jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,128
- 8,646
Leo nmejikuta nacheka mwenyewe.
Nakumbuka nilikuwa najisomea mwenyewe humu humu kuhusu Covid 19 wakat huo ikiwa iko China na kuhesabia ni gonjwa la wenzetu tu kwetu halitofika.
Ghafla siku isiyokuwa na jina ndo mgonjwa wa kwanza akatangazwa hali ikaanza kuwa tete watu full kuvaa mabarakoa. Mimi kiukweli zilinishinda na nkasema kuwa kamwe sitokuja kwenda quarantine ila Mungu akanambia mimi ndo mpangaji siyo wewe.
Nikiwa hospital moja ya Aga Khan bwana wakati naenda kupima vipimo nikawa naskia kuwa kuna semina ya manesi mle kwa ajili ya jinsi ya kujikinga na Corona na jinsi ya kuhudumia wagonjwa wa Covid 19, basi nikafanya kila njia na mimi nikaingia kumbe jana yake kuna mgonjwa walimgundua ana Corona Serikali ikamfuata then wakaambiwa wauguzi wote waliomhudumia yule mgonjwa wa Corona watafanyiwa semina.
Basi na mimi kufosi fosi ile nikawa mmoja wapo, walikuwa wauguzi wote, kumbe ilikuwa danganya toto kilichofata hapo wote nikiwemo na mimi kupelekwa quarantine.
Asikwambie mtu hakuna kitu kinachoweza kumuua binadamu kama hofu. Nashukuru Mungu wote tulipona na kuruhusiwa kurudi nyumbani japo wengi walikuwa hawana.
Baada ya kurudi nyumbani ndani ya week 2, nikaanza dalili zote za Corona kwenda kupima nikakutwa nina corona hivyo nikawekwa quarantine nyumbani kwangu nashukuru Mungu kwa kunipa mke mwenye nguvu ambae mbali na hofu zote za wakati huo kuhusu corona lakini alikuwa akinilisha na kulala na mimi nyumba na chumba kimoja ndani ya shuka moja hali ya kuwa ndugu zangu tu walikuwa wananikimbia.
Mtu wa mwisho ni bosi wangu ambae kila tukionana lazima acheke sana maana leo nimeenda kupima nikakutwa na corona jana yake nilishinda nae kutwa nzima baada ya kumwambia bosi nina corona kwenye simu alilia sana nakumbuka kauli yake moja tu "Jerry umeniua jerry nimekufa mimi"
Tupeane vituko vya Corona kwa upande wako