Spika Dkt. Tulia ajuzwe Wabunge 19 hawajawahi kuteuliwa na CHADEMA. Wameingia kwa kufoji nyaraka

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Hata kama Spika atawachukulia kuwa NI wanachama halali wa Chadema. Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.

Na wanaoandaa nyaraka hizo wameshatoa taarifa za sahihi zao na majina yao kufojiwa. Sijui wanataka Nani aje asibitishe Hilo. Wakati wewe unasema huyu ndio aliyeandaa Orodha ya Wabunge. Kamati kuu inakaa kikao inakupa barua kuwa hatukuandaa sisi. Na wanakujulisha Spika kuwa hao NI waalifu wamefoji nyaraka.

CHADEMA haina haja ya kutoa taarifa za uhai au kutokuwa mwanachama ili kuonesha uhalali wa akina mdee. Sababu hawatakiwi kuwepo bungeni sababu wameingia kwa njia haramu.

Basi Spika ajikite kuonesha uhalali wa nyaraka zilizotumika na majina na sahihi na katibu aliyepeleka majina kwa spika. Na vikao vilivyopitisha majina hayo.

Kushindwa kufanya hivyo kutaendelea kuoneshaa dunia kuwa Sheria ya Kinga dhidi ya kushitakiwa kwa spika ililetwa ili kumfanya Spika kutoa maamuzi ya kuangamiza upinzani. Na kuwe akuna mwanya wa kuipata haki kokote atakapoweza kuitafunga au kuipokonya kwa nguvu.

Kwa Sheria hiyo Spika Sasa ameweza kuvunja katiba bila hofu ya kushitakiwa, kupingwa Wala maamuzi yake kukatiwa rufaa.
 
Ata Kama Spika atawachukulia kuwa NI wanachama halali wa chadema. Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.

Na wanaoandaa nyaraka hizo wameshatoa taarifa za sahihi zao na majina yao kufojiwa. Sijui wanataka Nani aje asibitishe Hilo. Wakati wewe unasema huyu ndio aliyeandaa Orodha ya Wabunge. Kamati kuu inakaa kikao inakupa barua kuwa hatukuandaa sisi. Na wanakujulisha Spika kuwa hao NI waalifu wamefoji nyaraka.

Chadema haina haja ya kutoa taarifa za uhai au kutokuwa mwanachama ili kuonesha uhalali wa akina mdee. Sababu hawatakiwi kuwepo bungeni sababu wameingia kwa njia haramu.

Basi Spika ajikite kuonesha uhalali wa nyaraka zilizotumika na majina na sahihi na katibu aliyepeleka majina kwa spika. Na vikao vilivyopitisha majina hayo.

Kushindwa kufanya hivyo kutaendelea kuoneshaa dunia kuwa Sheria ya Kinga dhidi ya kushitakiwa kwa spika ililetwa ili kumfanya Spika kutoa maamuzi ya kuangamiza upinzani. Na kuwe akuna mwanya wa kuipata haki kokote atakapoweza kuitafunga au kuipokonya kwa nguvu. Kwa Sheria hiyo Spika Sasa ameweza kuvunja katiba bila hofu ya kushitakiwa, kupingwa Wala maamuzi yake kukatiwa rufaa.
 
COVID 19

20220214_201744.jpg

20220214_201655.jpg

20220214_201658.jpg
 
Ukweli mtupu umenena.ila alichoamua spika wa sasa na hata aliyepita ni kanyanga twende.
Chadema kama chama wafanye mengine swala la kina Mdee kutolewa bungeni wasahau.
Mwamuzi ni november 2025 baada ya uchaguzi
 
Hata kama Spika atawachukulia kuwa NI wanachama halali wa Chadema. Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.

Na wanaoandaa nyaraka hizo wameshatoa taarifa za sahihi zao na majina yao kufojiwa. Sijui wanataka Nani aje asibitishe Hilo. Wakati wewe unasema huyu ndio aliyeandaa Orodha ya Wabunge. Kamati kuu inakaa kikao inakupa barua kuwa hatukuandaa sisi. Na wanakujulisha Spika kuwa hao NI waalifu wamefoji nyaraka.

CHADEMA haina haja ya kutoa taarifa za uhai au kutokuwa mwanachama ili kuonesha uhalali wa akina mdee. Sababu hawatakiwi kuwepo bungeni sababu wameingia kwa njia haramu.

Basi Spika ajikite kuonesha uhalali wa nyaraka zilizotumika na majina na sahihi na katibu aliyepeleka majina kwa spika. Na vikao vilivyopitisha majina hayo.

Kushindwa kufanya hivyo kutaendelea kuoneshaa dunia kuwa Sheria ya Kinga dhidi ya kushitakiwa kwa spika ililetwa ili kumfanya Spika kutoa maamuzi ya kuangamiza upinzani. Na kuwe akuna mwanya wa kuipata haki kokote atakapoweza kuitafunga au kuipokonya kwa nguvu.

Kwa Sheria hiyo Spika Sasa ameweza kuvunja katiba bila hofu ya kushitakiwa, kupingwa Wala maamuzi yake kukatiwa rufaa.
Kwanini yeye aliingia kwa haki bungeni? kwanza hatuna bunge hata kidogo
 
Ajuzwe kwani yeye sialikuwa naibu sipika,wanajidanganya mda utakuja kusema, naninaona huko mbeleni watakuja kulipa hiyo mishahala na posho wanazozipata hisivyo sawa Kodi zetu wananchi
 
..Mkurugenzi wa makosa ya jinai / DCI alipaswa kuchunguza kilichotokea na kuwakamata wahusika.

..Waandishi wa habari wachunguzi walitakiwa kuchangamka na kudodosa ili kuibua KASHFA na kuwabaini wahusika.
Nimemsikiliza juzi Spika Tulia nikasikitika sana. Sijui kwanini aliamua kujibu maswali yale
Amedhalilika sana ukizingatia ni mwanasheria tena mhadhiri. Ilikuwa aibu

Tulia anasema suala waulizwe Tume ya uchaguzi. Sophia alipotimuliwa JYN alitangaza kupokea barua ya CCM. Sheria za nchi zinasema mtu akifukuzwa chama anapoteza Ubunge. Hivi hili nalo mhadhiri wa sheria halijui

Pili, anasema, Chadema wafuate taratibu! pathetic.
Taratibu za chama zinasimamiwa na chama si Spika wa Bunge.

Ikiwa alishajivua nafasi kwa kutupa mzigo kwa tume, ni taratibu gani za Bunge zinazoelekeza ''utaratibu ufuatwe'? Hapa watu wasifikirie utumbo wa Ndugai alioutengeneza kulinda COVID-19 kwa sababu zake

Chadema wametoa tuhuma nzito za kufoji nyaraka kutoka Tume ya uchaguzi. Ni wajibu wa vyombo husika kufuatilia. Wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea

Kisheria Tulia amechaguliwa na baadhi ya watu wasiowabunge kinyume cha sheria.

Tulia ni Spika, mwanasheria na Mhadhiri wa chuo kikuu! nadhani sisi kama nchi tujiulize
 
Hata kama Spika atawachukulia kuwa NI wanachama halali wa Chadema. Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.
Hilo la forgery mbona haliko kwenye barua? Kilichoandikwa ni "njama za kujiteua huku wakijua hiyo ni kazi ya kamati kuu". Njia pekee ya kudhihirisha kama ni kweli au la ni kutoa orodha ya wateule wa Kamati Kuu tuone kama ni majina tofauti. Hyo oroda mbona hatolewi? Wanaogopa ina majina ya wake, shangazi au dada wa vinara Mwenyekiti Mbowe, Mgombea Urais Tundu Lissu na wafadhili Lowassa na Nyalandu kwani kulikuwa na makubaliano.
 
..huko "kujiteua" ndio forgery yenyewe.

..Na hapo Mkurugenzi wa makosa ya jinai alitakiwa atume mashushu kujua nini kimetokea.
 
Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.

Na wanaoandaa nyaraka hizo wameshatoa taarifa za sahihi zao na majina yao kufojiwa.
Mkuu William Mshumbusi , with due respect, asante kwa bandiko hili. Mabadiliko kama haya yanasaidia sana kuonyesha matundu ya udhaifu mkubwa wa Chadema in doing the right thing and doing it right.

Forgery ni kosa la jinai, jee kuandika barua kwa Spika au kuzungumza na press ndio the the right way ku deal na forgery?.

Kama kweli kuna forgery, this is a police case. Kabla ya kuchukua hatua yoyote, Chadema was supposed to do a due diligence report kuiona barua iliyoandikwa, imeandikwa na nani, imesainiwa na nani, imepelekwa na nani, kwa despatch gani na copy yake. Kama hivi vyote havipo ofisini, that means ni forgery, hatua ya pili ni kuripoti polisi, hivyo polisi wangechunguza na Chadema ndipo wangepatiwa copy ya barua ya uteuzi iliyopelekwa NEC.

Ni kupitia barua hiyo ndipo jinai ya forgery ingethitibishwa na mtu pekee wa kuthibitisha jinai hiyo ni the one who alleges, must prove!.

Wapenzi wa kweli wa Chadema, watapenda kuona Chadema ikifanya the right thing, sio kuisifia au kuinyamazia wakati inafanya madudu, sisi wakosoaji wa Chadema, tunao onyesha madudu ya Chadema ndio tunaisaidia Chadema kuliko wanaoisifia!.

Kama NEC imepalekewa barua bonafide genuine ya uteuzi, ikawateua na kumpelekea Spika, akawaapisha. Baada ya kuapishwa huku nyuma Chadema ikaitisha a kangaroo court ya CC yake kuwavua uanachama, hata ningekuwa mimi nisinge kubali uhuni huu!.

Kwa vile Chadema inayo katiba yake na inao utaratibu wa kufuata kutimua wanachama wao, siku zote timua timua zote za Chadema, kwanini utaratibu huu haufuatwi?.

Hii tabia ya CC ya Chadema kukaa kama a kangaroo court na kutimua tuu wanachama wake, imeanza kuzoeleka, lakini sasa kwa Mdee imekutana na kisiki cha mpingo!.

Nashauri, kama tunapenda Chadema kwa dhati, tuisaidie to do the right thing. Mimi japo sio Chadema lakini ninaisaidia sana Chadema kwa ushauri wa bure kama hapa
P
 
..Mkurugenzi wa makosa ya jinai / DCI alipaswa kuchunguza kilichotokea na kuwakamata wahusika.

..Waandishi wa habari wachunguzi walitakiwa kuchangamka na kudodosa ili kuibua KASHFA na kuwabaini wahusika.

Cc Pascal Mayalla, Nguruvi3, Petro E. Mselewa , Tindo
Mkuu JokaKuu , kwanza naunga mkono hoja, DCI kuchunguza jinai hii, ila ili DCI achunguze ni lazima kwanza kuwepo mlalamikaji. Chadema lazima iripoti polisi ndipo hatua za uchunguzi zifuate.

Waandishi wa habari za kichunguzi tupo, ila kabla hata sisi hatujafanya chochote, hatua ya kwanza ni kuiona barua ya uteuzi kutoka Chadema kwenda NEC. Bila Chadema kutoa ushirikiano kwenye hili, no IJ journalist can do anything!.
Chadema ina matatizo ya handling some issues.
P
 
Chadema wametoa tuhuma nzito za kufoji nyaraka kutoka Tume ya uchaguzi. Ni wajibu wa vyombo husika kufuatilia. Wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea
Mkuu Nguruvi3 , nashauri tuisaidie Chadema to do the right thing. Chadema wametoa tuhuma nzito za forgery, kuwa barua ya uteuzi wa wabunge hao wa viti maalum wa Chadema, imefojiwa. Kwanini mpaka sasa Chadema haijaripoti polisi jinai hii ili hatua stahiki zichukuliwe?.
P
 
Mkuu JokaKuu , kwanza naunga mkono hoja, DCI kuchunguza jinai hii, ila ili DCI achunguze ni lazima kwanza kuwepo mlalamikaji. Chadema lazima iripoti polisi ndipo hatua za uchunguzi zifuate.

Waandishi wa habari za kichunguzi tupo, ila kabla hata sisi hatujafanya chochote, hatua ya kwanza ni kuiona barua ya uteuzi kutoka Chadema kwenda NEC. Bila Chadema kutoa ushirikiano kwenye hili, no IJ journalist can do anything!.
Chadema ina matatizo ya handling some issues.
P

..kwa mazingira haya sio lazima pawepo na mlalamikaji. Hapa kuna harufu ya jinai na DCI alipaswa kunusa ili kupata ukweli.

..waandishi wachunguzi hawatakiwi kusubiri hisani ya Chadema bali wanatakiwa wawe pro active kuusaka ukweli toka NEC, Ofisi ya Bunge, na Chadema.

..mpaka sasa hivi hakuna muandishi aliyekwenda kuulizia jambo hili NEC. Hiyo inaonyesha waandishi wetu wamezubaa, au hawako makini ktk majukumu yao.
 
Back
Top Bottom