Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Revola

Revola

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
1,166
2,000
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
 
jaap

jaap

JF-Expert Member
Dec 25, 2018
904
1,000
Sauda kilumanga alichaguliwaga kwenda south Africa kuigiza thamthilia ya is dingo watu wakauliza je atakubali kupigwa denda
Yaaaani huyo Dada Kama unapicha yake hebu niwekeee nimuone si alikuwa mweusi hivii
 
Revola

Revola

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
1,166
2,000
Daaah Mzee umenikumbusha mbali Sana aiseeeee kitamboo sana, hivii hauna ka video kake?
 
Revola

Revola

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
1,166
2,000
Aisee zama hizo zilikua tamu sana.kwa cartoon nilikua napenda silverhawks,captain planet,double dragon,supermario,sonic,batman,flintstone na bila kusahau shivooooooo.kwa movies na series ni RoboCop, Mzee WA totoz point man jamaa alikua anapenda kuvaa pluneki,seketo dia ya mooo.kabla muvi haijaanza lazima kile kibwagizo niimbe nao..secreto diaaaaa moooo secretoooo secretoooo diaaa mooo.isidingo niliifatilia kipindi imeanza kulikua na jamaa matata anarasta derick nyati,Tausi kina mujuba aisee nilikopi adi kutongoza lafudhi ya kikenya,mambo hayo kina bishanga bashaija na nyingine ilikua inaitwa dhoruba ilikua inatisha mpaka wakaiondoa.Mzee flani anafufuka alafu anasema nakuja kama dhorubaaaaaa yani shule iko maporini kuwahi Namba nikawa naogopa nikiikumbuka hiyo muvi.kipindi hicho kwenye mpira kulikua na vichwa kama babayaro,babangida,Sunday olise,ucheokochuku,okocha,kanu,ndiefi,ronaldo de Lima anachambua Uwanja mzima,batistuta,otega,edgar Davis,zizu na wengine wengi.masumbwi Tyson k.o. za kutosha.na kwa matangazo ni lile la nipen NGUO nifue komoa na sabuni ya komoaaa ayeyeee komoaaa.jingine ni Mshindi sabuni yenye nguvu yenye kutakatisha kuliko zote mshindiiiii.pia kuna la gazeti letu mtanzania gazeti la habari kemukem habari za kitaifa habari za watoto na makala maalum kwa jamii yote.kuna chai bora kilele cha ubora chai bora ni majani ya tatepa iwe na maziwa isiwe na maziwa vyovyote vile utachangamka.la mwisho ni tufanye kazi kwa nguvu zote kazi kazi tujenge taifa letu baada ya kazi ni kuburudika ni wakati WA tusker.mpaka Leo ndio bia yangu
Daah kitambo sanaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Revola

Revola

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
1,166
2,000
Hili ndilo tangazo la christmass ambalo hata coca cola wenyewe wanakili walipitiliza ubunifu.................lina mzuka wa hali ya juu. Kama uliliona utotoni miaka ya 1996 basi unaweza tokwa na chozi maana linarejesha kumbukumbu nyingi sana za miaka ile wakati huo sikukuu ilikuwa ni raha sana tofauti na sasa.
Kaka hauna matangazo mengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom