G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,595
- 36,017
Huyu mama siwezi kumuita "Daktari wa falsafa" maana hastahili! Kwenye zama hizi tunashuhudia kiongozi mbaya kabisa kuongoza mhimili wenye uwajibikaji wa moja kwa moja kwa wananchi.
Huyu ni Tulia Ackson naibu spika wa bunge ambaye anasemwa kuwa ni mtaalamu wa sheria! Sheria ipi? Amejivua nidhamu ya taaluma na kuwadhihaki kwa kiwango kikubwa wana taaluma. Sina wa kumlinganisha naye ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwani ndiye mbovu kuliko wote!
Huwezi kwenye zama hizi kuongoza mhimili kama bunge halafu ukaishia kutoa maamuzi na kuongoza hovyo hovyo kisha ukajiona uko timamu na unastahili bila ya kuwa na nguvu nyuma yako! Nguvu inayokupotosha tena kwa kiwango kikubwa kabisa.
Nani kasema kuwa bunge linaweza KUWEKWA kwenye kiganja kimoja cha mtu tena kwenye zama hizi? Ni kwanini iwe Tanzania? Ni kwa sababu bunge limekabidhiwa viongozi wabovu sana na wasiojisimamia kama Tulia Ackson (mama aliye mfano mbaya wa malezi )
Amekuwa akisimamia maamuzi ya hovyohovyo kisheria mbali na yeye kuwa mwanasheria! Mwanasheria? Mbona anazidiwa mbali sana na spika aliyepita bi Anna Makinda mbali na kuwa hakuwa mwanasheria? Bi Anna Makinda aliwatumia wana sheria kama Tundu Lissu na Mkosamali kujimarisha na akajijengea heshima kupitia wao! Yeye anawaona sii lolote na kutoa maamuzi ya ajabu kuwasimamisha mwaka mmoja wabunge wanaowakilisha wananchi.
Sasa ni heri mwana mama Tulia Ackson akajirudi na kuwaza upya, je yuko sahihi? Kwanini yeye tu? Bunge chini yake limefanywa kuwa chombo cha hovyo kisicho na maamuzi na kilichopoteza matumaini kwa wananchi! Yote haya yanasababishwa na mtu mmoja, Tulia Ackson Mwansau kiongozi asiye jitambua!