Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Kuna vibaka walikuwa wanasumbua sana mtaani. Hasa nyumba niliyokuwa nimepanga. Tulikuwa kama wapangaji 7 ukiachia mbali kijana wa mwenye nyumba. Mwenye nyumba alikuwa haishi hapo ila kijana wake tu

Sasa siku ya siku saa tatu usiku tumefunga geti dogo nje akapiga kelele kuashiria kuna kibaka karuka ukuta. Watu fasta wakawahi kwenye sehemu ya kurukia ukuta ili asitoroke. Tuka mweka mtu kati.

Jamaa mpangaji mmoja akaanza kumpiga kichwani mapigo hatari. Nikaogopa anaweza kufa. Halafu ni uani. Kesi ya kuua hiyo. Mtu mwemyewe mdokozi tu kwa jinsi nilivyofikiria. Nikamzuia na bahati nilikuwa nasikilizwa. Niliwaambia hiyo kazi niachiwe mimi.

Nikachukua vyuma Vya kutundikia mashati kama sita hivi halafu nikawasha jiko LA gesi. Nikawa naweka kwenye jiko LA gesi mpaka viwe vyekunduuu. Halaf namtumbukizia ndani ya jeans yake au ndani ya shati lake. Haloooo

Si kuruka na Makelele hayo. Harufu ya nyama kuungua ikasambaa kama tunachoma nini sijui.

Ikabidi aanze kumtaja boyfriend wa mpangaji mwenzetu kwamba wanafahamiana

Yakaanza kama mabishano kati yao. Boyfriend wa mpangaji mwenzetu akidai hamjui kabisa mwanzo. Lakini kibaka anakomaa na kutoa maelezo ya kina kuthibitisha kufahamiana. Dah.

Mimi Niko bize kuweka vyuma kwenye jiko LA gesi na vikiwa vyekundu nambambikia mwilini. Halafu yeye anaropoka kuomba msamaha na kusema ni jamaa yake na huyo jamaa.

Ikabidi T-shirt na jeans avichanechane ikabidi kumwekea vyuma vya moto katikati ya mapaja na kwapani huku akiwa kashikiliwa. Aisee

Walikuwa wawili Mwenzie alitutoroka.

Baada ya hapo hatukusikia tena purukushani za vibaka mtaani
Chaaaaah inahitaji roho ngumu
 
Ilikuwa ni saa kumi na moja jioni tukitoka Dar na malori yetu kama saba hivi kuelekea kigoma kwenye miradi so tulipofika Nyakazi mida hiyo tukaona tupumzike na kula chakula kidogo hapo , muda wa saa noja jioni tukaona huu mida mizuri tuendelee na safari tukalale kibondo
Tulipoanza safari tuu mbele kidogo kuna barrier ya polisi kalenge na baada ya hapo mita chache ni daraja na lami ya kidogo nikakukuta mwenzangu kashapaki kawasha packing light nikajiuliza kulikoni hii break down ya mita chache kumbe wazee wa Urundi washafika bana niliona kwanza mfano ni miti ilivyokuwa inadondosha matawi kwa risasi zilivyokuwa zinarindima
Nikachimbwa bit la kusimama chap nikasimama na kuanza kulala chini ya gari hapo sina tena nguvu
Wenzangu wote walokuja nyuma kila mmoja alipack kwa wakati wake ndipo boss alokuwa na wild load alimiminiwa risasi wala aikujua ni ngapi maana alikuwa kama matundu kila kona ya mwili
Ilipofika saa nne usiku tukaja kuokolewa

Nyingine 2014 nilipanda basi la princess Munaa kutoka dar kwenda mwanza shinyanga tuliingia saa sita kamili
Tukashusha abiria pale na kuendelea na safari ili kesho yake niwaho kwenda kupiga kura ya uchaguzi wa serikali za mitaaa kufika ngungumalwa darajani tukakuta lorry limetekwa likalazimishwa likuche Cabin njiani wakaongeza na jiwe moja
Punde basi likagonga lile jiwe dereva alichezea bapa ss wengine wote tulishuka mle kama wasichana wote kila mmoja chochote ulichonacho uweke kwenye sandarusi iliyokuwepo mlangoni milio ya risasi usiombe nilitamani ardhi ipasuke nijifiche humo ila nikawa nishachelewa sio kwa kipondo tulichokula siku acheni mambo ya kutekwa sikia kwa jirani tuuu
 
Kuna vibaka walikuwa wanasumbua sana mtaani. Hasa nyumba niliyokuwa nimepanga. Tulikuwa kama wapangaji 7 ukiachia mbali kijana wa mwenye nyumba. Mwenye nyumba alikuwa haishi hapo ila kijana wake tu

Sasa siku ya siku saa tatu usiku tumefunga geti dogo nje akapiga kelele kuashiria kuna kibaka karuka ukuta. Watu fasta wakawahi kwenye sehemu ya kurukia ukuta ili asitoroke. Tuka mweka mtu kati.

Jamaa mpangaji mmoja akaanza kumpiga kichwani mapigo hatari. Nikaogopa anaweza kufa. Halafu ni uani. Kesi ya kuua hiyo. Mtu mwemyewe mdokozi tu kwa jinsi nilivyofikiria. Nikamzuia na bahati nilikuwa nasikilizwa. Niliwaambia hiyo kazi niachiwe mimi.

Nikachukua vyuma Vya kutundikia mashati kama sita hivi halafu nikawasha jiko LA gesi. Nikawa naweka kwenye jiko LA gesi mpaka viwe vyekunduuu. Halaf namtumbukizia ndani ya jeans yake au ndani ya shati lake. Haloooo

Si kuruka na Makelele hayo. Harufu ya nyama kuungua ikasambaa kama tunachoma nini sijui.

Ikabidi aanze kumtaja boyfriend wa mpangaji mwenzetu kwamba wanafahamiana

Yakaanza kama mabishano kati yao. Boyfriend wa mpangaji mwenzetu akidai hamjui kabisa mwanzo. Lakini kibaka anakomaa na kutoa maelezo ya kina kuthibitisha kufahamiana. Dah.

Mimi Niko bize kuweka vyuma kwenye jiko LA gesi na vikiwa vyekundu nambambikia mwilini. Halafu yeye anaropoka kuomba msamaha na kusema ni jamaa yake na huyo jamaa.

Ikabidi T-shirt na jeans avichanechane ikabidi kumwekea vyuma vya moto katikati ya mapaja na kwapani huku akiwa kashikiliwa. Aisee

Walikuwa wawili Mwenzie alitutoroka.

Baada ya hapo hatukusikia tena purukushani za vibaka mtaani
Binadamu washenzi sana

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Me nilikutana nao mwaka jana. lakin hao tuseme ni vibaka wako na bodaboda. ilikua arusha njiro natoka kwenye sherehe kwenye kotaz za fidforce njiro .basi nikatembea mpama barabara kuu .ikapita boda nikasimamisha . nikapanda jamaa akaenda simama sehemu.kumbe kuna wenzie wawili .duuu wazee sjui nilipata wapi ujasiri yaani kama movies nilishuka .kwenye pikpk mazima nikamvaa mwenye sime wengine hawakua na siraha .nilishika ile sime kwenye makali uku wengine wakinipiga ngumi za uso .sikuhachia sime mpaka nilipofanikiwa kuwanyanganya .baada ya kuona nmechukua sime wale jamaa wanakimbia kuwasha toyo haiwak lkn na mimi hapo sina nguvu tena . najaribu kuwafata nashindwa . baada ya hapo natembea kuomba msaada watu wananikimbia maana niko na panga ina damu nyingi na mimi mikono inamwagika damu .mpaka leo vidole vi wili havifanyi kazi.
staki kumbuka iyo siku
Pole sana
 
Aise hizo kota kwenye iyo mitaa ni balaa ..mimi nishataitishamwaga pale nilikuwa na tabia za kutoka chuo saa sita/saba usiku pale IAA uhasibu ..basi bana wahuni haoo wakantaitisha bahati nzuri wawili ni machali ambao nawajua..ivo ikawa pona ang apo. Kwanzia sku iyo nikawa napita mida kaa iyo tukikutana nao nawatoa za fegi wanantema..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
sitasahau aise,paa paaa paaaa,zliikuwa ni smg/shortgun zinakoroma,siku hiyo nyumba ilizingilwa na majambazi wakiwa na smg,na shortgun.nilijificha lakini jamaa walifanikiwa kunidaka,wakawa wanataka niwaonyesha mpunga ulipo.2006 hiyo maeneo ya pugu dar,tukiwa tunafanya biashara ya ng'ombe tunazitoa mikoani na kuuza soko la ng'ombe pale pugu.jamaa waliondoka na mpunga mlefu sitasahau.kuanzia sku hiyo nikapa sitafanya biashara ya ng'ombe,niliondoka dar na kurudi kutuliza kichwa mkoani.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Kufika camp jamaa angu anakuja...nikamwambia we mrombo walaaaah leo ndo utanijua,nikatoa simee nilikua Ni mchinjee,maana katika ile issue nilikua namuita yeye kanyuti na wale majamaa niliwajua niwale tulio kua nao na nikajua kasuka mchezo yeye,kipindi hiyo tunafata mafta taa na blue band na nafuta ya kashuku kenya
Kuna kifodi kimoja kina hili jina lako Arusha.
 
Ilikua kahama miaka ya 1995 hv, saa kumi alfajiri tunatoka home maeneo ya nyasubi tunaenda stand kupanda bus,wakati huo kuna bus mbili tu za kwenda mwanza lake trans na Chwezi,sasa tunatembea tunaelekea stand ile nyasubi ilikua na miembe mingi saaana mikubwa baba kashika bonge la rungu na tochi pia mabro wawili walikua wanatusindikiza na mbwa pia,tumefika mahali kwenye miembe jamaa zikatokea ziko 4,baba akasema kwa sauti USIKUUU kumbe kama ni mtu wa amani unatakiwa ujibu MCHANA yale majamaa hayakujibu,ghafla mbwa alipgwa bonge la fimbo, jamaa walikua na mapanga pia,sasa sisi tunapiga kelele mshua anakomaa nao,dah waliondoka na mabegi mawili lakin mmoja alipihwa rungu la kichwa akazirai so hiyo ikawa ndo rip yake coz wananzengo walikuja wakapiga wakachoma moto, siai safari ikaishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini wakuu,
Naona uzi umepoa,ngoja namimi niweke kisa changu..

Hii haikunitokea mimi ila ilimtokea mtu aliyekuwa karibu na familia yetu,Namkumbuka kwa jina moja la MACHIWA

HUYU alikuwa ni “Mtumishi” wa serikali..

Kwa walioshi/wanaoifahamu TARIME ya miaka 2000’s ilikuwa hatari sana kwa ujambazi wa kutumia silaha.
To make a story short, kuna GANG moja ya Majambazi ilikuwa identified na marehemu alihusika katika kutoa taarifa na kuzipeleka kwa “wahusika”,Kumbe baadhi ya “wahusika” nao walikuwa wanashirikiana na hilo GANG la majambazi sugu.

KILICHOTOKEA

Baada ya Marehemu kuonekana kuwa ni THREAT kwa hilo GANG,basi walipanga njama za kumpoteza kabisa ili iwe fundisho kwa wengine..ilikuwa usiku mmoja marehemu amejipumzisha na familia yake,alishtukia mlango unavunjwa na wauwaji wakaingia ndani,hawakupora hata sh.100 mbali na kwamba marehemu aliwaomba wachukue chochote wanachoweza ilimradi wasamehe roho yake na ya familia yake,majambazi hawakujali,walimpigisha magoti mbele ya familia yake na kumkatakata mapanga mpk walipohakikisha amefariki then wakaondoka.

Marehemu alifariki kifo cha uchungu na kuacha familia yake na watoto wakiwa wadogo just because he tried to what was right but the system WAS full of ASSHOLES.

R.I.P Mr.Machiwa,Naimani wengi walioishi tarime miaka hiyo wanafahamu hii stori na incase nikiwa nimekosea/nimesahau kitu naomba anayeweza aongezee nyama.

Note;Nyie majambazi mliohusika na alitewatuma(probably mpo humu); MAY YOU ROT IN HELL!!!!
Dahh Kifo cha Udhalili sana..
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Noma sn!
 
Ukiwa umepigwa ambush siku zote cha kwanza angalia nguvu ya adui kama unaweza toboa au vp halafu kitu kingine simple ambacho kinaweza kusaidia....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom