Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
UKIFANYA MEMA NA MUNGU ATAKULIPA MEMA
Mtoto alimuweka mama yake kwenye kituo cha kulelea wazee, na alikuwa akimtembelea kila baada ya muda.Siku moja akapigiwa simu kutoka kituoni kwamba mama yake yuko katika hali mbaya amezidiwa taabani akamkimbilia mama yake haraka kituoni ili amwone mama yake nini kilichomsibu.
Alipofika akamuuliza mama yake. Unataka nikufanyie nini mama yangu
Yule mama kwa utaratibu akasema. Vema, nataka uweke mapangaboi (Feni) kwenye nyumba hii ya wazee kwani hamna feni, pia uweke majokofu ya chakula safi.. mara nyingi nimelala bila ya kula
Mtoto akamjibu mama yake kwa mshituko. Sasa ndiyo unataka haya hali ya kuwa unatolewa roho! kwa nini hukulalamika kabla!
Mama akajibu kwa huzuni. Ndiyo Mwanangu, nimejizoesha joto na njaa lakini nakuogopea wewe hutazoea (joto na njaa) pindi watoto wako watakapokuleta hapa utakapozeeka
Subhana Allah! Nani kama mama
UKITENDA UBAYA UTALIPWA KWA UBAYA WAKO ULIOTENDA
TUWATENDEE WAZAZI WETU WEMA MUNGU ATUJAALIE TUWE WEMA KWA WAZAZI WETU SEMA AMIN.