Tukusanye ule utabiri wote wa Samia kuwa Rais wa Tanzania

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Aisee ama hakika nlikuwa naperuzi peruzi page ya Instagram ya Madam President, aisee nimeshitushwa na mambo mawili.

1. Mara zote tangu awe makamu wa Rais 2015, amekuwa akiji promote kwa hadhi ya juu sana. Na hapa ndipo nimegundua ule msemo wa Bosi wangu Mkaburu 'Always promote your self'. Ukiangalia mwenendo wa post zake, utagundua amekuwa ni mtu wa kushiriki mambo mengi sana ya kijamii na kiuchumi. Pamoja na kuwa muislamu ila nimeona mara nyingi sana akiichanganya katika hafla za wakristu pia, pia nimegundua ni mtu anayethamini mahusiano ya kidiplomasia.

2 . Cha pili ni kwamba nimeshuhudia watu kadhaa wakiweka utabiri wao kwamba atakuja kuwa President. Hii hapa chini ni comment ya mtu ambaye aliitoa wiki karibu 200 zilizopita. Naanza kuamini kwamba viongozi huletwa na Mungu muda wao ukifika, na muda wao ukifika pia huondolewa kwa nguvu za kimungu. Huwezi kukataa hili. Ni kama kutimia kwa unabii

samia.JPG
 
Back
Top Bottom