Tukutane hapa wapenda music wenye asili ya Congo

Haya sasa. Nani mkali?





Nairobi Makuti.... hahahahaa nice one.

Huyu mtu wa kuitwa emile lemingongo jamaa yupo vizuri msikilize vizuri penye jojo ngonda anavyo lala mika
Yo lingi ngana lela
Maloko mimi
Tabu fatu nisembu
Lisibaba naleliyo kam swahili
Juu ya mapendo lavis na cchiluba
Kulwa Kulwa shekyala na lingala
Nakolela labifu mozonga
Okwaa mimi mamaa
kisha anaingia blaise bula na kufanya yake hakika ule mchanyato sijui kama utakuja kutokea tena
 
Kaka unaufahamu vzr muziki wa Zaire kizazi kwa kizazi nimependa ,mm huwa naifagilia sauti ya papa wemba kwa kweli hakuna wa kumlinganisha,pia nilipendaga uchangamfu wa nouvelle generation wana zimpompapompa halafu huwa najiuliza mpk leo yule rapper wa Blaise Bula alikuwa mtoto maana ile sauti!
Ha ha ha ha. Yule dogo alikua anajua sana, kama kuna watu wana taarifa zake watujuze yuko bendi gani au aliacha muziki? Alikua mzuri na atalaku zake, wimbo ukiitwa Ponderation wa Blaise Bulla
 
Mtu ambaye amesaidia sana mziki wa Congo kuwa maarufu Ufaransa na hadi nje yake hasa kwa wanamuziki wa Wenge na Papa Wemba ni huyu Mere Malu. Walimwita kama ni Meya ya Paris.

Mama alikuwa Bonge la Mafia. Mali za wizi na halali alificha kwake. Wanamuziki wakifika hawana chakula basi walikula kwake ila kulala kwako. Ukishajulikana hakukuachia. Papa Wemba na Wenga walibaki waaminifu kwake hadi alipofariki na wakamlilia sana wote lwa pamoja.

Tufanyie ihsani pana kibao kaimba boziana kinaitwa mubali ya mere malou a zalaki na biso nabiso kipo youtube kama hutajali tuwekee hapa tuburudike mimi sina utaalamu wa kuhamisha
 
View attachment 451908

Huyo mtoto aliyebebwa ndio Diam, na huyo mwanamke kama wa kitusi ndio Amida Shatur, Papa Mukulu JB Mpiana alikubali matokeo
Na huyo msichana mkubwa ndio Dayida, binti mkubwa wa JB Mpiana, nae pia kamwimba sana
Yeah, Amida eee mama ya Dayida utasikia kwenye wimbo 48Heures Gecoco lakini Feux de La Amour(zingatia spelling mistakes na symbol za kifaransa),humo kote anawaimba Amida na Dayida. Ila nasikia huyo Dayida anapenda makuu jijin Kinshasa. JB Mpiana ameonyesha roho ngumu sana hasa inapokuja Kinuani kumfanyia mambo ya ovyo kiasi kile. Anyway ndo kupenda huko.
 
Dah, kaka unanikumbusha vitu adimu, baadhi ya mashairi ni haya

Amour eloko oyo esalema pona banso: mapenzi ni kitu kilichoumbwa kwa ajili ya wote
Eclaquer nga porte na zolo mawa nanga : leo hii pemdo lanifungia mlango usoni masikini mie
Natikali isolee na couloir ya deception : Najikuta nikiwa mpweke nikijazwa na majonzi, simanzi namasikiyiko
Bolingo eboyi kosekisa nga: pendo lanikosesha raha na tabasamu

Mawa efandeli nga na matama: huzuni yajichora shavuni mwangu
Efungoli robinet ya Pinzoli: na kufungua bomba la machozi
Soki ezalaki mayi ya REGIDESO: ingekuwa "Machozi yangu" ni maji ya REDIDESO
Mbele baye kolongola compteur: Basi Bomba lingeshafungwa kwa wingi wa maji ,yaliyoririrka
Bolingo po' nini yo okomi moselu na maboko manga lokolaaaa ngolooo?: Pendo kwa nini wateleza mikononi mwangu kama samaki
Mkuu kama unaweza kutiririka hivi na tafsiri basi kwa nini usitupe tafsiri ya wimbo Omba-Titanic Album, Jeanette-Internet Album au hata Serge Palm?

Hivi kwenye wimbo uliotungwa na Fi Care Mwamba uitwao Le Spoir de Chicago Album Dance de Internet, yule jamaa aliyeimba ubeti wa kwanza kavaa kama Yasser Arafat anaitwa nani? Ubeti wa pili kaimba Fi Care mwenyewe na sauti nzitoooo, kuna lile Bonge katoboa masikio kaimba ubeti wa tatu nae sijui anaitwa nani. Lakini ubeti wa nne kaimba Chai Ngenge. Sijajua huu wimbo wa Fi Care unazungumzia nini kuhusu Chicago japo nasikia Fi Care akimtaja Fidel Castro kwa mbali.

Lakini pia wimbo Tour Eiffel ambao ni mnara pale jijini Paris, sijui una maudhui gani japo kwa mbali namsikia Alain Mpela-Afande akilitaja nchi ya Ufaransa-France.

Namalizia kuuliza ule wimbo wa Bye Bye Julie, namsikia mzee mzima wa Tshituka akimtaja mzee Nelson Mandela(R.I.P)! sijajua maudhui yake ni nini! Anaefaham hayo mambo niliyoyagusia japo kwa uchache atujazie maujuzi na maarifa.
 
Aliweka wazi japo watu wanasema mjini hawahami nadhani kibao kiliitwa RDC
Hapana, huo wimbo unaitwa KINSHANSA, umo kwenye Disc 2 kama sikosei ya Album ya Toujours Humble. Na ukiangalia video unaona watu wa mjini akimaanisha Jiji la Kinshansa wanavyopigana kutafuta maisha, mara wapake rangi majengo yaaani maisha ya 'DEI waka'ili siku ziende, na hapo ndipo anaposhauri watu 'Warudi kumashamba' wakalime kama maisha yenyewe mjini yako tight.
 
Wanamuziki maalufu wa kikongo:-
Men
-Werrason. -Koffi olomide (Mopao). -Pepe kalle. -Franco Lwambo Makiadi -Fally ipupa.-Kanda Bongoman, -Ferre Gola. -Wazekwa.- Awilo Longomba - Papa Wemba. -Madilu System. -Tabu ley. -Defao, -J.B Mpiana,-Aurlus Mabele,-Joseph kabaselle,-Mbuta likasu, -Ghatto, -Lucian Bokilo,-Bozi boziana,-Victoria elyson ...
Women
- Mbilia bel -Cindy lecour,-Fayatessy -Yondo sister -Tshala muana,-Scola,-Betty .....
Groups (Makundi)..Band
-T.P OK JAZZ ,-Empire Bakuba, -Quartier Latin International,-Wenge Musica ,B.C.B.G -Soukous stars,-Extra Musica,-G7 Ca va ler,-Loketo...
UMESAHAU VIJANA WA ZAMANI: ZAIKO LANGA LANGA ,: JOSE NYOKA LONGO
 
Hapana, huo wimbo unaitwa KINSHANSA, umo kwenye Disc 2 kama sikosei ya Album ya Toujours Humble. Na ukiangalia video unaona watu wa mjini akimaanisha Jiji la Kinshansa wanavyopigana kutafuta maisha, mara wapake rangi majengo yaaani maisha ya 'DEI waka'ili siku ziende, na hapo ndipo anaposhauri watu 'Warudi kumashamba' wakalime kama maisha yenyewe mjini yako tight.
Safi kabisa ni Kinshasa penye wengi jambo kamwe haliwezi kuharibika
 
Nasilikiza wimbo wa Koffi Olomide uitwao Mduara-Rond Point(Round Point)

Naona ubeti wa kwanza aliyeimba sauti yake kama SUZUKI 4x4, Ubeti wa Pili simjui aliyeimba, ubeti wa tatu sauti iko kama ya Fally Ipupa japo ni zaman kidogo huu wimbo sijui kama Fally Ipupa alikuwepo, ubeti wa nne sijui nani kaimba, ubeti wa tano Koffi anamtaja Serge Kasanda. Huu wimbo Round Point, Julie,Affaire de Etat, Riziki, Moprate Landile, Attentant,kwangu naona Koffi alitutendea haki sana.
 
Kuna "masuwa"
Mkuu [HASHTAG]#Mbulu[/HASHTAG] hii kitu nimeiona first time ndo video zimeanza tz kwenye mabasi.

Nakumbuka nilipanda basi la superstar pale stand ya kisutu naenda moshi...ikawekwa mkanda wa kideo...kitu cha Masua teroriste.
.balaa sana!
 
Back
Top Bottom