TUKUMBUSHANE:- Nyimbo za harusini za makabila mbalimbali

Hii nayo ni kabla ya harusi
1>tatizo ni baba mkwe,mke amenibania.
Sipendwi na wangu wakwe,wote wamenichunia.
Wameamua nifyekwe,mbali kunifutilia.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
2>ndoa yenyewe ni fupi,tena yakimkataba.
Kosa langu lipo wapo wapi,miaka kumi si haba.
Mrefu siyo mfupi,haba na haba kibaba.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
3>ukweli inaniuma,ila siwezi kusema.
Nikisusa ni lawama,ningejitoa mapema.
Nimefeli hii ngoma,kweli sina cha kusema.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
4>mke huyu mke gani,hajafunzwa unyagoni.
Nimwoe nimweke ndani,maji yafike shingoni.
Bora niwache njiani,hata kama nahuzuni.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
5>bora ndoa niizime,harusi nihairishe.
Vyema mimi nikalime,koo nisihatarishe.
Matunda nikayachume,acha wanikaribishe.
Tatizo ni baba mkwe,kupenda posa nyingine.
Shairi=TATIZO NI BABA MKWE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
 
Ni segere jadumka sina ungoya, umekosea Kidogo hapo kwenye jadumka, halafu kuna ule mwingine usemao Nimdodoo mame wa ngw'ai ni mdodo aauaaauaa, wabwanga nnanao, wandee nnanao.......Siku hz zimeachwa kwaito ndio inatawala
Wazanzibari wanaimbaje kwenye harusi zao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom