Tukumbushane tuliowapokea mashujaa wa vita vya Kagera

Hujui kitu. Neno mchumba, rafiki, babu au bibi hutumiwa na watu wazima kuwatambua watoto, a social interaction. Mtoto hitaji lake kubwa ni kupenda, kujaliwa.
Kumuita mwanangu naona sahihi. Kwa kizazi hiki ambacho watoto wanajua vingi na ukamuita mchumba huoni ya kuwa unawahamisha kwenye reli.
Ukimuita mchumba ndo ataona anapendwa kuliko kuitwa mwanangu.??
 
Babangu alituambia kipindi cha vita waliokuwa wanalinda mipakani uapnde wa mara kule rorya walikuwa wanachinjiwa mifugo au waliwaruhusu tu kuchinja maana waliwapokea kama wafalme
 
Uzi wa wakongwe, anyway wakti huo nilikuwa darasa la tatu, kipindi hicho kulikuwa na wazalendo kikweli.
 
Dah! Una kumbukumbu nzuri sana! Yule Kamanda aliye wapungia mkono na kuwatania "nani mchumba wangu" na kuwagawia zile biskuti, ndiye mimi.

Nilishastaafu Jeshini kitambo! Kwa sasa nimejichokea huku Magamba Lushoto nalima tu ngogwe.

Yaani hapa nilipo natamani Mwalimu angekuwepo madarakani ili tukawang'oe tena Madikteta wote wa huu ukanda wa Afrika Mashariki. Kuanzia yule Mu7, PK, Salva Kiiir, na pia yule mpya aliyeanza kuota ndoto za kwenda huko 2025!!
Tulikuwa wazalendo kwelikweli wiki nzima tunapigigwa na Jua tukiwasubiri pale Stesheni ya Dodoma, unajua zamani na changamoto za mawasiliano walipofika ilikuwa nderemo na vifijo, ilikuwa fahari kubwa Sana kuonyesha heshima zetu kwao. Siku hizi kuna majinga machache yanavaa skafu halafu yanajiita mazalendo huku matendo yao ni ya kuyaonea huruma.
 
Sikumbuki mwaka vizuri Ila nilikuwa darasa la 4 Kati ya 78 au 79. Ilitangazwa kuwa Vita imeisha na MASHUJAA wetu wanarudi nyumbani.

Tulienda kuwapungia mkono stesheni wakati walipopita na treni nakumbuka tuliimba nyimbo za kizalendo za kumsifu Baba wa Taifa hili na kumkashifu Dikteta Idd Amini Dada. Ulikuwa ni uzalendo wa kwenye damu kabisa.

Tukio moja ambalo sitalisahau kuna Shujaa ( Mwanajeshi) alituona tuko kikundi watoto wa kike akatuuliza ' Nani mchumba wangu' wote tukajibu Mimi, Mimi akatupa biskuti. Biskuti zao zilikuwa za chumvi. Tulifurahi Sana maana tulikuwa tunaenda kishule hata watu binafsi walikuwa wanakuja.

Uzalendo huu natamani ungekuwepo leo. Karibuni mliobahatika kuwaenzi MASHUJAA WA Taifa hili.
Namkumbuka Sikamona na mpenzi wake Rusia.
 
Wanawake Mungu anawaona..

Nyie tangu utoto ni wapigaji tu. Sasa ona huyu alimdanganya shujaa kuwa ni mchumba wake.

Kapewa biskuti, alafu akala kona. Kachukuliwa na Baharia
Ayaaa yamekuwa haya tena. Jamani neno mchumba ni la kawaida wewe katika makuzi yako mzazi au MTU yoyote hajawahi kukutania kuwa utamuoa Fulani? au wenzetu mnaishi angani?.
 
Mkuu ungetaja tu hayo makabila yaliyokuwa yakilia ili kuweka sawa historian yetu


Alienda baba yangu huko, huwa anatupa story ilikuwa inapiga mizinga ya maadui mpaka baadhi ya wajeda wa kibongo wanalia kama watoto....

Akagusia wajeda hao walikuwa haswa makabila ya.........

Sitaki bifu wazeee huwa nacheka sana
 
Back
Top Bottom