Tukumbushane mara ya kwanza kuona video/TV ilikuwa Mwaka gani

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wakuu Leo baada ya kuwasha TV na kukuta maadhimisho ya siku ya kifo cha baba wa taifa mwl J.K Nyerere basi nikakumbuka miaka 21 iliyopita ambayo ndo ilikua siku ya kwanza kuona video katika Yale mabanda umiza
Nakumbuka siku hiyo nlikua napita karibu na jengo la abiria wilaya flani ya mkoa wa Mtwara nikasikia bunduki zinapigwa ndani,bro akaniambia njoo tuingie tuangalie trela then tuendelee na safari yetu
Nakumbuka enzi zile muvi kama za Anorld shoziniga,Van dame,chuck Norris ,Bruce Lee na legendary wengine wa action muvi ndo zilibamba sana hiyo ni mwaka 1996

Mwaka 1999 wakati wa kifo cha baba wa taifa tulifuatilia matangazo ya TV kupitia kuchungulia dirishani kwa tajiri mmoja hivi yani TV ilikua nyumba moja moja enzi hizo

Ebu na wewe tukumbushe mara ya kwanza kuona TV/Video ilikua mwaka gani
e4396fb865793444880ac5b43ea28051.jpg
 
1994 magomen Kota ilikuwa hauingii kwa huyo baba bila ya kuoga na kuvaa nguo safi,na ni marukufu kukaa kwenye Kochi tulikuwa tunakaa chini katv nchi 14 tena black and white sauti kuongeza mpaka uende kwenye TV na uzungushe hakuna remote kipindi iko...
 
1978 Nairobi nchini kenya nilipobahatika kwenda kwa Shangazi kumtembelea ndiyo nikaona watu wanacheza kwenye tv
 
Pumzika kwa Amani mzee Shemeji shemeji,.mtu wa kwanza kuonyesha video kwa pesa mkoa wa morogoro.
 
Pumzika kwa Amani mzee Shemeji shemeji,.mtu wa kwanza kuonyesha video kwa pesa mkoa wa morogoro.
 
kwa mara yakwanza kuona tiv ilikuwa nisiku ya mazishi ya baba wataifa (nyerere)...l
 
Back
Top Bottom