Tukumbushane tuliowapokea mashujaa wa vita vya Kagera

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,410
8,393
Sikumbuki mwaka vizuri Ila nilikuwa darasa la 4 Kati ya 78 au 79. Ilitangazwa kuwa Vita imeisha na MASHUJAA wetu wanarudi nyumbani.

Tulienda kuwapungia mkono stesheni wakati walipopita na treni, nakumbuka tuliimba nyimbo za kizalendo za kumsifu Baba wa Taifa hili na kumkashifu Dikteta Idd Amini Dada. Ulikuwa ni uzalendo wa kwenye damu kabisa.

Tukio moja ambalo sitalisahau kuna Shujaa (Mwanajeshi) alituona tuko kikundi watoto wa kike akatuuliza 'Nani mchumba wangu' wote tukajibu Mimi, Mimi akatupa biskuti. Biskuti zao zilikuwa za chumvi. Tulifurahi Sana maana tulikuwa tunaenda kishule hata watu binafsi walikuwa wanakuja.

Uzalendo huu natamani ungekuwepo leo. Karibuni mliobahatika kuwaenzi MASHUJAA WA Taifa hili.
 
Kuna ndugu yangu kwa sasa ni marehemu alipigana ile Vita. Yeye alikuwa kwenye kikosi cha mizinga. Aise ile mizinga ilimuathiri sana. Cha ajabu baada ya Vita kuisha walirudi home, baadae aliugua sana TB. Kumbe madhara ya mizinga ndio yakaanza kujionyesha. Sijui kwanini serikali haikuwaangalia hawa mashujua kwa jicho la tatu.

RIP soldier Gaitano.
 
Kuna ndugu yangu kwa Sasa ni marehemu,alipigana ile Vita ,yeye alikuwa kwenye kikosi Cha mizinga,aise ile mizinga ilimuathili Sana,Cha ajabu baada ya Vita kuisha walirudi home, baadae aliugua Sana TB ,kumbe madhara ya mizinga ndo yakaanza kujionyesha.sijui kwa nn serikali haikuwa angalia Hawa mashujua kwa jicho la tatu.RIP soldier gaitano.
Amekufa kishujaa
 
Nilikuwa darasa la nne nakumbuka ilikuwa nne mji wa Mbeya ulirindima kwa sauti za ving'ora na honi za magari huku msururu mkubwa wa magari yaliyo wabeba mashujaa yakiongozwa na magari ya viongozi na ving'ora yalikuwa yanaingia town center yakitokea mafiat, ilikuwa ni siku ya kipekee iliyogusa hisia za watu wengi. Baada ya hapo nakumbuka tulikuwa tunaokota sufuria mbovu na kuzitoboa vishimo viwili pembeni na kuziweka kamba tukawa tunazivaa kuigiza helmet za kivita walizovaa mashujaa.
 
Mgeni aje home afu aanze kuwaita mabinti zangu "wachumba wachumba" namfukuza arudi nyumbani kwake hata kama muda wa kupata usafiri umepita.

NB; Niko nje ya mada ndugu mtoa post ila ina relate kidogo na baadhi ya mistari ya post yake.
 
Back
Top Bottom