Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Tukio lipi ulilowahi kulifanya ukiwa shuleni ambalo mpaka leo ukikumbuka unaona ni kituko usichoweza kukisahahu?
Mi nakumbuka kumtandika mwalimu fimbo.Alikuwa teacher mnoko sana lkn chapombe sana.Siku hiyo tukaambatisha wakati wa mbalamwezi akiwa kalewa chakali sana anatafuta njia ya kwenda kwake.
Enzi hizo walimu wa msingi wanakaa nyumba za shuleni.Basi tukawa kama wanne hivi,tukamtegea mwalimu kavuka korongo,tulimtandika bakora za mgongo na fimbo zinaitwa mdawi.
Mwalimu alikimbia sana akaanguka kwenye mtaro akavunjika mkono.Kesho yake shule alikuja na hangover na manundu.Mmoja wetu akawa hana koo,akajisifia kuwa sisi ndio tulimchapa teacher ili watu watusifie.Zikafika kwa mwenyekiti wa kijiji na mratibu kata.Tulikula fimbo za hatari sana na kuwaita wazazi juu.Sitaki kukumbuka hii siku.
Kituko cha pili ni kumuwekea dada mkuu kioo katikati ya miguu yake wakati wa kuhesabu namba asubuhi.Tukacheki ndani kumbe alikuwa kwenye zile siku zao.Sasa enzi hizo vijijini hizi "always" hazikuwepo,ni mwendo wa vitambaa na vinepi.Na kwa sbb ya elimu ndogo ya afya,unakuta msichana yupo siku zake lkn hajui.Basi pale tukashuhudia mambo makubwa...Kelele zikawa nyingi!!Nimeonaaa nimeonaaaaa Nimeonaaaaa!!
Dada Mkuu mbio kwa mwalimu wa nidhamu!!Ilikuwa balaa,tulikula fimbo sana za mgongo,walimu wanawake walitushambulia sana.Haya yalikuwa ni matukio yakukumbukwa enzi za shuleni.
Sekondari kulikuwa na jamaa mnoko sana,alifukuzisha watu wengi sana kwa tabia za umbea umbea.Siku tukapanga na yeye afukuzwe.Vikachukuliwa viatu vya jamaa vipyaa,zilikuwa ndula zimeandikwa "Kawasaki".
Kawasaki ikawekwa kwenye begi la jamaa chini.Halafu ikatangazwa kuwa kuna wizi umetokea,na kwa sbb ya umbea wa jamaa yeye ndio akapenyezewa hizo habari ili azitangaze na atengeneze modality ya kuvitafuta na kutoa taarifa kwa mwalimu wa nidhamu.
Ikawa mshikemshike bwenini,chumba kwa chumba na begi kwa begi.Na hapo mwalimu alishasema atakayepatikana navyo basi ni kufukuzwa shule.Asijue kuwa viatu vipo kwake,jamaa alikuwa mbelembele sana.
Mwisho wa siku begi lake kumwagwa chini,kawasaki ikaonekana...Watu wakataka kumgawana,na sbb ya umbea wake,kelele zilivuma sana na hatimaye jamaa aliondolewa shule.
Haya ni matukio ya shule,ambayo yanaweza kuwa yalifanyika sbb ya utoto au hali ya uanafunzi,lkn yataendela kubaki ktk kumbukumbu za maisha ya shule.
Je mdau wa JF...Una tukio lolote au kituko enzi za shule na huwa unakikumbuka sana kila ukifikiri enzi za maisha yako ya shule!??