Tukuru wanapingana na sfo?

TAKUKURU wako kwenye utekelezaji wa mkakati mkubwa wa kumwandaa Lowassa Kuingia ikulu 2015, Mkakati huo unanzia na KUmweka Chenge kuwa spika ili kuzuia mijadala yote iliyokuwa inaongelea mambo ya ufisadi, na baada ya miaka miwili hiyo issue ya ufisadi itakuwa sio issue, hapo ndipo Lowassa atakapo jiinua tena na kuja kwa kasi ya ajabu nadhani kama JK hatampa sasa uwaziri basi baada ya miaka miwili wakati hiyo issue ya ufisadi imekwsha atampa uwaziri labda hata kuwa kiranja wa mawaziri
 
he he he he he inatisha huyu ndo supika wetu, aisee naanza kutamani kubadili uraia
 
TAKUKURU wako kwenye utekelezaji wa mkakati mkubwa wa kumwandaa Lowassa Kuingia ikulu 2015, Mkakati huo unanzia na KUmweka Chenge kuwa spika ili kuzuia mijadala yote iliyokuwa inaongelea mambo ya ufisadi, na baada ya miaka miwili hiyo issue ya ufisadi itakuwa sio issue, hapo ndipo Lowassa atakapo jiinua tena na kuja kwa kasi ya ajabu nadhani kama JK hatampa sasa uwaziri basi baada ya miaka miwili wakati hiyo issue ya ufisadi imekwsha atampa uwaziri labda hata kuwa kiranja wa mawaziri

ni heri samwel sitta awe rais kuliko lowasa, nyerere alishasema aliyosema kuhusu lowasa....na hawezi kuwa kiranja wa mawaziri wkt alijiudhuru kwa kashfa....
 
Tatizo linaanzia kwa Kikwete mwenyewe,anajilinda mwenyewe kupitia kuwalinda akina Chenge kwa sababu anaogopa wakiumbuliwa watamuanika yeye pia, kwani walishasema vya kwao ni vijisenti tu.

Mwacheni Lowasa agombee asafishe njia kwa upinzani
 
Lowassa kura rais ni kiama TZ, ni mtu wa visasi sijawahi ona!!!!!!!!!!! Anatumia madaraka vibaya huyo hakuna mfano.
 
Hosea anatumiwa, kama alivyotumiwa na EL katika kashfa ya Richmond. Ni dhahiri anasema uongo kuhusu SFO. Ni bora asingeitaja SFO katika kujenga hoja yake ya kumsafisha Chenge. Someni stori hii hapa chini imetoka katika Mwananchi ya leo na nimeweka msisitizo kwenye red.Takukuru wamsafisha na kashfa ya ufisadi

Ramadhan Semtawa

TAASISI ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jana iliwasha moto mpya baada ya kutoa taarifa inayoeleza kuwa mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge hakuhusika kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, ikiwa ni siku moja baada ya mbunge huyo wa Bariadi Magharibi kutamba kuwa hahusiki.

Takukuru ilisababisha kizaazaa kama hicho mwishoni mwa mwaka 2007 wakati ilipotoa taarifa ya uchunguzi wa kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji wa umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development, ikielezea kuwa hakukuwepo na harufu ya rushwa kwenye tenda hiyo, jambo lililolifanya Bunge licharuke na kuunda kamati yake teule iliyofichua uozo mkubwa.

Taarifa ya kamati hiyo teule ya Bunge ilisababisha Edward Lowassa ajiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu na kufuatiwa na mawaziri wawili waliowahi kushika Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.

Wakati kashfa hiyo ikielekea kutulia, Takukuru jana ilitoa taarifa inayomsafisha mbunge huyo mteule wa Bariadi Magharibi katika kipindi ambacho Chenge ametangaza kuwania kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri, ambalo liliibua kashfa nyingi katika kipindi chake cha miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Takukuru iliyotolewa jana na afisa habari wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani uchunguzi wake kuhusu kashfa hiyo pamoja na ule uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza, umeshindwa kumhusisha Chenge na kashfa hiyo ya rada.

"Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa Rada umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge, katika tuhuma hizo," inasema taarifa hiyo fupi yenye aya mbili.

Kapwani ambaye alizingumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Takukuru, inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hicho kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na rushwa kwa kuwa jukumu hilo ni la wote.

Mwananchi ilipomuuliza mkurugenzi huyo mkuu wa Takukuru, Edward Hoseah sababu za kutoa taarifa hiyo sasa wakati uchunguzi ulikamilika tangu Februari, hakutaka kutoa ufafanuzi na badala yake alisema: "Nadhani afisa habari wangu amekwishatoa taarifa. Ni vigumu yeye aseme halafu na mimi niseme."

Hata hivyo, taarifa ya SFO kuhusu kumalizika kwa uchunguzi huo iliweka bayana kuwepo na ufisadi ambao ulifanyika kwa kutumia ujanja wa kutotunza kumbukumbu za fedha na hivyo kampuni ya BAE System, ambayo iliiuzia Tanzania rada hiyo kukiri kosa hilo na kulazimika kulipa faini ya pauni milioni 30 ambazo zinatakiwa zitolewe kwa taasisi za hisani za kusaidia Watanzania.

Pia serikali za nchi husika kwenye sakata hilo zilitakiwa kufanya uchunguzi wake na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa, kitu ambacho Tanzaania iliahidi kukitekeleza lakini ikitaka fedha hizo za faini zisiende kwa taasisi zisizo za kiserikali.

Hata hivyo, hakuna taarifa zozote zilizotolewa na serikali baada ya kumalizika kwa uchunguzi huo hadi juzi wakati Chenge alipotangaza kuwa hahusiki na kufuatiwa na taarifa hiyo ya Takukuru.

Chenge alitajwa kwenye kashfa hiyo, iliyotikisa Bunge la Uingereza, baada ya SFO kubaini kuwa alikuwa amehifadhi takriban Sh1.2 bilioni kwenye akaunti yake ya benki moja ya nje ya nchi. SFO ilibaini akaunti hiyo wakati ikifuatilia mzunguko wa fedha zilizonunua rada hiyo.

Baada ya SFo kutangaza matokeo ya uchunguzi huo, Chenge alilazimika kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Miundombinu na alipoongea na waandishi wa habari alisema kiasi hicho cha fedha ni "vijisenti tu".

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliahidi kuwa serikali ingewashughulikia wote waliohusika baada ya Kampuni ya BAE Systems kutangaza matokeo ya uchunguzi wa kashfa hiyo.

Siku hiyo, Februari 9, Membe alisema: "Lazima tulifikishe suala hili mwisho; yaani lazima tujisafishe... tukae vizuri ili tuonekane kwamba mashimo yote ya rushwa yamefukiwa. Na kama kuna mtu yeyote amehusika katika kashfa hii, hiki ndicho kipindi ambacho utawala bora wa Tanzania unatakiwa kuimarishwa."

Juzi katika mkutano wake na waandiashi wa habari kuhusu sababu zilizomsukuma kuwania kiti cha Spika wa Bunge la Muungano na kufafanua kuhusu "makandokando" yanayozunguka jina lake, Chenge alitamba akisema: "Ninavyojua mimi, SFO wamelifunga jalada la rada. Kuweni na ujasiri kwenda kuuliza Takukuru na DPP, mkishindwa mkome kulihusisha jina langu na rushwa ya rada."

Taarifa hiyo Chenge inamaanisha kuwa alishakuwa na habari kuhusu msimamo wa Takukuru kwenye kashfa hiyo.

Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP), Eliezer Feleshi hakuweza kuzungumzia suala hilo jana kwa madai kuwa alikuwa kikaoni na hata alipofuatwa ofisini, aligoma kuzungumzia suala hilo.
 
Wana JF,

Twaomba Tujua shughuri Kuu muhimu za TAKUKURU ndani na Nje ya nchi hiii?

TAKUKURU leo ndio Chajifanya ndio CIA,FBI,MI6,MOSSAD,KGB,NSA ya Tanzania???? au mbona watakuwa ni wanafiki hawa.

Hivi TAKUKURU wanatuonaje sie WATANZANIA jamani kwa kuwa hatuzi jui sheria au?? jamani hawa wajamaaa nadhani wanatakiwa warudi tena Darasani kuperuuuzi na Kudadisi kuona kama watanzani ni mazuzu kiasi hicho.

SFO walituma report huku TZ na hakuna hata tume imeundwa kwenda UK kujiridhisha kwa madai hayo na kama iliundwa basi ni kinyume na katiba ya nchi na kulikuwa kuna jambo ndani la kumlinda mtu hapo.
 
Back
Top Bottom