Tukumbushane; Wakumtoa Kafara haujichagulii mwenyewe isipokuwa unachaguliwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
KAFARA HAUJICHAGULII MWENYEWE; UNACHAGULIWA.

Na, Robert Heriel

Naomba tukumbushane kidogo,

Ili mtu yeyote afanikiwe lazima kafara lihusike, upande wowote ule iwe Kwa upande wa Mungu au upande wa Shetani,
Na Kwa wale wasioamini masuala ya Shetani na Mungu basi, tunaweza iweka iwe upo upande mwema au upande wa Uovu.

Kafara lazima litolewe ili ufanikiwe.

Kwa bahati mbaya Kama sio nzuri kafara haujichagulii, Bali unachaguliwa na huyo unayemuomba Msaada au mafanikio.

Kuna watu waliwahi kwenda Kwa waganga WA kienyeji wakiwa wamejipanga kabisa kuwatoa watoto wao Kafara, lakini walipofika Kwa waganga wakaambiwa tofauti na walichokuwa wamefikiria,

Siku zote kile unachokipenda kuliko vyote ndio hupendekezwa kitolewe kafara.

Kama unapenda watoto wako zaidi basi ukienda Kwa mganga au Kwa Mungu basi hicho ndicho utakachoambiwa ukitoe, utoe Yule mtoto umpendaye.

Kama unampenda Mkeo au mumeo, na hapa nazungumzia upendo uliopitiliza sio ule upendo wa juu juu. Basi ukienda Kwa waganga au Kwa Mungu kuomba msaada basi jua kafara litamhusu Mkeo/mumeo.

Kuna watu huenda Kwa waganga, wakifika wanaambiwa hapa hakuna makafara ya kumwaga damu, lakini hupewa masharti kwenye sehemu nyeti mno, mfano mtu Kama anapenda kunywa pombe ataambiwa asinywe pombe mpaka anaingia kaburini, au kama anapenda wanawake basi ataambiwa asichepuke awe na Mke mmoja tuu, yaani lazima utoe kafara kile ukipendacho kuliko.

Ni kawaida mtu akahangaika sana kwa njia halali na siku anakaribia kufanikiwa unakuta Mama/Baba yake anakufa au mke au mume wake anakufa. Mtu huyo hulia Sana, huona Mali alizozipata hazina thamani Kama aliyekufa.

Ukiomba mazuri iwe Kwa Mungu au Kwa Shetani basi jua umeamua kumtoa au kutoa kafara moja ya vitu ulivyonavyo unavyovipenda Sana.

Hakuna Duniani aliyefanikiwa pasipo kutoa Kafara. Kafara ndilo humfanya mtu awe na roho ngumu Sana.

Ni hatari kutafuta mafanikio Kwa ajili ya mtu mwingine au ya starehe Fulani, kwani hicho hicho umachohangaikia ndicho unachokifanyia replacement na mafanikio uyatafutayo.

Wengi waliotafuta pesa ili wanywe na wastarehe waliishia kuambiwa wasitumie tena vilevi na waliokaidi Walikufa.

Wengi waliotafuta mafanikio ili Wale vizuri waliishia kupata magonjwa ya uzito uliopitiliza, unene, shinikizo la damu, sukari n.k wakaambiwa wapunguze au waache kabisa Kula vyakula hivyo.

Apendaye Sana huumia Sana.
Maisha yanahitaji kiasi.
Ukihitaji ziada utapaswa ufanye ziada, lazima utoe kafara.

Lengo la maisha ni kuishi kawaida, Kupata matokeo yakawaida.

Hata waliotaka kufaulu kwa kiwango cha juu walitoa kafara muda na nguvu zao Kwa kusoma usiku kucha, walitoboa ozone ili tuu wapate daraja la Kwanza,

Maisha ya kawaida ndiyo yaliyokusudiwa yawe yafuraha.

Ukihitaji mafanikio makubwa jua IPO tayari kutoa Kafara moja ya mambo uliyonayo uyapendayo, je ni Mama au Baba yako sijui, je mi Mkeo au mumeo sijui, je mi mtoto Mimi sijui, au je mi Afya yako?

Penda kiasi, mafanikio kiasi.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kuna watu hawatakuelewa simply Kwa sababu kwao kafara wanahusisha na ushirikina.

Labda neno kafara unge substitute na neno sadaka nadhani wengi wangeelewa, na nadhani ndicho haswa unachomaanisha.

Mungu ndio wa kwanza ku set standards za utoaji sadaka ili upate ukitakacho kwa kumtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwa ajili ya binadamu.

Abraham Baba wa Imani aliweka mzigo wa mwanaye pekee mezani ili apate kutunukiwa cheo cha Baba wa Imani.

Ukitaka kuwa TO weka mezani (sadaka) muda wako and everything.

Nadhani andiko lako lina muelekeo huu.
 
Kuna watu hawatakuelewa simply Kwa sababu kwao kafara wanahusisha na ushirikina.

Labda neno kafara unge substitute na nebo sadaka nadhani wengi wangeelewa, na nadhani ndicho haswa unachomaanisha.

Mungu ndio wa kwanza ku set standards za utoaji sadaka ili upate ukitakacho kwa kumtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwa ajili ya binadamu.

Abraham Baba wa Imani aliweka mzigo wa mwanaye pekee mezani ili apate kutunukiwa cheo cha Baba wa Imani.

Ukitaka kuwa TO weka mexani (sadaka) muda wako and everything.

Nadhani andiko lako lina muelekeo huu.


Haswa, nafikiri umelielezea vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom