Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Mwaka 2007 asubuhi tukiwa kwenye daladala kufika buguruni mama mmoja kabaini simu yake imechomolewa na kibaka na anauhakika kibaka hajashuka akauwasha moto kuwa aliyeiba simu hajashuka akamwambia dereva tafadhali twende polisi akajitokeza Kaka mmoja akamwambia yule mama simu yako ni Aina gani na ni Sh.ngapi mama kajibu Nokia elfu sabini

Kaka akazama mfukoni akatoa laki moja tusiende polisi maana anaharaka saa hiyo tumekaribia mataa Buguruni gari ya Gongolamboto hiyo.

Mama kajibu sitaki laki line yangu instead majina ya wateja wangu wa samaki sitaki laki yako nataka simu yanguu twende polisi

Huyo aliyekua anataka kutoa laki alikua siti ya mbele karibu na dereva, basi Hari ziliporuhusiwa alitoa bastola akamuelekezea dereva akamwambia hatuendi polisi endesha gari kuelekea tazara bwana red Kumbe hakuwa peke yake huku kwenye siti niliyokaa Mimi Kumbe nimekaa na mwenzie naye akatoa bastola akaiinua juu akiamuru tutulie

Ulimi Wang ulikua wa moto mdomoni mpaka ninaufeel nilitetemeka Sana dereva alinyoosha mpaka Around uwanja wa taifa wakashuka jamaa wanne na Makoti makubwa wakaenda zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
huyo aliibiwa na kibaka ila hiyo mijambazi iliona tukifika polisi wata search kila mtu alafu watagundulika.
 
Hii sasa nilisimuliwa tu hivyo sijui kama ni chai ama kweli.
Kuna siku majambazi walivamia nyumba yenye familia, walipofika wakaamuru watu wote walale chini kifudi fudi, baada ya raia kulala wote jamaa wakakomba kila kitu chepesi kubebeka kisha mmoja wao akawasha redio kaseti iliyokuwemo humo ndani halafu akaweka tape/kanda-(samahani watoto wa 2000) waliojirekodi wakipiga mikwara ya kufa mtu humo ndani akaplay kisha wakasepa, sasa familia kutoka saa tisa usiku wakawa wanaamrishwa na redio mpaka asubuhi wakawa bado wamelala kifudi fudi na majambazi kitaaambo yameshaondoka


Sent from my iPhone using JamiiForums
alafu ukute ni auto reverse
 
mie mwaka 2009 mwaka mpya walikuja njemba zaidi ya 10,nakumbuka mzee ndo siku alikuwa ameuza spacio yake kwa milioni 9 hata bank alikuwa hajaipeleka wakavunja mlango but kabla walipiga risasi moja juu mi nlivyoskia tu fasta nkapanda juu ya dari nlipanda vipi mpka leo sikumbuki basi wakafanya yao mzee alikuwa analia kama mtoto,asubuhi akaitwa mpemba akafanya dua yake bhana dah wapemba siyo watu wazuri maana baada ya dua tu jirani zetu zaidi ya wa 3 waliondoka siku ile ile mpka jioni vitu vyote vilirudi na faini juu
heahima kwenu wapemba


Sent from my iPhone using JamiiForums

Asante sana
 
Mwaka fulani nimetoka Mbeya na Mr saa saba za usiku, Kufika maeneo fulani karibu na Morogoro kuna kona fulani hivi ya kishkaji, sijui Mr alikua na nini kichwani hakuangalia mita kadhaa mbele, mi nimelala zangu nakula usingizi kwa raha zangu, ghafla nikahisi kama gari imepaki ghafla, nikasikia ananiambia amka amka!

Kufungua macho naona malori mawili yamepaki pembeni ya njia mbele ya malori kuna gari dogo nayo imepaki halafu kuna bongee la gogo katikati ya barabarani Mr akanambia kuna tukio la utekaji hapa either linaendelea ama kimeisha muda si mrefu, Salaleee usingizi ulinitoka wote, nikakwambia Mr turudi tulikotoka akanambia No, kwenye matukio kama Haya huwa haturudi nyuma.

Nilipaniki nusu nimnase kibao nikamwambia sasa tusirudi nyuma tubaki hapa watushike na sisi? Akasema anavyoona yeye lile tukio limeshaisha na wenye magari haya either wamepaniki wamekimbilia vichakani ama watekaji wamewachukua wameondoka nao. Nililoa jasho hadi pichu, mi kwa akili yangu nilikua nafikiri wamewakusanya wenye magari wako nao mahala wanatuangalia na watajitokeza sio muda kutuchua na sisi Ndio maana nilikua namsisitiza Mr turudi tulikotoka ye anamsisitiza hakuna kurudi.

Akanambia ye anashuka ajaribu kutoa gogo tupate pakupenya, hivyo mimi nishike wheel ikitokea wakajitokeza wakamkamata mi nirudishe gari reverse vyovyote vile bora nipate ajali ila wasinikamate nikiwa mzima anasisitiza maana wanaweza kunibaka. Haya mabishano yote yalifanyika kwa dakika kadhaa, mwisho kishingo upande nikamkubalia ashuke. Akashuka nikakamata usukani, nikafunga belt nikajiandaa huku natetemeka hakuna mfano.

Ile ameshuka tu akakamata gogo naona ni zitooo hata haliwezi akatokea kijana porini amepigwa vibaya sana kumbe alikua mmoja wa madereva waliotekwa, kidogo wengine wakajitokeza wakawa wanaelezana kilichotokea, mwisho wakakubaliana watembee kwa kuongozana hadi wakutane na Barrie ya mapolisi watoe taarifa. Wale madereva na makonda wao walikuwa wamepigwa sana wanavuja tu damu, nakumbuka mmoja sikio la kulia lilikua limelegea kama linataka kudondoka na kwa wakati huo niliona kama hasens chochote zaidi ya kuona tu midamu inamvuja. Basi ndo hivyo tukaondoka kwa kuongozana tulifika Barrie ya polisi karibu kabisa na Moro tukawaacha sie tukasepa zetu, tumbo liliniuma siku hiyo sitasahau sijui ni sababu ya uoga.
We kweli una mume bana
 
Mwaka fulani nakumbuka majambazi yalifunga mtaa wetu tulipokuwa tunaishi!.. Jamaa walivamia nyumba ya jirani kwanza walipiga risasi kama 2 angani na 1 wakaua mbwa then wakaingia ndani ya nyumba.
Walimchukua mzee mwenye nyumba na familia yake wakawafungia chumba kimoja then wakaanza hamisha samani za sebureni kama zao, nje wamepaki canter kabisa hapo mvua inapiga balaa.
Kuna mjeshi flani alitoka ulevini sasa njia ya kuelekea kwake lile canter likawa limeziba, akawa anapiga horn walitoe, akapiga moja angani alipoona wasumbufu. majamaa ndio kukimbia, yakaacha canter lao!.
Sasa yule mjeshi akaenda gonga kwa yule mzee anatukana kinoma inakuaje wanahama usiku, ndio wenye kujiweza tukaanza toka!.Kumbe mtaa mzima ulikuwa macho upo kimyaa unaangalia sinema!.
Kesho yake ikawa story ya mtaa ulevi wa mjeshi ulivyookoa mtu kugeuka masikini!. Sidhani kama ile familia watamsahau yule mzee mjeshi!.. Watu tukawa tunajiuliza wale jamaa wangeact kulitoa lori lao njiani yule mjeshi angekuwa mjinga wa mtaa.
ha ha ha
 
Baada ya kushonwa,,,,,
20211011_172328.jpg
 
Hawa mbwiga walivamia mbagala rangi tatu kwa Jirani yetu, baada ya kumaliza uharifu wao wakaenda jikoni Na kuchukua msosi Na kuanza kula sebuleni kama kwao vile, mwisho wakanya kwenye makochi Na kuondoka, yaani hawa watu ni laana tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huko USA mwizi aliiba supermarket na akanya halafu hakuflash mavi yake.FBI wakaenda wakapima DNA kwenye havo mavi na jamaa akadakwa kilaini tu.

 
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu, binafsi nimewahi kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya Sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, sikusita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

Unaweza kushare mawili matatu kama umewahi kukumbwa na maswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.

Pia soma Fanya yafuatayo ukigundua kuna majambazi nje ya Nyumba yako
Dah punguza kutembea usiku kwa miguu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom