Tukutane hapa tuliowahi kufanya na kufanyiwa matukio ya Kikatili na kutisha maishani

Miaka flan tupo std 5, ni watoro wazoefu. Tumeiba mihogo kwenye shamba la balozi tunaichoma mahali.
Gafla tumekamatwa na mgambo tukapelekwa mpaka ofisi ya ccm pamoja na mihogo na mashina yake kama ushahidi, faza alikuwa mkali balaa ikithibitika ni ukweli tumeiba itakuwa shida sana!

Tuliachiwa na wazazi wakaandikiwa barua za wito.

Nilichekecha kwa dk chache tu, nikaamua kurudi ofisini nyatunyatu na nikaiba ile mihogo pamoja na mashina yake! Kesi ikaisha!

Mpaka leo nikiendaga kule kijijini wazee wakiniona hawanaga ham.

Ktk utoto huohuo tulitengenezaga ndoano tukaitega juu ya daraja na kufanikiwa kuiba kiasi kikubwa cha mizigo iliyo kwenye carier ya bus, na kusababisha vijana wakubwa pale mtaani kukamatwa na polisi bila sisi kuhisiwa chochote"
 
Nipo form si kipindi hiko, nikaenda hospitali kumsalimia classmate (wakike) alikuwa amelazwa hospitali ya mission karibu na shule. Wakati nipo kitandani Dr akaingia na kutufukuza, sikumbuki nilimjibu nini. Kesho jumatatu kengele ya dhalula inagongwa mida ya saa tano wote tukaenda assembling ground. Mara naitwa jina toka mbele na mwalimu mkuu akiwa na discipline master na yule Dr. Akasema ndio huyu aliyekuwa anakula mate na mgonjwa.
Aisee nilichezea bakora hapo, Mimi ndio nikawa mfano wa watu wanaotafutwa wenye mademu shuleni (maskini ya Mungu hata hakuwa demu wangu). Nikaulizwa nichapwe bakora 20 au nipewe suspension? Nikawaza ukali wa mzee, nikakubari bakora. Nilichapwa zaidi ya bakora 20
Yule demu alipokuja kusikia baada ya kupona alimvaa Dr alafu akaenda kusema kwa mwalimu mkuu, kumbe alikuwa anamtaka kitambo tu anamchomolea. Lilikuwa gumzo, Ila wakayamaliza kiutu uzima huku mimi, nilishaumia.
Baadae yule demu akaja kuwa demu wangu kiukweli sasa tukiwa vyuo tofauti. Tulikuwa tukikumbushiana hiyo stori anacheka na kusema sasa tunafanya kweli au walitutabiria 🤔
Now ni friends wa kawaida ameolewa na watoto wawili, we are happy
 
Nipo form si kipindi hiko, nikaenda hospitali kumsalimia classmate (wakike) alikuwa amelazwa hospitali ya mission karibu na shule. Wakati nipo kitandani Dr akaingia na kutufukuza, sikumbuki nilimjibu nini. Kesho jumatatu kengele ya dhalula inagongwa mida ya saa tano wote tukaenda assembling ground. Mara naitwa jina toka mbele na mwalimu mkuu akiwa na discipline master na yule Dr. Akasema ndio huyu aliyekuwa anakula mate na mgonjwa.
Aisee nilichezea bakora hapo, Mimi ndio nikawa mfano wa watu wanaotafutwa wenye mademu shuleni (maskini ya Mungu hata hakuwa demu wangu). Nikaulizwa nichapwe bakora 20 au nipewe suspension? Nikawaza ukali wa mzee, nikakubari bakora. Nilichapwa zaidi ya bakora 20
Yule demu alipokuja kusikia baada ya kupona alimvaa Dr alafu akaenda kusema kwa mwalimu mkuu, kumbe alikuwa anamtaka kitambo tu anamchomolea. Lilikuwa gumzo, Ila wakayamaliza kiutu uzima huku mimi, nilishaumia.
Baadae yule demu akaja kuwa demu wangu kiukweli sasa tukiwa vyuo tofauti. Tulikuwa tukikumbushiana hiyo stori anacheka na kusema sasa tunafanya kweli au walitutabiria
Now ni friends wa kawaida ameolewa na watoto wawili, we are happy
ha ha ha, dahh!!
 
Hizi hekaya unakosea kuziita story za kweli, kama ni stori za kweli za mtu mmoja basi inatakiwa historia yake ya utoto ifanane, mara useme umezaliwa Dar, Uzi mwingine useme ulizaliwa kigoma ukaja Dar, mara useme wazazi walikuwa masikini mara tena baba alitoka UK, Au UK ya Ukerewe?
 
Siku hiyo nilichelewa kurudi nyumbn mida Kam ya tano iv ucku hapo kijijini kulikua na bonge la mti ambao ulikua ktk njia ambayo ni maarufu Sana ila pale wazee wetu walikua wakitukataza Sana kupita hiyo njia ila sababu walikua hasemi ila ni msisitizo Sana hasa nyakati za ucku
Bas bwana siku hiyo nmetoka zangu kwa washkaji kupiga stori kutokan na mda ilishaenda Sana nkaona kuzunguka ni mbali na huku tilishakatazwa kupita ucku hasa ukiwa alone
Nkaona poa mi mwanaume bhana potelea mbali liwalo na liwe nkavua yebo zang nakuzishka mkononi safari ikaanza mwendo Kam wa mchaka mchaka baada ya km nusu km ivi nakaribia jirani na ule mti mara gafla naona macho makali yanang'aa Sana mbali kdg na ule mti nkajikaza na kupita kwa mbali maana nakarbia home siwezi kurudi nlipotoka
Ile namalizia tuu kuyapita gafla hamadi dude hili apa nyuma nilikimbia skuwahi kukimbia vile bahati nafika tuu omu namkuta mdogo wangu anafunga mlango huku Niko speed 260 ile naingia tuu dogo kabamiza mlango pigwa Sana mikucha pale mlangoni tokea siku hiyo saa 12 jiion npo ndani
Mpaka leo sikuwahi na wala hatukuwahi kujua alikua ni mnyama gani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmhhh!!!! Hatari sana
 
Nikiwa nabiri matokeo ya form kitaa siki moja nikaenda ghet kwa washikaji
Nilipokalibia nyumba wanayoishi nikaokita wallet in Kama 40k
Nikaiweka mfukon nilivofka kwa washikaji nikatulia tu sikuambia mtu,
Sku kadhaa mbel nshatumia hela nikakuta washikaji wengin wanamlaumu mweny ghet kawaibia hela na ukawa msala mkubwa Sana. Na ilo ghet alitaka kutimuliwa sabb Kuna tich flan alimsaidia kupanga hapo

Ilibid mm nikae kimya tu maan nikisema niliokota hkun hataye niamini.
 
Tuliogelea na mwana mtoni jamaa akazama tuliamua kukimbia

Nilishuhudia ugomvi utotoni mwenzetu akambonda na jiwe kichwani mwenzie damu ziliruka kama kuku aliechinjwa
 
Mimi nilifichiwa chakula na shangazi yangu. Mwaka jana mtoto wa huyo shangazi ALINIOMBA NIMSAIDIE KUMPELEKA MAREKANI KUSOMA. Kweli usitende ubaya kwa mtu sababu ya kesho hauyajui. Full story hapa chini....

Nilikuwa nasoma Ilboru, mjomba (mdogo wake mama) na mke wake (shangazi) alihamishiwa kikazi arusha tokea dar, wakawa wanaishi sanawari. Nilifurahi kupata ndg wa karibu arusha, tena sanawari na ilboru secondary ni karibu mno. Mama mzazi ndio alimsomesha huyo mjomba sekondari hadi chuo. Basi nikadhani nao watanijali. Uncle alikuwa mtu wa safari sana za kikazi, kwa hio mara nyingi mkewe ndio alikuwa home arusha.

Mara mbili au tatu kwa mwezi (siku za jumapili) nikawa naenda kuwasalimia. Mara za kwanza mambo yakawa sawa tu. Huwa wanakula vizuri sana, kwa hio nilikuwa nabadili diet vizuri sana.

Baada ya miezi miwili hivi kuisha tokea wahamie arusha, mambo yakawa sio mambo. Nikienda kuwasalimia, huwa naenda mida ya saa nne, nakula lunch, halafu naondoka saa kumi hivi. Ikawa sasa naenda hadi naondoka hakuna msosi.

Hiyo ya kwenda na bila kupata msosi ilitokea kama mara tatu hivi. Mara ya nne sasa.. kitu hicho hicho.. nikakaa, hakuna kitu, njaa kweli yani hadi akili hafikirii vizuri kiasi cha mimi kusahau MADAFTARI YANGU hapo kwa uncle sababu nilikuwa naenda nayo kujisomea.

Basi kufika njiani nikakumbuka nimeyasahau hayo madaftari, nikarudi kwa uncle kuyachukua. Nikakuta WAMEJAZA MEZA CHAKULA WANAKULA. Hapo hata dakika 20 tokea niondoke hazikuisha. Manake chakula kilishapikwa zamani na walikificha.

Ilini-pain sana, lakini hio ni moja ya mambo yaliyonipa uchungu na maisha. Niliandika barua mbaya sana kwa uncle kumshitaki, ila ndg wakasema nimekosea heshima. Ndg nao wakamsapoti aunt.

Leo hii katika familia YOTE UNCLES NA AUNT, mimi ndio fogo kupita wote. Nimejenga sana, magari kibao, na pia nina projects zangu USA ambako nilikuja baada tu ya kumaliza form IV na ndio palinisaidia ku-win life. Na ndio hao walionitendea ukatili kama huo leo wananinyenyekea ili niwasaidie.
Pole sana mkuu tunaomba ajira
 
Nipo form si kipindi hiko, nikaenda hospitali kumsalimia classmate (wakike) alikuwa amelazwa hospitali ya mission karibu na shule. Wakati nipo kitandani Dr akaingia na kutufukuza, sikumbuki nilimjibu nini. Kesho jumatatu kengele ya dhalula inagongwa mida ya saa tano wote tukaenda assembling ground. Mara naitwa jina toka mbele na mwalimu mkuu akiwa na discipline master na yule Dr. Akasema ndio huyu aliyekuwa anakula mate na mgonjwa.
Aisee nilichezea bakora hapo, Mimi ndio nikawa mfano wa watu wanaotafutwa wenye mademu shuleni (maskini ya Mungu hata hakuwa demu wangu). Nikaulizwa nichapwe bakora 20 au nipewe suspension? Nikawaza ukali wa mzee, nikakubari bakora. Nilichapwa zaidi ya bakora 20
Yule demu alipokuja kusikia baada ya kupona alimvaa Dr alafu akaenda kusema kwa mwalimu mkuu, kumbe alikuwa anamtaka kitambo tu anamchomolea. Lilikuwa gumzo, Ila wakayamaliza kiutu uzima huku mimi, nilishaumia.
Baadae yule demu akaja kuwa demu wangu kiukweli sasa tukiwa vyuo tofauti. Tulikuwa tukikumbushiana hiyo stori anacheka na kusema sasa tunafanya kweli au walitutabiria
Now ni friends wa kawaida ameolewa na watoto wawili, we are happy
Unapasha kimasihara.
 
Yeah wapo pamoja mpaka kesho, kaka anajua kila kitu ila ndio hivyo tena tangu kipindi hiko hakuna aliewahi kumkumbushia mwenzie chochote kuhusiana na hayo maisha zaidi ya salam tena salam ni kaka ndio alianza, mimi niliondokaga kwa hasira nikawa sitaki hata kuwasikia ila mwisho wa siku niliona haina haja sote mavumbini tutarejea nikasamehe lakini wifi sijawahi onana naye na Mungu alivyo wa ajabu kila wakija home mimi sipo au mimi nikienda wasalimia kwao siwakuti sijuagi why inakua hivyo ni muda mrefu mnoo umepita na salam zenyewe ni kupitia mitandao ya kijamii
....Unasamehewa kwa sababu tu ilikuwa bado mdogo!
Huu ndio unsfiki wetu waafrika ambao tunatakiwa kuupiga vita kwa nguvu zetu zote!
Umemsikia dhahiri shemeji yako na mama yake wanakusema na kukupangia ubaya wa kukufungia mlango ili wakunyime chakula alichonunua kaka yao, halafu Wewe ndio unasusa na kukimbilia kwenu hivi hivi?
Hapo Mimi ungenipenda Comrade.
Pamoja na Udogo wangu ningeliwatokea na kuwaambia nilichosikia na mipango yao dhalimu waliyopanga kunifanyia...na kaka ningemjulisha kilichotokea mbele yao na ndio ningeomba anipe nauli nirejee home nimuache na wajinga wake roho mbaya wale!!!
 
kipindi niko form 3 nilihama shule. kutoka shule ya kijijini kwetu kuja shule ya mjini ingawa zote DAY. hapa mjini nilikua nnaishi kwa dada yangu ambaye alikua ameolewa. pale kwa dada nilikuta jamaa wengine wawili ambao ni wadogo wa shemeji. hawa jamaa moja alikua anasoma form 5 mwingine alikua tuu yupo pale home.

unyanyasaji niliopata pale ni wa kisaikolojia kutoka kwa shemeji. shemeji alikua akitoka anapenda mambo ya fashion saana. kununua nguo na viatu anapenda mno. so kila akirudi utakuta kanunua nguo kibao zake na za wale wadogo zake. mimi sikuwemo katika mgao. viatu American buti zile anawaletea wadogo zake me sipewi. basi nilikua naumia moyo sana. hadi ninamaliza form four sijawahi pewa nguo hata ya kuachiwa na shem. nakumbuka nmewah pewa singlend tuu na ni kwa sababu aliyenunuliwa haikumtosha.

zaid ya hivo wale wadogo zake shem walikua na roho kama kaka yao tuu. mfano utakuta tuko sebulen tuna chek tv, km yy anataka kutoka basi anainuka na kuzima tv. anasepa na mm nipo hapo sebulen. na kuwasha TV siruhusiwi.

sister alikua hapendezwi ile ya kuzuiwa kuchek tv na ikawa inafanya wagombane ni vile tuu hana sauti.
 
Back
Top Bottom