Tukutane hapa wapenda music wenye asili ya Congo | Page 14 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukutane hapa wapenda music wenye asili ya Congo

Discussion in 'Entertainment' started by Adolph hitler jr, Dec 22, 2016.

 1. Adolph hitler jr

  Adolph hitler jr JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2016
  Joined: Nov 5, 2016
  Messages: 1,794
  Likes Received: 1,543
  Trophy Points: 280
  Ni muda mwingine tena tukutane hapa wale wapenda Muziki (Music) wenye asili ya Ki-kongo unaojumuisha:-
  1:- Bolingo.
  2:- Zouk.
  3:- Sukuos.
  4:- Kiringala.
  5:- Kikasai.
  6:- n.k
  Kwa malengo ya kupeana taarifa na burudani mbalimbali kuhusiana na Music huu kama vile :-
  - Taarifa za wasanii mbalimbali wanaoimba aina hii ya Muziki..
  - Kubadilishana Videos,Audio na Image za miziki mbalimbali...
  - Kutaarifiana kuhusu wana-mziki wapya na wa kale...
  - Kupeana tafsiri Congo to Swahili..
  - N.k
  NOTE
  - Lugha yeyote inaruhusiwa ikiwemo Kikongo,Kifaransa na Kiswahili..
  - Music wa kizazi chochote tajwa hapo juu ruksa kuzungumzia na kuweka Video, Audio au picture yake. ..

  KARIBUNI SANA (WELCOME).
   
 2. Masiya

  Masiya JF-Expert Member

  #261
  Jan 2, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 3,691
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Kuna jina limetajwa mara moja au mbili kwenye michango iliyotangulia. Mimi nasema hawavumi lakini wapo. Simaro Masiya Lutumba hii ni ngome ya TP OK Jazz (1961-1993) na Bana OK (1994 hadi leo). Virtuoso wa rythm guitar-Micra Jazz 1958, Congo Jazz 1959-60 kabla ya kualikwa na Franco 1961 kumreplace Bholen alyekwenda Negro Success (1961). Huenda akawa mtunzi bora wa nyimbo aliyewahi kutokea DRC (Mabele, Ebale ya Zaire, Mbongo, Maya, nk) ameimbisha waimbaji wengi wakuu wa DRC-karibu wote wa OK Jazz, Papa Wemba, Pepe Kale, Koffi Olomide, Mbilia Bell, Fere Gola etc). Kwa wapenzi wa OK Jazz Luambo (Franco) na Lutumba (Simaro) ni kama pande mbili za shillingi (baada ya kuondoka kwa Vicky Longomba around 1970 aliyeanzisha Lovy du Zaire). Simaro ni poet na philosopher. Ni Mzee ameshapiga miaka 78- na kila mwaka kwa miaka isiyopungua 5 sasa ikifika mwezi March hufanyiwa Birthday Party-na nyimbo zake hutawala akipiga yeye au nguli wengine wakishiriki. Familia ya Luambo ilipomsimamisha kuwa President wa OK Jazz (1993/94)-ndio ulikuwa mwisho wa TP OK Jazz ile tunayoifahamu kwani wanamuziki karibu wote waliondoka na Papa Lutumba na kuanzisha Bana OK (Madilu alikwenda solo).
   
 3. JipuKubwa

  JipuKubwa JF-Expert Member

  #262
  Jan 2, 2017
  Joined: Jun 1, 2013
  Messages: 1,856
  Likes Received: 1,316
  Trophy Points: 280
  Nipo ofisini kwangu hapa mwanzo mwisho nakula bolingo tu.
   
 4. Roga Roga

  Roga Roga JF-Expert Member

  #263
  Jan 4, 2017
  Joined: Dec 20, 2013
  Messages: 388
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kuvutwa huku............akiwa WMMM au akiwa solo?
   
 5. m

  mtoto wa mjin JF-Expert Member

  #264
  Jan 4, 2017
  Joined: Oct 15, 2016
  Messages: 417
  Likes Received: 367
  Trophy Points: 80
  Wakuu mwenye audio ya probleme sur probleme ya extra musica aiweke...yaan hawa jamaa hawatopiga rumbha kali kama hii...labda kidogoo panique tottalle
   
 6. Roga Roga

  Roga Roga JF-Expert Member

  #265
  Jan 4, 2017
  Joined: Dec 20, 2013
  Messages: 388
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  composer roga roga ni shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiida
   
 7. h

  ho chi minh JF-Expert Member

  #266
  Jan 5, 2017
  Joined: Sep 27, 2016
  Messages: 16,403
  Likes Received: 91,680
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kupenda bongo fleva hata siku moja,
  Sijajua ni umri ama kitu gani.
  Kuna watu kama Soki Vangu hazungumzwi,
  Michelino mavatiku Vusi ni hatari kwenye solo,
  Lengi Lenga, Dindo Yogo, Djo Mpoy, Carlito Lassa, Josk Kiambukuta, Yollou Mabiala, Ya Ntesa Dalients, Mangwana na wengineo wengi tu.
  Orch Kiam, Viva makale, Zaiko langalanga, Orch Veve, Wana sosoliso, Tp ok jazz, African sukisa, mangelepa, shamashama, afrisa international, Sokous stars, soukous master, empire Bakuba, Wenge musica bcbg, extra musica, Loketo, Matchatcha!
  Jamaa wameanzia mbali sana, wana ushindani wa kweli, wanaipenda kazi yao,
  Jamaa waliburudisha, wanaburudisha na wataburudisha.
   
 8. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #267
  Jan 6, 2017
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  Super Mazembe, Lipua Lipua
   
 9. homboyz

  homboyz Senior Member

  #268
  Jan 6, 2017
  Joined: Oct 19, 2016
  Messages: 114
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  YouTube
   
 10. milangomitatu

  milangomitatu JF-Expert Member

  #269
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 30, 2016
  Messages: 374
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 60
  Jamaa upo vizuri Big up
   
 11. milangomitatu

  milangomitatu JF-Expert Member

  #270
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 30, 2016
  Messages: 374
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 60
  Napenda Sana kizazi cha 3 ila cha 5 ndo cha mwisho katika vizazi vyote ulivyotaja katika muziki mzuri
   
 12. M

  MPUNGA JF-Expert Member

  #271
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 802
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Sikiliza shughuli nzito ya Nguli the Best ATALAKU the BEST ANIMATOR kwetu huku tunasemaga Rapper au M-ghani jina lake ROBERTO WUNDA EKOKOTA bahati mbaya sana ilibidi asitishe CAREER yake ya muziki baada ya kufanyiwa operesheni ya koo.

  Alikuwa ni MBISHI ananata na BITI balaaa. Msikilize hapa jinsi alivyokuwa anakomaa na Gitaa la Solo la Prince Makaba. Tuianze weekend na kibao hichi murua cha DJINO chao WENGE MUSICA maana hapa ilikuwa ni DREAM TEAM haijawahi kutokea na haitakuja kutokea ndani ya CONGO DRC na Ukanda huu wa Maziwa Makuu humu ndani vilikuwa vimesimama vichwa haswaaa Kuanzia JB MPIANA MUKULU SOUVERAIN PREMIER PAPA NA CHERRY PAPA DAIDA MZEE WA WENGE BCBG SIKU HIZI; NGIAMA MAKANDA WERRASON LE ROI DE LA FORRET PAPA NA EXAUCEE IGWEEEEE! MZEE WA WENGE MUSICA MAISON MERE SIKU HIZI; PRINCE ALLAIN MAKABA (SOLO); BLAISE BULA ENGINEER WENYEWE WAFARANSA WANASEMA INGENIEUR; DIDIER MASELA (BASS GUITAR);ADOLPHE DOMINGUEZ MZEE WA WENGE TONYA TONYA SIKU HIZI.

   
 13. Masiya

  Masiya JF-Expert Member

  #272
  Jan 6, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 3,691
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Hapo penye nyekundu. Mkuu ilikuwa ni timu nzuri na bora lakini kusema haijawahi na wala haitatokea naamini hayo ni mahaba. Mimi nikiangalia kutoka generation ya kwanza hadi hii ya tano (kiuhalisia hawa ni extension ya generation ya 4) sifa ya bendi bora naipa TP OK Jazz ambayo ilisheheni the best of the best katika kila idara (haya ndio mahaba yangu). Wenge Musica 4X4 nawakubali sana lakini TP OK Jazz ni habari tofauti kabisa.
   
 14. h

  ho chi minh JF-Expert Member

  #273
  Jan 6, 2017
  Joined: Sep 27, 2016
  Messages: 16,403
  Likes Received: 91,680
  Trophy Points: 280
  Umesema kweli kabisa!
  Upande wangu pia Tp ok jazz haitatokea tena!
  Ilikuwa na vichwa vikali tupu,
  Naamini ilikuwa ni bendi bora ya karne iliyopita ktk Afrika.

  Congo wana hazina na historia iliyotukuka ktk mziki.
  Kwa sasa nadhani bendi kongwe ni zaiko langalanga.
   
 15. Blaque

  Blaque Senior Member

  #274
  Jan 6, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mwenye historia ya huyu mtu tafadhari
   

  Attached Files:

 16. M

  MPUNGA JF-Expert Member

  #275
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 802
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Yap kabisa nakubali TP OK JAZZ ilikuwa imekamilika na bora kila idara kwa wakati wake. Lakini kuna tofauti kidogo na Wenge Musica. Maana TP OK Jazz iliichukua muda na ilikuwa ikisajili wale bora kabisa muda baada ya muda. Lakini Wenge Musica ilikuwa kama "EVOLUTION" vijana wapya kabisaa wachanga na wasomi wa ngazi ya Chuo Kikuu wakiwa kabendi kao cha burudani wakati wa likizo wanapewa ushauri wanapewa moyo wanaambiwa acheni ndoto za kazi za kuajiriwa ifanyeni hii Wenge Musica ndiyo awe mwajiri wenu wanahamasika na wanakubali.
  Wanaishtua CONGO na DUNIA na kibao MULOLO wanakuja na generique mpya ya muziki unaochezeka siyo wa mchakamchaka kama Soukouss na pale mbele wanashambulia Jukwaa vijana wa Kiume Tu.Hama kwa hakika walikuwa ni wapya kila kitu kipya walikuwa kama wanatokea sayari nyingine. Huo ndiyo utofauti na upekee unaowatenganisha na wengine.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #276
  Jan 6, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Lassie passer
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #277
  Jan 6, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Pipina ya Jean bendeli mpiana.
   
 19. Masiya

  Masiya JF-Expert Member

  #278
  Jan 6, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 3,691
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwako OK Jazz ndiyo ime Evolve na Wenge ni Revolution. Walikuja na mapigo tofauti kabisa na ndiyo maana wao ndio waanzilishi ya generation ya 4. Lakini kama wewe ni wazamani OK Jazz iliingia ulingoni 1956-vijana 6 na Franco akiwa about 18 nao magoma yao yalibadilisha mziki wa kongo ingawa wote walikuwa wanamuziki wa Studio Loningisa ya Mgriki Papa Demitrou. Mwanamuziki aliyeanzia kujifunza band music ndani ya OK Jazz nafikiri ni Prince Youlou Mabiala pekee 1964 au 66 (aliletwa kwa sauti yake). Wengine nafikiri wote waliobaki wameingia OK Jazz wakiwa wanamuziki wa muda. Nikitaka kusikiliza mziki wa vijana basi natua the wenge clan na nikitaka kusikiliza mziki uliotukuka basi nawasilikiza TP OK Jazz (Bana OK) clan.
   
 20. n

  ngajone JF-Expert Member

  #279
  Jan 6, 2017
  Joined: Jan 9, 2015
  Messages: 508
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 60
  Me mkuu bado nina ukakasi wa kujua mwanamuziki GATHO kama alikufa au alifungwa maana kipindi kile taarifa zilikuwa zinakanganya sana mala wengine waseme alikufa mara wengine waseme alifungwa kwa ukweli natamani kujua GATHO alipoteaje kwenye Muziki ghafla
   
 21. Vitaimana

  Vitaimana JF-Expert Member

  #280
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 2, 2013
  Messages: 3,560
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Umeisahau Beya
   
Loading...