Kinachomfanya mtu kuwa ni mbunge ni pale anapokuwa ni mwanachama hai wa chama cha siasa na hii ni kwa mujibu wa katiba. Bunge linapaswa KUHESHIMU ibara ya 71(1)(e) ya KATIBA ya Tanzania.
Bunge siyo Mamlaka ya Rufaa ya Wanachama wa vyama vya Siasa. Kwa maana hiyo, Bunge halina uhalali wowote kujadili taratibu za KINIDHAMU ndani ya CHAMA CHA SIASA. Kwenye sakata linaloendelea hivi sasa Spika Tulia Ackson amepotoka.
IELEWEKE KWAMBA:-
Kamati Kuu na hatimae Baraza Kuu la CHADEMA lilitoa maamuzi juu ya Uanachama wa Halima Mdee na Wenzake na sio Ubunge wao. Kwa lugha rahisi CHADEMA waliwavua uanachama na sio Ubunge wao;
IELEWEKE KWAMBA:-
Kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipengele kidogo cha (e) cha Ibara hiyo kinaeleleza iwapo mbunge atakoma kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge, basi atapoteza ubunge wake.
UTATA:-
Kimsingi Halima Mdee na wenzake walikuwa wanachama wa CHADEMA na hawakuteuliwa na chama cha siasa (CHADEMA) kuwa wabunge. Hivyo kwenye muono wa CHADEMA, Halima na wenzake sio wabunge. Taarifa iliyokwenda kwa Spika ni kuvuliwa uanachama kwa wale wanaoitwa wabunge na Ofisi ya Bunge. Sio Wabunge wa CHADEMA kwa kuwa sio wanachama wa CHADEMA.
Ipo hoja kwamba sio kazi ya Bunge au Spika kuhoji wamepatikanaje kama barua ya utambulisho ya NEC imemfikia. Lakini vilevile sio kazi ya Spika kupindisha maamuzi ya vikao halali vya chama badala ya kufuata takwa la kikatiba, ibara ya 71 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipengele kidogo cha (e). Mchakato wa kisheria wa kuhoji maamuzi ya chama haupaswi kuwa chini ya mwamvuli wa kinga ya Spika wa bunge bali ni mchakato wa kimahakama nje ya bunge.
Zuio lolote la kimahakama dhidi ya Ubunge wao ni zuio dhidi ya Ofisi ya Bunge katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba kwa wale ambao wanawatambua kama wabunge ambayo tayari hawana chama cha siasa ambacho kinawadhamini. Kwa kifupi sio wanachama wa Chama cha Siasa kwa mujibu wa katiba ya chama husika.
KIMSINGI:-
Spika wa Bunge alipaswa kutimizima jukumu lake la kikatiba na Mdee wa wenzake kufuata taratibu zao za kisheria wakiwa nje ya Bunge.
Inawezekanaje Judicial Injunction (Zuio la Mahakama) linatoka baada ya kauli ya Spika lakini Spika anasema kulikuwa na zuio kabla?
HITIMISHO
Kwa kuwa mchakato wote wa kuwapata wabunge hao 19 kutoka CHADEMA kuwa batili, mjadala mpana ulipaswa kujikita katika uadilifu wa Ofisi ya Bunge na Tume wa Taifa uchaguzi. Utaratibu wa kuwapata wabunge haupaswi kuishia CHADEMA, bali unapaswa kuanzia kwenye mchakato mzima wa kuwapata wale wanaoitwa wabunge.