Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Tuambie, unaelewa nini ukisikia Siku ya Mtoto wa Afrika? Kipi kinagusa katika kumbukumbu hii? Nini unafanya ili kuienzi siku hii? Je, unafahamu kwamba hata wewe ni Mtoto wa Afrika?
Sasa taarifa ikufikie kuwa, ifikapo Juni 16 mwaka huu tutakuwa pamoja na Timu ya Jamii Media (JamiiForums) kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Park (JMK Park) jijini Dar es salaam.
Ndugu MwanaJF, kama ungepewa nafasi ya kuzungumza chochote, ungesema nini kuhusu siku hii?
Tiririka..
========
IJUE SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA UFUPI:
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kuwaenzi mamia ya watoto walioandamana kudai usawa katika elimu iliyotolewa na serikali ya kibaguzi ya makaburu mnamo mwaka 1976 huko Soweto, Afrika Kusini.
Mamia ya watoto wa kike na wa kiume walipigwa risasi na kupoteza maisha kikatili huku mauaji hayo yakiendelea kwa takribani wiki mbili na kupelekea vifo vya zaidi ya mamia huku maelfu wakijeruhiwa.
Siku ya Mtoto wa Afrika ilitangazwa kuwa siku rasmi na Jumuiya ya Umoja wa Afrika mwaka 1991 na husheherekewa Juni 16 kila mwaka kuwakumbuka watoto hawa na kutambua thamani, utu, na umuhimu wa Mtoto wa Afrika.
Mwaka huu, shirika la C-Sema na Jamii Media wataungana na wadau mbalimbali kuiadhimisha siku hii muhimu katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park (JMK Park), Dar es salaam. Sherehe hizi zinalenga kuwaleta pamoja watoto takribani 500 kwa ajili ya michezo na mashindano mbalimbali.
Siku hii itakuwa ni ya kipekee maana watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo, kujifunza na kufurahia huku wakijifunza kuthamini mchango wao katika kujenga Taifa.