Uchaguzi 2020 Tulia Trust imefanya mambo makubwa Mbeya kuliko mbunge yeyote yule katika historia ya jiji hilo

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,478
20,390
Sugu ana street creds lakini huwa kuna muda vijana inabidi walipe kodi za nyumba,wanunue vocha, wakina mama wawe na vikundi vyenye hela na mitaji,watoto waende shule nk nk hapo ndipo anapokuja Tulia kama mbunge sahihi kwa wana Mbeya.

Nimekaa Mbeya kwa muda kidogo nakuona mambo yanavyokwenda kwenye ground kwa kweli suala la Sugu kurudi sio mjadala tena kama Dada Tulia atakuwa mgombea ubunge Mbeya.

Siasa za sasa hivi zinahitaji wanasiasa wanaowainuia wananchi kiuchumi na sio kuwainua kwenye maandamano pekee.

Tulia trust imewatoa vijana mitaani imewapa pikipiki,bajaji,wakina mama wamewezeshwa mitaji na mikopo,madarasa yamejengwa nk
 
Mi naona aendelee kutoa hivyo hivyo na hiyo trust yake,asigombee ili aiendeshe trust yake vizuri zaidi!Au ni ile nipe nikupe?Kwamba ni rushwa kwa wananchi?Mtu hawezi kutoa bila kutegemea kitu in return?
 
Nani alisema kazi ua Mbunge ni hayo yanayofanyika na Tulia Trust? Watanzania mtaondokana lini na Tabia ya Ombaomba, na ya kutarajia vitu vya bure? Unafikiri hao wamachinga na akina mama, na madereva wa bajaji ndio wakazi pekee wa jiji la Mbeya? Mbona mawazo ya kimaskini sana. Kazi ya Mbunge sio kugawa pesa Bali kujenga uwezo. Kazi ya Mbunge siyo kudanganya wanawake na vijana bali kuwakilisha jamii yote Bungeni. Sifa za Mbunge ni kukubalika na jamii, siyo kupumbaza jamii. Jukumu la Mbunge ni Uwakilishi na Utetezi; Jukumu ambalo Sugu kalifanya kwa ufasaha na weledi.
Acheni kupokea shilingi chache, kuuza akili zenu. Acheni kupokea mikopo duni, kuondoa ubunifu wenu. Watu wa Mbeya ni Wachapakazi, Msikubali Kufundishwa Uzembe, Utegemezi na Utwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo naona unanipa taarifa ya kuwa , Tulia Trust imepelekwa ili impigie Tulia kampeni ..
 
Hapo naona unanipa taarifa ya kuwa , Tulia Trust imepelekwa ili impigie Tulia kampeni ..

Mbeya mjini huyo Tulia bora atulie kwani kwa haki bin haki hapati kitu ila kwa mazoea ya hivi karibuni wanaweza na dunia inatambua hivyo
 
25'000 per day ambayo dereva bajaji anapaswa kupeleka kwa boss wake ni mzigo mkubwa
Ila acha tuone, yote ni heri kama yanafanywa kwa nia njema
Sugu ana street creds lakini huwa kuna muda vijana inabidi walipe kodi za nyumba,wanunue vocha, wakina mama wawe na vikundi vyenye hela na mitaji,watoto waende shule nk nk hapo ndipo anapokuja Tulia kama mbunge sahihi kwa wana Mbeya.

Nimekaa Mbeya kwa muda kidogo nakuona mambo yanavyokwenda kwenye ground kwa kweli suala la Sugu kurudi sio mjadala tena kama Dada Tulia atakuwa mgombea ubunge Mbeya.

Siasa za sasa hivi zinahitaji wanasiasa wanaowainuia wananchi kiuchumi na sio kuwainua kwenye maandamano pekee.

Tulia trust imewatoa vijana mitaani imewapa pikipiki,bajaji,wakina mama wamewezeshwa mitaji na mikopo,madarasa yamejengwa nk
 
Naunga mkono hoja, na kwa vile hadi jeneza lilishazikwa, aliyepo ni msukule tuu, Tulia atulie tuli, jeneza lifanye mambo, then yeye atapita bila kupingwa.
P
 
sema Tulia Trust imefanya mambo makubwa Mbeya mjiniya 'kutoa rushwa' kuliko wabunge woote waliopita wa CCM wa Mbeya mjini kwa ujumla
 
Mkuu sugu tilimwamini ila keki anakula peke yake hatukumbuki wapiga kura

Hela ya kujenga magest anayo ila ya kuinua Wananchi wake hana

Tunasubiri October tumfute rasmi Mbeya
Kwani unafikili ananjaa Kama wewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom