Tukumbushane tuliowapokea mashujaa wa vita vya Kagera

Ukoo wangu wote walikuwa vitani asee.

Babu-alikuwa commanding officer kwenye moja ya unit iliyokuwa front.

Baba mkubwa-Alikuwa kwenye kikosi cha kusupply msosi kwa wapiganaji.

Baba mkubwa mwingine-Alikuwa rubani.

Baba mzazi-yeye alienda awamu ya pili kulinda doria baada ya uganda kuwa tayari imetekwa.

Baba mdogo-alikuwa kikosi cha mizinga.

Baba mdogo wa pili-alikuwa front kukabiliana na adui.

Ninachoshukuru Mungu hawa watu wote bado wako hai mpaka dakika hii.
Kwahiyo una mengi ya kuandika kuhusu vita hiyo. Je, umeshawahi kuandika au kumwaga madini hapa JF?
 
Vita ambayo wala haikua na sababu yeyote
Wazir mkuu mstaafu mzee Malecela wakati bifu likiendelea si mwal.JK akamtuma aende kwa Idd Amin akampe ujumbe wa Tanzania kuhusu msimamo wa TZ, wee alijua analiendea kaburi lake, maana Amin kichwa ilikuwa bangi.
 
Kwahiyo una mengi ya kuandika kuhusu vita hiyo. Je, umeshawahi kuandika au kumwaga madini hapa JF?
Kwenye ile kikosi Cha anga hakikufanikiwa sana. Vikosi vikivyo fanikiwa Sana nahisi Ni mizinga na wapiganaji .
 
Kwenye ile kikosi Cha anga hakikufanikiwa sana.vikosi vikivyo fanikiwa Sana nahisi Ni mizinga na wapiganaji .
Hivi kikosi cha anga si ndo walikuwa akina Robert Mboma?! Na kwa vita za Afrika nadhani vikosi vya anga haviwezi kuwa na efficient sana unless watu waamue kufanya uharibu wa kupiga mabomu miji na vijiji.
 
Sikumbuki mwaka vizuri Ila nilikuwa darasa la 4 Kati ya 78 au 79. Ilitangazwa kuwa Vita imeisha na MASHUJAA wetu wanarudi nyumbani.

Tulienda kuwapungia mkono stesheni wakati walipopita na treni nakumbuka tuliimba nyimbo za kizalendo za kumsifu Baba wa Taifa hili na kumkashifu Dikteta Idd Amini Dada. Ulikuwa ni uzalendo wa kwenye damu kabisa.

Tukio moja ambalo sitalisahau kuna Shujaa ( Mwanajeshi) alituona tuko kikundi watoto wa kike akatuuliza ' Nani mchumba wangu' wote tukajibu Mimi, Mimi akatupa biskuti. Biskuti zao zilikuwa za chumvi. Tulifurahi Sana maana tulikuwa tunaenda kishule hata watu binafsi walikuwa wanakuja.

Uzalendo huu natamani ungekuwepo leo. Karibuni mliobahatika kuwaenzi MASHUJAA WA Taifa hili.
Those soldier were heroes,
Sio wa sasa hv wanaoona ufahari kukamata Raia kummpa kipigo,mateso,na kumrekodi na kutupia clip mtandaoni,siku hizi jeshi limejaa mabishoo watupu,tunagombania nao madem kitaa,
Utoporo mtupu
 
vp huyu singi ako mdogo aliekuwa kwenye kikosi Cha mizinga,maana mm ndg yang alikuwa kikos Cha mizinga aise ,anasema miznga ikichanganya kuunguruma akili inakuwa sio yako tena,na nikikuwa namuona wakati mwngne Kama ana wenge hivi.
Yuko fresh kabisa hadi leo na anaendelea na mishe zake zingine za kimaisha, amestaafu kwa sasa akiwa na cheo cha luten kanali ingawa naona uvutaji wa fegi ndio umekuwa ulevi wake mkubwa.
 
Mimi nimesimuliwa kama wewe coz wakati vita inapiganwa sikuwa hata nimefikiriwa kuzaliwa mkuu.
Na ninachomaanisha ni hiyo kufahamu mengi kwa kusimuliwa kwa sababu hata kama ingekuwa umeshazaliwa bado usingeyafahamu ila kwa kusimuliwa!
 
Huo mwaka 78 nilikuwa na miezi kadhaa tangu nizaliwe, walivyopita na kuanza kunisemesha nikawachekii nikaona hawa wanazingua tu, hawana jipya nikakamatia vizuri na kuendelea kunyonya maziwa kwa mama kwa kasi ya 4G, kongole kwenu mashujaa....
 
Moja Kati ya vita za hovyo kabisa kupiganwa dunia. Kulikuwa hamna haja ya kuingiza majeshi yetu ndani ya uganda. Tulitakiwa kuwafurusha wanajeshi wa uganda waondoke ndani ya nchi yetu na tubaki kulinda mipaka.

Vita nyingine ya hivyo ni Kati ya Ethiopia na Eritria. Mwandishi nguli Ahamed Rajabu aliwahi kuifananisha hii vita na watu wawili wenye vipara wanaogombea kitana. Maana ardhi wanayogombea haifai kwa chochote.
Do you underestimate the motives that were behind the despicable dictator of the century!? Acha kabisa kilichofanyika kuliondoa nduli kilikuwa na manufaa kwa waganda wenyewe na eneo zima la Afrika Mashariki...
 
Mimi nimesimuliwa kama wewe coz wakati vita inapiganwa sikuwa hata nimefikiriwa kuzaliwa mkuu.
Nakumbuka Idd Amini alidai atapiga Mwanza halafu chai anakuja kunywa Dodoma. Basi tulielekezwa tuchimbe mahandaki, handaki lilikuwa na shepu ya L juu mnafukia majani ili adui asione ikafika siku ya rehesal king'ora kikapita wote tukajificha. Ndugu zangu anaombea VITA tumkatae Kwa nguvu zetu zote.
 
Wazaziii wazazi wetu eeh 2 mashujaa waliokufa walikufa kishujaa mashujaa waliorudi wamerudi kishujaa lengo letu wazazi ilikua moja kuilinda ardhi yetuu eeeh daah balaaa kabisaa
 
Do you underestimate the motives that were behind the despicable dictator of the century!? acha kabisa kilichofanyika kuliondoa nduli kilikuwa na manufaa kwa waganda wenyewe na eneo zima la afrika mashariki...
Jamaa alikuwa jeuri Sana yaani akiamka Tu anadai ziwa Victoria lote ni lake. Jamaa alikuwa chizi Nyerere angemchekea hata huyo Museveni asingeonja Ikulu.
 
Mgeni aje home afu aanze kuwaita mabinti zangu "wachumba wachumba" namfukuza arudi nyumbani kwake hata kama muda wa kupata usafiri umepita.

NB;Niko nje ya mada ndugu mtoa post ila ina relate kidogo na baadhi ya mistari ya post yake.
Hujui kitu. Neno mchumba, rafiki, babu au bibi hutumiwa na watu wazima kuwatambua watoto, a social interaction. Mtoto hitaji lake kubwa ni kupenda, kujaliwa.
 
bado wapo hai,japo wengi wao hatunao tena.ila jwtz katka kumbukumbu za siku hii ya mashujaa,ingefanya mpango wa kuwatambua kila wilaya nch zima,angalau wapewe nishani ya heshima,lakini siku za kumbukiz za siku ya mashujaa Basi wawe wanakutanishwa kwenye wilaya zao kwa pamoja,itawapa faraja Sana Hawa wazee wetu mashujaa.
Tenda wema wende zako, usingoje shukrani. Mwingereza bado anawaenzi wafrica walio isaidia katika vita vya pili. Tanzania hao mashujaa wa vita ya Kagera, leo ukiiuliza wizara ya ulinzi au MMJ, hata ilipo orodha ya waliopigana vita hiyo walio bado hai, hawajui.
 
Sikumbuki mwaka vizuri Ila nilikuwa darasa la 4 Kati ya 78 au 79. Ilitangazwa kuwa Vita imeisha na MASHUJAA wetu wanarudi nyumbani.

Tulienda kuwapungia mkono stesheni wakati walipopita na treni nakumbuka tuliimba nyimbo za kizalendo za kumsifu Baba wa Taifa hili na kumkashifu Dikteta Idd Amini Dada. Ulikuwa ni uzalendo wa kwenye damu kabisa.

Tukio moja ambalo sitalisahau kuna Shujaa ( Mwanajeshi) alituona tuko kikundi watoto wa kike akatuuliza ' Nani mchumba wangu' wote tukajibu Mimi, Mimi akatupa biskuti. Biskuti zao zilikuwa za chumvi. Tulifurahi Sana maana tulikuwa tunaenda kishule hata watu binafsi walikuwa wanakuja.

Uzalendo huu natamani ungekuwepo leo. Karibuni mliobahatika kuwaenzi MASHUJAA WA Taifa hili.
Dah! Una kumbukumbu nzuri sana! Yule Kamanda aliye wapungia mkono na kuwatania "nani mchumba wangu" na kuwagawia zile biskuti, ndiye mimi.

Nilishastaafu Jeshini kitambo! Kwa sasa nimejichokea huku Magamba Lushoto nalima tu ngogwe.

Yaani hapa nilipo natamani Mwalimu angekuwepo madarakani ili tukawang'oe tena Madikteta wote wa huu ukanda wa Afrika Mashariki. Kuanzia yule Mu7, PK, Salva Kiiir, na pia yule mpya aliyeanza kuota ndoto za kwenda huko 2025!!
 
Back
Top Bottom