Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Niko hapa nasikiliza "Christina Moshi" Rudia posti ya mwanzo nitawapatia nilizonazo hapa na kama kuna mtu anazo angependa kushare nitumie kwenye email yenye jina la "mwanakijiji" kwenye anuani hii ya jamiiforums.

"tulipokubaliana kwa hiari, tulikuwa wawili, watatu mungu wetu!!" .. kibwagizo mwah.. silali leo; mtakoma!

nakutumia muda mfupi ujao
 
Siku uliyoondoka, uliniacha nalia na machozi. Umekwenda kuishi mbali nami, eorgina wa mamaaa. Sipati usingizi nikikumbuka tulivyoishi mimi nawe..
.Huyo Ndiyo Georgina. At one point ilikuwa nyimbo iliyobeba maana kubwa sana kwangu maana nilipitia kisa cha aina ile ambayo Marijani Rajabu alijaribu kuisimulia.
 
Hii thread imetulia sana, nakumbuka nyimbo za Bimalee enzi za akina Roy, Beresa, Jumbe, Marijani nk. Kuna wimbo una-verse zifuatazo nadhani unaitwa margaret

shangazi yako nae akakusihi sanaa
uje kumuona mama Margaret ukapuuza
kukaa kwako mjini faida zake umeziona
wazazi wako wawili sasa wameshakutola

Halafu kali ni ule wa mwishomwisho wa maisha ya Dudumizi unaitwa Theresa by Vijana Jazz enzi za 80s (RIP Jerry)

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu
siku ya harusi

Theresa, penzi gani analokupa wewe theresa
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa

.........................................
 
Zuwena, Zuwena kweli nampenda..
Mtoto aliyeumbika mwenye tabia za kupendeza
 
CHRISTINA-DDC MLIMANI PARK:
Ama kweli penzi jamani, halikadiriki, hata ulipime kwa mzani gani x2,
Nililichezea kamari, penzi lake Christina na kujisahau kama lingenikaa na kudumu maishani x2.....

Chorus:
Niliichezea kamari roho yangu na kuuza utu wangu x2
Kwa wasiothamini penzi wala maana ya kupendwa!

Kwa kweli Christina leo naomba unielewe........(SAMHANI HAPA SIKUMBUKI!!!)
Nilihadaika na mambo ya dunia (Christina),
Nilihadaika na anasa za dunia (Ooo Mama),
Binadamu hujifunza kutokana na makosa.....
Niliichezea kamari roho yangu na kuuza utu wangu x2
Kwa wasiothamini penzi wala kujua maana ya kupendwa!
Jamani... Ni hatari!!!!
 
Tuzikumbuke pia nyimbo hizi:

Konjesta-Sikinde
Edita-SikindeMama Chichi-Selemani Mbwembwe & Vijana Jazz
Theresa-Vijana Jazz

..Kipenzi changu Edita sikia nikupe ukweli niliokuwa naoooo kusema kweli nimechoshwa natabia zakoooo x2

Nikuulizapo ulikuwa wapiii, ulikuwa kwa shangazi kariakoo......

beti nyingine sikumbuki
 
TAUSI- Juma Mrisho Ngulimba wa Ngulimba (Urafiki Jazz Bandi) ....Tausi huyo wala sio ndege ila ni mwanadamu mwenye kusifika..nimesimama chini ya mbuyu nimejinamia Tausi wangu karuka nabaki nalia..
 
Hii thread imetulia sana, nakumbuka nyimbo za Bimalee enzi za akina Roy, Beresa, Jumbe, Marijani nk. Kuna wimbo una-verse zifuatazo nadhani unaitwa margaret

shangazi yako nae akakusihi sanaa
uje kumuona mama Margaret ukapuuza
kukaa kwako mjini faida zake umeziona
wazazi wako wawili sasa wameshakutola

Halafu kali ni ule wa mwishomwisho wa maisha ya Dudumizi unaitwa Theresa by Vijana Jazz enzi za 80s (RIP Jerry)

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu
siku ya harusi

Theresa, penzi gani analokupa wewe theresa
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa

.........................................

Bibii,hoteli gani hujalala maama,kinywaji gani hujakunywa mama,chakula gani hujakula maama,basi sema raha ipi unataka ili nielewe niiponye Roho yangu,Theresa

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi

Theresa, penzi gani analokupa huyo kijana
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa,mamiii

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi

Mkulu De Novo,respect yaani Dudumizi alikuwa ni Hazina kwa kweli
 
Naipenda JF, mfano hakuna.Hata nichukie namna gani nikija JF, najikuta narudi panapostahili na kuendelea na shughuli ipasavyo.
Thank you all.
 
Aza Aza, waraka ulotuma nimepata, punguza wasi kijana,
Kuna mengi nimesikia lakini, ah! Nimedharauuuuuuu!!!
 
July eeeh, nikupe nini uridhike, July eeh cha kukupa sinaaa mamaaaa.

Ufukara nilionao mamaa, ufukara umekuwa kashfa kwa mapenzi yangu, kwako kwako eeh.

........ hata sitiri nafsi yangu wee mamaaa, thamani ya kukupenda eeeh July, naomba ufahamu hivyo oooh mama.
Nimeshiriki dunia nzima kukupenda eeh, lakini wewe kipenzi mwenzio nasema

nasikitika iyoo mama eeh nasikitika iyo mamaaa aa.
July eeh July eeh, nasikitika iyo mamaaa.
 
Naipenda JF, mfano hakuna.Hata nichukie namna gani nikija JF, najikuta narudi panapostahili na kuendelea na shughuli ipasavyo.
Thank you all.
karibu sana!
''YOU CAN'T VERIFY AND TRUST KILAKITU BWANA!....:D''
 
Bibii,hoteli gani hujalala maama,kinywaji gani hujakunywa mama,chakula gani hujakula maama,basi sema raha ipi unataka ili nielewe niiponye Roho yangu,Theresa

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi

Theresa, penzi gani analokupa huyo kijana
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa,mamiii

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi

Mkulu De Novo,respect yaani Dudumizi alikuwa ni Hazina kwa kweli

Mkuu yaani mpaka machozi yamenitoka aisee, nakumbuka tuna redio kaseti za spika moja aisee... national!!! They guy was unique ni pombe tu aisee

Sasa kuna moja inaitwa imacculata

bibi imakulata yeye
haloo imakulata mamaa
nakutafuta sikuoni bibi
napiga darubini sikupati eh ehe heheee

ni umbali gani ulipo? nijulishe
nipigie simu namba 26561 ahaaa x2

Haki ya mungu
nakupenda imakulata
nachotaka njoo nishike mkono
twende mbele ya wazee

GAdemu!!
 
Hiba, nimelibeba pendo lako, kama mwana na mbeleko x2
Nina maana kukwambia, mchana usiku silali, natafuta pesa,
Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora, yenye thamani na penzix2

Hiba oo Hiba, imekuwaje Hiba hiba oo Hiba nielezee oo!
Ninapokuuliza hutaki kusema nami Hiba, ninapokuuliza wewe unanunanuna....
Unanisikikitisha sana unapokataa kula nami Hiba...........
 
..Kipenzi changu Edita sikia nikupe ukweli niliokuwa naoooo kusema kweli nimechoshwa natabia zakoooo x2

Nikuulizapo ulikuwa wapiii, ulikuwa kwa shangazi kariakoo......

beti nyingine sikumbuki

Kipenzi changu Edita sikia nikupe ukweli niliokuwa naoooo kusema kweli nimechoshwa natabia zakoooo x2

Ni siku nyingi nilielezwa mengi niliyapuuza,nilijua ni fitina za majirani tu wanataka kututenganisha(rudia tena)

Lakini leo nimeamini,kipenzi Edita methali ya Kiswahili yasema kwamba lisemwalo lipo(rudia tena)

Nikitoka kazini sikukuti,nikuulizapo ulikuwa wapi,nilikuwa kwa shangazi Kariakoo,kumbe una wako wa Pembeni kipenzi Edita

Hukuridhika umemleta kwangu wakati sipo nipo kazini,waweza kuchukua kila chako uende zako,kipenzi Edita

Nikitoka kazini sikukuti,nikuulizapo ulikuwa wapi,nilikuwa kwa shangazi Kariakoo,kumbe una wako wa Pembeni kipenzi Edita
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom