Tukutane hapa tuliopambana na ndoto za kukojoa kitandani

togetherTight

Member
May 21, 2017
99
100
Salaam wakuu.

Katika uzi huu tuambizane namna tulivyopitia masahibu mbalimbali katika kupambana na tatizo la kukojoa kitandani, either utotoni au hadi katika utu uzima hasa kupitia ndotoni.

Binafsi katika umri wa kujitambua (miaka minne na kuendelea) sikuwahi kukojoa kitandani bila kupitia ubishi wa nafsi ndotoni.

Yaani nilikuwa nikiota nipo ktk harakati za kawaida katika maisha then nabanwa haja ndogo, tatizo linakuja ninapotaka kukojoa nilikuwa nikijishtukia km naota au ni uhalisia.
Nilijaribu hata kujirusharusha ili km ni ndoto bas niamke lakini mwisho ilikuwa nikujidanganya na kukojoa kitandani, hadi nilipokata shauri kuwa sitaruhusu kukojoa popote iwapo nilikuwa na wasiwasi kuwa ni ndoto, hadi niamke usiku huo au asubuhi.

Karibuni tupeane uzoefu tofautitofauti..
 
Back
Top Bottom