Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

CTN wakat huo nakumbuka ilikuwa jumapili saa nane mchana ilikuwa wanaweka picha za kihind!!akna san deo,bab deo,salman khan nk
Duh umenikumbusha mbali sana kijana. Walikuwa wanaweka picha za kihindi na kiarabu. Full watu kuchinjana na ndio movies za Kina kuchi kuchi khotae za kihindi. Umenikumbusha mtangazaji wa taarifa wa DTV alikuwa Ephraim kibonde. Na sitasahau yule Rainfred Masako alivyo tangaza ajali ya Mv. Bukoba.
Ivi huyu mzee Rainfred Masako yupo wapi alikuwa mtangazaji wa ITV.
Kuna mtangazaji mwingine alikuwa DTV alikuwa anaitwa Godfrey Mgodo
 
Tulikuwa tukishindana kuguess nani atatangaza habari ITV, Ila nilimpenda Sauda kilumanga habari za kiinglish sijui yuko wapi now
Yaaaani huyo Dada Kama unapicha yake hebu niwekeee nimuone si alikuwa mweusi hivii
 
1474140415424.jpg
kuna hii pia...ilikua na jina lake ila nimelisahau...adi wahusika nilikua nimeweka majina ya kichwani enzi izo ila nimesahau yote
 
Kifuatacho ITV, yule dada muhindi ndo alikuwa anasema kifuatacho ITV na kutoa muhtasari kidogo kama ni tamthilia, nakumbuka tamthilia ya Acapulco, na moja ilikuwa kali sana nimesahau jina ila ina neno beach!
Angalia kwenye uzi juu nimegusia mkuu
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.
Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
Mkuu hujanitendea haki kumsahau rino lenz (sijui kama nimepatia kuandika jina ila ujumbe umefika)
 
Jumamosi itv walikuwa na hekaya za journey to the west a.k.a brother monkey sun wukong, zhu bajie nguruwe na master shifo hsuan tsan. Pia katuni za kina john quest, silver hawks na popeye the dreamer.

Nakumbuka pia tangazo la michael power na katili hekta dekta kama movie flani hivi ya kuitangaza bia ya guiness

Kule ctn na ndugu yake cen katuni network kila saa kumi jioni. Tangazo la tritel watu wamebeba bonge la simu.

Dtv tulikuwa tunaona ligi ya uingereza kila wiki mchambuzi dakta leakey stori nyingi. Pia kulikuwa na vitimbi vya mzee majuto, mwanachia, mangushi na gladys zipompapompa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom