Tukumbushane visanga na Sheria za nyumbani enzi za utoto

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Mimi nakumbuka familia yetu wazazi hawakuwa strict sana kivile kiasi cha kuogopwa na watoto. Ila kuna Sheria 3 kuu ambazo watoto hasa wa kiume ilibidi tuzifate na kuzitii kama tulihitaji kuendelea kuishi kwa amani na utekelezaji wake ulikuwa unasimamiwa kwa hali ya juu sana.

1. Hakuna kula kama hujaenda kanisani.
2. Hakuna kula kama hujaoga
3. Kila mtoto wa kiume ataosha vyombo kwa zamu zilizowekwa.

Wewe unakumbuka nini?
 
Hahahaha inaonekana mzee alikuwa hacheki na mtu
 
1. Kuosha vyombo kabla ya kwenda mpirani.

2. Kuosha vyombo kabla ya kwenda shule

3. Kurudi kabla ya saa 18:00 kuingiza kuku

4. Nitarudi kuleta zaidi aisee ila zile dose zinanishukia nisipofata hizo.
 
Ukirudi nyumbani mwisho sa 12...

Nilikuwa narud saa2 usiku nachapwa ila kesho tena saa 2 usiku nachapwa kesho tena saa2 usiku

Mzee akabadili sheria ikawa saa2 usiku nikaifuata hadi form 2 nikaivunja nikaanza kuivunja nikawa narudi saa4 usiku napigwa kesho narud saa4 usiku

Katika maisha yangu hamna kitu sipendi km kunyimwa uhuru

Cha ajabu nilivyokuwa nikawa narud saa1 usiku mwenyewe tena advance level yote mimi saa 1 usiku nipo ndani...
 
Hakuna kuchelewa kurudi yaani kabla ya saa moja uwe umerudi

Mzee wangu hata leo nikienda kwake ni mtabe kwenye hili yeye anasema kama unachelewa uchelewe ukiwa kwako na sio kwangu
 
Ukirudi nyumbani mwisho sa 12...

Nilikuwa narud saa2 usiku nachapwa ila kesho tena saa 2 usiku nachapwa kesho tena saa2 usiku

Mzee akabadili sheria ikawa saa2 usiku nikaifuata hadi form 2 nikaivunja nikaanza kuivunja nikawa narudi saa4 usiku napigwa kesho narud saa4 usiku

Katika maisha yangu hamna kitu sipendi km kunyimwa uhuru

Cha ajabu nilivyokuwa nikawa narud saa1 usiku mwenyewe tena advance level yote mimi saa 1 usiku nipo ndani...
Umegundua nini?

Ulipofika advance ulijitambua

Ila huku chini ulikua unaendeshwa na mob psychology na ulikua unachelewa for nothing nina uhakika na hilo
 
Ofcourse ni story tu za kijinga na washikaji
 
Vikojozi hakuna kunywa maji au kinywaji chochote kile ikishafika saa 1 usiku
Hii umenikumbusha mkuu, huyu ni mimi kabisa. Aisee nimeyamwaga sana kitandani baba na mama walipata sana tabu lakini haikua makusudi basi tu ilikua inatokea. Sasa kimbembe wakati naenda Form one, mzee aligoma kununua godoro akaamuru niende na godoro nililokua nakojolea. Basi bana nikaenda nikatafuta fundi akanitengenezea cover la kufunika ramani za mikojo zisionekane, mie huyo nikazama zangu skuli.

Kasheshe ni pale nilipoyamwaga halafu nilikua nalala na bro fulani hivi yeye alikua form 6, kuanzia siku hiyo niliamua kubadili ratiba ya kulala, nilikua napiga misuli mirefu kulala mie ikawa ni saa 9 or kumi usiku saa kumi na mbili nipo macho. Kunzia hapo nikawa nimeagana na kukojoa. Ila ile hali ilinitesa sana.

NB: Kukojoa kulikua na manufaa sana kwangu, Kutokana na kupiga ile misuli mirefu kuna baadhi ya masomo nilikua sishikiki class na ndio mambo niliyobobea hadi leo.
 
Aisee hiyo noma sana mkuu...!! Ratiba ya Kurudi nyumbni mwisho saa moja yani

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Ukirudi nyumbani mwisho sa 12...

Nilikuwa narud saa2 usiku nachapwa ila kesho tena saa 2 usiku nachapwa kesho tena saa2 usiku

Mzee akabadili sheria ikawa saa2 usiku nikaifuata hadi form 2 nikaivunja nikaanza kuivunja nikawa narudi saa4 usiku napigwa kesho narud saa4 usiku

Katika maisha yangu hamna kitu sipendi km kunyimwa uhuru

Cha ajabu nilivyokuwa nikawa narud saa1 usiku mwenyewe tena advance level yote mimi saa 1 usiku nipo ndani...
ndo ile wanasemaga akikua ataacha
 
Hii umenikumbusha mkuu, huyu ni mimi kabisa. Aisee nimeyamwaga sana kitandani baba na mama walipata sana tabu lakini haikua makusudi basi tu ilikua inatokea. Sasa kimbembe wakati naenda Form one, mzee aligoma kununua godoro akaamuru niende na godoro nililokua nakojolea. Basi bana nikaenda nikatafuta fundi akanitengenezea cover la kufunika ramani za mikojo zisionekane, mie huyo nikazama zangu skuli.

Kasheshe ni pale nilipoyamwaga halafu nilikua nalala na bro fulani hivi yeye alikua form 6, kuanzia siku hiyo niliamua kubadili ratiba ya kulala, nilikua napiga misuli mirefu kulala mie ikawa ni saa 9 or kumi usiku saa kumi na mbili nipo macho. Kunzia hapo nikawa nimeagana na kukojoa. Ila ile hali ilinitesa sana.

NB: Kukojoa kulikua na manufaa sana kwangu, Kutokana na kupiga ile misuli mirefu kuna baadhi ya masomo nilikua sishikiki class na ndio mambo niliyobobea hadi leo.
hahahaha kwamba ulitumia changamoto yako kama fursa..gud.
 
Pindi nipo promary
Digi alikuwaga mtata sana, Ulitoka shule ni kumwagilia migomba, Kuchukuwa chakula cha Nguruwe kwenye hotel kwa zamu mimi na mdogo wangu, kipindi cha kilimo kulima mashama mbali na mji km 50 toka home kwa baiskeli.

Hamruhusiwi kutoka kabisa kwenda kucheza, wakati mwingine unajiiba badala ya kwenda tuition ndio unaenda kucheza siki timu yetu ya mpira ya mtaani ikiwa na game unazuga mmeambiwa mrudi shule hivyo yaani.

Siku ajue mlienda kucheza mtakula mboko mpaka basi

Kuna siku kulikuwa kuna game timu ya myaani na timu nyongine, nikasema leo lazima niende kwa vyovyote vile, bahati mbaya sana, siku hiyo ni siku maji yanatoka, lazima umwagilie migomba na bustani, nilichokifanya, nilienda kufunga maji kwenye coke kubwa, inayoleta maji home, maza akasema mbona leo maji yamekatika mapema si kawaida, akasema ngoje akacheck kwenye coke kubwa, duh kufika jamaa wakamwambi mbona mwanao ndio kaja kufunga hapa, maza akatulia tuli, akazuga kama hajamindi vile akapita karibu yangu alininyaka kama kuki vile, alinishushia kipigo cha hatari.

Kila nikifurukuta ananidhibiti kwa miguu, kama anachinja kuku, nikaona hapa naweza kupoteza uhai, ikabidi nijifanye kama nazimia hivi, nageuza geuza macho na kukoroma, alitoa bonge la tusi shenzi linajifanya limezimia kipigo kikazidi, nikaona ishakuwa so hii, nilimuomba msamaha huku nalia, ndiyo akaniachia siku hiyo milimwagilia halafu siku hiyo maji hayakukatika nimwagilia mpaka usiku sana.

Sekondary
Nilikuwa shakuwa kidogo uhuru lakini home ni mapema saa 1 usiku, kumwagilia migomba na bustani, kulima mashamba ni lazima, minyoo ya kihuni, kuvaa kihuni hakuna.
 
mzee alikuwa mtata sana
 
Back
Top Bottom