Tukumbushane MATUKIO YA KUSIKITISHA yaliyotokea TZ 2011

Baadhi ya matukio ya kusikitisha kwangu binafsi ni;
  1. Zile picha za wabuge wanaolala bungeni na kisha kuongezewa posho
  2. Dhana ya gamba ilivyoonyesha wazi kwamba viongozi wa CCM hawana mipango endelevu hata ya miezi sita
  3. CHADEMA kwenda kumuona JK huku wakijua kwamba JK haaminiki hata iweje
  4. Malumbano yasiyo na tija (hasa lugha kali) kati ya Mh na kiongozi wa wafu radio
  5. Upuuzi wa waliosukuma gari la Jairo
  6. Mgao usio kwisha
  7. Dowans payment
  8. Kifo cha Dr. Mziray wa emergency department MNH
  9. Utetezi wa Pinda kuhusu kuuza "strategic" ardhi kwa wageni
  10. Vilio visivyo na maana vya baadhi ya viongozi
  11. Mv Spice Island sinking
  12. Malumbano ya PPF na ukandamizaji wa wanyonge
 
sitosahau siku ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuruMATUSI YALISIKIKA LIVE kwenye TBC 1. Kwakweli ni aibu ya karne
 
Kuadhimisha miaka ya uhuru ambao taifa lililopata uhuru likiwa limeshafariki.
 
Sintosahau kauli za JK
1. Sijui kwanini Tz ni maskini
2. Wanafunzi wanaopata mimba ni kiherehere chao
3. Simjui mmiliki wa Dowans
4. Mimi siwezi kujigeuza mvua nikanyesha nikajaza mabwawa ili umeme upatikane
5. Kubwa zaidi nikuibuliwa mafisadi wengi ndani ya ccm na Jk bila aibu aliwakumbatia bila kumwajibisha hata mmoja kama Jairo na wenzake.

mkuu umeisahau hii, '' kwakweli mnahoja nzuri lkn nisipo'sign wenzangu watanshangaa''
 
Mh Rais Dr W.Slaa aliibiwa kura 1st November 2011 na Usalama wa Taifa na kumfanya Jakaya Mrisho Kikwete kuwa rais wa Usalama wa taifa.
 
Sintausahau huu mwaka! Ni mwaka ambao viongozi wa nchi wameikataa historia na kulazimisha sherehe za uhuru kuwa ni za Tanzania bara na kupinga kwa nguvu zote kwamba sio uhuru wa Tanganyika!
 
MBEYA
>>Sinto sahau Mabom na risasi yaliyo pigwa na askari kwa wananchi
>>kitendo cha wananchi kuteka mkoa kwa masaa kadhaa kikamanda.
 
Sintosahau kamsemo ka Kainerugaba Msemakweli "MAFISADI WA ELIMU" hatimae baadh waliokuwa DR.Fulan waukwaa Udokita wa MAJOHO
 
mabomu ya gongo la mboto, kifo cha sheikh Yahaya,.kifo cha Gaddafi, kuachiwa huru kwa askari waliomuua Imran Kombe, lowassa kumpasulia ukweli jk kuhusu richmond, kuvuma kwa habari et mwisho wa dunia 21/5/11
 
Kwa nini tusikumbushane ya furaha? Kila tukikumbuka za kusikitisha tunazidi kuvuta nuksi tu...
 
Tanesco kukata umeme uwanja wa taifa siku mechi ya simba na yanga fainali,wimbo wa taifa kugeuzwa kuwa alaji
 
sita usahau mwezi Nov 2011 na hasa siku nilipompoteza Baba yangu mpendwa
 
kwangu ni hili la kufungia mwaka ambapo leo tumesafiri na basi la LUCKY STAR from mwanza toDar tulipofika nyamilama wilaya ya kwimba. gari lilipata break down hadi saa sita hakijaeleweka, nimeamua kujirudia home coz saa sita basi halijaondoka hata likiondoa litafika saa ngapi? siku ikaishia kiivo nikikumbuka huanga nalia
 
Back
Top Bottom