwe kwa jumla na tuwauzie tutakaopata.
Tukawa tunafanya hivyo siku zinaenda tukaja kupata dada mmoja alikua Mabibo anauza pochi jumla 31,000, alikua anaturushia picha ya mizigo ambao utakuja na tukawa tunakusanya oda mizigo ukifika kama nina oda mbili nae tano au zaidi tunaenda tunachukua tunampelekea wateja.
Siku zinaenda mpaka tulipokuja kujua sehemu ambayo alikua akichukulia yule dada wa Mabibo kumbe alikua anachukua kwa mtu hapa Kariakoo.
Tulipomjua tukawa na sisi tunachukua kwa huyo mtu, tukipata oda hivyo hivyo mpaka tukazoeleka pale kuna siku yule baba akatuita na kutuambia kama tuko serious tufanye nae kazi.
Yani awe anatupa mzigo tunauza tunapeleka pesa yake tukamwambia sisi pia tulipenda ila tulikua hatujui ni vipi tutakuaproach utuamini, akasema mnaishi wapi tu kasema hapa hapa Karakoo mtaa wa Uhuru na tutakua tunauzia pale pale nyumbani akakubli akawa anatupa mzigo tulianza na pisi mia, ikaenda mpaka tukawa tunachukua pisi 400.
Tukasema nyumbani sio salama akatafuta duka mwenzangu tukapata Livingston tukahamia kule tulipohamia kule muuzaji mkubwa wa dukani nikawa mie kodi yaa miezi sita ilipoisha tukarudi home.
Baadae tukapata mtaa wa Kongo ambako tupo mpaka sasa na mpaka sasa ilifikia tunachukua mpaka pisi 800 au 900 sasa cha ajabu ni hivi tangu tuanze nakumbuka faida ashawahi kunigawia mara moja na hivi sasa anasafiri mwenyewe kwenda China, ingawa pesa ya kwenda China ameongezewa na shemeji yani mumewe na sasa hivi naona kama imani kwangu imepungua.
Hivi simuelewi mda mwingine kiukweli w akaamka kanuna bila sababu mimi simuulizi nafanya yangu, sasa ni mda tangu karudi China mzigo wanazingua bado haujafika mpaka Leo, sasa naomba mniambie nimuingie vipi?Maana tulianza wote but now naona kama yeye ndio mmiliki pekee wa ile biashara na mimi sielewi position yangu maana silipwi chochote na mimi ndio mtunza kumbukmbu na mkaa na mahesabu.
Niko kumnufaisha mwenzengu wakati kwangu kunateketea, na kubwa ni kwamba ananitumia sasa, kwa ufala wangu nimekuwa kama kijakazi maana nowdays tulipangiana ratiba home tulikua hatuna mdada wa kazi kua mimi niwe napika mchana yeye usiku but daily mi zamu yangu nitafanya, but mwenzangu apiki zaidi atawapa watoto chips basi siku zingine atanunua za nyumba nzima siku nyingine watoto na yeye tu wangu mtajijua.
Hapo katikati alitoa pesa akalipia viatu kama pea kumi na tatu eti akanipa sasa sijui ndio kanipa kama mtaji hivyo pea 13 sielewi, Am so comfused.
Nowdays nikiwa dukani sister yake tunatizamana nae maduka utaona akija mteja anakuja au akitoka anakuja umeuza nini, mwenyewe anataka kila kitu kiandikwe hataki kupata hasara tena sasa najiuliza mi nishawahi kuingiza hasara humu? Au kuiba? AFANYEJE?
jiongeze mwabie akulipe mshahara anza kujiengua pole pole .. hapo we ni mfanyakazi tu