Uchaguzi 2020 Tulia Ackson, Wana Mbeya tunasema fedha siyo za Rais fedha ni za umma, usitupotoshe

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Dr. Tulia Ackson Ni vyema ukajifunza unapozungumza na Wananchi na ukatambua nafasi ya kazi unayotuomba tukupatie Wana Mbeya.

Kazi ya Mbunge siyo kwenda kuomba fedha kwa Rais, fedha za nchi ni zetu. Kazi ya Mbunge Ni kwenda kusimamia utungwaji wa sheria, usimamizi wa rasilimali zetu zikiwemo fedha pamoja na kushawishi matatizo yetu yapatiwe sluhu.

Ni kosa kubwa sana kwenda kumsikiliza Rais anataka Nini, siku ukienda kinyume naye utasimamiaje haki zetu?

Mbunge apaswi kusimama kwa kumtegemea mtu flani, Mbunge anapaswa kujisimamia. Kwa namna usivyoweza kutofautisha kuwakilisha wananchi na kujinyenyekeza kwa wakubwa wewe siyo mtu sahihi kwetu.

Matatizo ya wananchi yanatatuliwa kwa Kodi zao siyo hisani ya kiongozi, umetukosea sana. Lakini pia kushindwa kujua matatizo yetu kwa miaka mitano kunatosha kusema utofaa kutuongoza.

Kutuletee mchele, cement, arambee, jezi, na fedha kwa wajumbe wakati wa kuelekea uchaguzi ilikuwa Ni rushwa, mbona ukuyafany haya maisha yako yote ukiwa UDSm na hata ukiwa mtumishi wa Umma? Wewe mbeya umeijuia baada ya Ubunge before hata likizo ulikua ukanyagi huku, leo unatulazimisha tumchague mtu aliyekaribu na Rais, je asipotaka kukusikiloza utafanyaje?
 
Huu udaktari wake ni wa aina gani?? Ni Kama ule Uprof wa Maji Marefu??

Kimsingi ametudhihaki Wana Mbeya. Anadhani Hadi leo hatujui majukumu ya Mbunge. Kwa mfano tukampa Kura akashinda Ubunge halafu JPM akakosa Urais, Rais akawa TL je atajiuzuru ubunge???

Hoja za kipumbavu km hizi hazipaswi kutumiwa na mtu wa hadhi yake. Uchu wa Madaraka unamfanya ajifedheheshe yeye na taaluma yake. Kwa hoja hii hapaswi kabisa kupewa hata Kura moja Mana inaonesha wazi Hadi sasa hajafahamu majukumu ya kazi anayoiomba. Ni aibu sana kwa mwanasheria wa level yake kutoa hoja ya kitoto km hii.
 
Back
Top Bottom