Tukumbushane yaliyojiri mlipuko wa mabomu ya Gongo la Mboto

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,912
Nakumbuka siku hiyo wakati ukitokea mlipuko wa mabomu maeneo ya Gongo la mboto, nilikua sinza, ghafla nikaanza kuona miale ya moto juu ya anga, binafsi nilihisi labda tayari kimenuka.

Naanza kutafuta namna ya kuwatafuta watu wangu wa karibu naona simu hazitoki, nikasema ehee.

EBwana wee siku hiyo ilikua ya tofauti kidogo ila kesho yake tukaanza kupokea wakimbizi wa muda.

Wakati haya yanayotokea ulikua wapi na ulikua ukifanya nini?
 
Nilikuwaga bado sijaja Dar chuo kikuu nilikuwa pande za kijijini nikasikiaga tu kwenye habari na hivi hata smartphone sikuwa nayo bado naweka kambi Hapa kusoma tu comments.
 
Nakumbuka siku hiyo wakati ukitokea mlipuko wa mabomu maeneo ya Gongo la mboto, nilikua sinza , ghafla nikaanza kuona miale ya moto juu ya anga , binafsi nilihisi labda tayari kimenuka...
Nakumbuka siku hiyo mi nilikuwa zamu wakati nataka kuingia mle ghalani nilisikia kitu kinacheua kama mtu kafunua bia kidogo nikatoka mbio kumuita afisa wa zamu kabla nilipofika pale main get ndo nikasikia.

Nitamalizia baadae boss kaja.
 
Kila yanapotokea mambo makubwa kitaifa hua napata habari kwenye tv
Siku anapotea kanumba nliwashavredio asubuh nakutana na taarifa
Siku ya nabomu nlikua naangalia tv naona chin maneno yanapita
Dah rip ndugu zetu
 
Mjini mipango kweli

Kipindi kile,kashfa kidogo tu unautema Uwaziri lakin Hussein Mwinyi hakutema Uwaziri pamoja na mabomu yote yale akiwa Waziri, lakin mwenzie Shamsi Vuai aliutema Uwaziri huo huo wa Ulinzi kwa kuwa tu watu walichapwa viboko na Askar wa JWTZ kwenye operation Tokomeza

Mwinyi mtu wa Chenga sana

Anaondoka Wizara ya Afya nyuma yake ukatokea Mgomo Waziri wa wakati huo Dr Mponda akapoteza Uwaziri

Mwinyi anaondoka Wizara ya Ulinzi anaenda Afya Nyuma yake kunatokea Operation tokomeza na hatimae Shamsi Vuai anapoteza Uwaziri kwa shinikizo la Wabunge
 
Hiyo mbona ishu ndogo sana,sema nashindwa kuelewa kwanini casualties ilikuwa juu sana

Huku damusca hivyo ni vitu, kutwa mara tatu
 
Mjini mipango kweli

Kipindi kile,kashfa kidogo tu unautema Uwaziri lakin Hussein Mwinyi hakutema Uwaziri pamoja na mabomu yote yale akiwa Waziri, lakin mwenzie Shamsi Vuai aliutema Uwaziri huo huo wa Ulinzi kwa kuwa tu watu walichapwa viboko na Askar wa JWTZ kwenye operation Tokomeza

Mwinyi mtu wa Chenga sana

Anaondoka Wizara ya Afya nyuma yake ukatokea Mgomo Waziri wa wakati huo Dr Mponda akapoteza Uwaziri

Mwinyi anaondoka Wizara ya Ulinzi anaenda Afya Nyuma yake kunatokea Operation tokomeza na hatimae Shamsi Vuai anapoteza Uwaziri kwa shinikizo la Wabunge
Lilikua tukio lililozua taharuki na heka heka za aina yake.
 
Nilikua mwaka wa kwanza Ifm nikiwa naishi mtaa wa feri kigamboni karibu na kanisa la kkkt pale.
Mida hiyo nilikua hostel
 
Mie nilikuwa mikoani kikāzi. Mke wangu na watoto walikimbia toka Kipunguni hadi Kibangu usiku huo. Kwa hakika mtu hawezi kulizidi bomu spidi - lakini walijiwa na wazo la kukimbia.

Kulikuwa na uzi wa tukio hilo humu. Niliandika comment kadhaa za kulaani waliozembea hadi hali ile kutokea.
 
Pole sana mkuu.
 
link yake naiomba
 
link yake naiomba

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!
 
Back
Top Bottom