Tukumbushane: Hivi kwanini Nyerere alikataa J. S. Malecela asigombee urais kupitia CCM

Pamoja na John Samwel Malecela kuwa mwanasiasa mwenye nguvu ndani ya chama cha Mapinduzi CCM na Serikalini lakini juhudi zake za kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea urais ziligonga mwamba kwa vipindi vyote viwili vya 1995 na 2005.

Sababu gani zilizofanya ashindwe:

Mbio za Malecela 1995

Ingawa Malecela alikuwa ni mgombea aliyekubalika kati ya wagombea wengine wa CCM lakini Baba wa Taifa JK Nyerere hakufurahishwa na kitendo cha Waziri Mkuu wakati huo Mh. Malecela kuruhusu hoja ya Serikali tatu iletwe bungeni, vile vile hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujihusisha na Zanzibar kujiunga na OIC. Kwa hiyo kitendo hicho kilimkera sana Mwalimu hadi akafikia kumtaja Malecela kuwa ni muhuni na mroho wa madaraka. Nanukuu mwandishi mmoja,

"Nyerere saw him as someone who was driven by personal ambition in his quest for the presidency and warned CCM leadership that he would not even attend the party congress if Malecela was on the short list of possible candidates".

Vile vile kulikuwa na hear say kwamba Malecela alikuwa groomed na nchi moja ya kiarabu ili kufanikisha mbio zake za urais na ilisemekana kuwa ilibidi abadili jina(dini) na kujiita Jumanne Samwel Malecela. Kutokana na msimamo wa Mwalimu jina lake halikupendekezwa na Mkapa akaibuka kidedea.

Mbio za Malecela 2005

Baada ya kutofanikiwa lengo lake 1995 Malecela hakukata tamaa alionekana kutokuwa karibu sana na Mwalimu Nyerere na hasira hizo zilienda mbali na kusababisha hadi kwa familia yake imchukie Mwalimu na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM, kiasi kwamba katika kinyang'anyiro cha mwaka 2005 jina lake halikuvuka hata raundi ya kwanza wakati Mh. Kikwete alipoibuka kidedea. Inasemekana kinyongo cha Malecela kukosa urais kwa safari mbili kiliendelea hadi kusababisha makundi ndani ya chama.

Kwa vile wakati ule alikuwa bado na cheo cha Makamu Mwenyekiti rais Kikwete kwa kuona hali ilivyo ndani ya chama ikabidi atafute mbinu ya kumtoa pale, akasema anataka asaidiwe kwenye kiti kile cha M/M/kiti na damu changa lakini matokeo yake mwaka 2007 akateuliwa Pius Msekwa kiasi kwamba watu wakajiuliza damu changa iko wapi. Kwa vile ilionekana Malecela bado ana nguvu ndani ya chama uongozi wa juu wa chama katika kumpunguza nguvu zaidi ukafanya juu chini ili Malecela asishinde kwenye kura za maoni za ubunge jimbo la Mtera.

Mimi binafsi ingawa sikuwa kwenye michakato hii toka 1995 enzi za Mwalimu hadi 2005 enzi za Mkapa/Kikwete lakini nafarijika kwamba huyu Mzee hakupata kutuongoza kwenye nafasi ya urais kwa vile kama alivyosema Mwalimu ni Mbinafsi,Muhuni, roho isiyo na utu'You Can Go to Hell' alitaka kutuingiza OIC, kama si Nyerere kuliona hilo mapema tungejuta.

I say again thank God he is/was not a President of Tanzania.
 
Ndugu Luteni,

Respect!

Naomba niulize maswali kadhaa:
>Why Malechela ?
>Why now ?
>Je huu ni mwendelezo wa Mzee MM wa kumleta Mwalimu ne wazee wengine kwenye mwangaza ?
>Je haya masula yantusaidia vipi kujikomboa kwenye majanga lukuki yanayotuangamiza ?
>Je sii haki kumwacha huyu mzee apone in peace ?
>Je lile suala kuu. suala la kufa au kupona, suala la katiba mpya linauhusiano gani na haya ?
>Je huoni ni muhimu kwa nyakati hizi kupeleka nguvu zetu, fikra zetu na raslimali zetu kudai katiba ya watu ?
>Je tutafanikisha nini kwa kumnanga Mzee Malechela ?

Maswali ni mengi tuu, ila kwa sasa ni hayo tuu mkuu !
 
Jibu ni rahisi sana yeye ni public figure kwa hiyo sambamba na mambo mengine tunayojadili lazima tujue wazee wetu waliongozaje kama walikuwa wamoja tujue kama walikuwa hawaelewani kwanini ili itusaidie kwenye uongozi wa nyakati zetu ndio maana kuna somo la historia lazima tujue tulikotoka.
 
Pamoja na John Samwel Malecela kuwa mwanasiasa mwenye nguvu ndani ya chama cha Mapinduzi CCM na Serikalini lakini juhudi zake za kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea urais ziligonga mwamba kwa vipindi vyote viwili vya 1995 na 2005.

Sababu gani zilizofanya ashindwe:

Mbio za Malecela 1995

Ingawa Malecela alikuwa ni mgombea aliyekubalika kati ya wagombea wengine wa CCM lakini Baba wa Taifa JK Nyerere hakufurahishwa na kitendo cha Waziri Mkuu wakati huo Mh. Malecela kuruhusu hoja ya Serikali tatu iletwe bungeni, vile vile hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujihusisha na Zanzibar kujiunga na OIC. Kwa hiyo kitendo hicho kilimkera sana Mwalimu hadi akafikia kumtaja Malecela kuwa ni muhuni na mroho wa madaraka. Nanukuu mwandishi mmoja,

“Nyerere saw him as someone who was driven by personal ambition in his quest for the presidency and warned CCM leadership that he would not even attend the party congress if Malecela was on the short list of possible candidates”.

Vile vile kulikuwa na hear say kwamba Malecela alikuwa groomed na nchi moja ya kiarabu ili kufanikisha mbio zake za urais na ilisemekana kuwa ilibidi abadili jina(dini) na kujiita Jumanne Samwel Malecela. Kutokana na msimamo wa Mwalimu jina lake halikupendekezwa na Mkapa akaibuka kidedea.

Mbio za Malecela 2005

Baada ya kutofanikiwa lengo lake 1995 Malecela hakukata tamaa alionekana kutokuwa karibu sana na Mwalimu Nyerere na hasira hizo zilienda mbali na kusababisha hadi kwa familia yake imchukie Mwalimu na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM, kiasi kwamba katika kinyang’anyiro cha mwaka 2005 jina lake halikuvuka hata raundi ya kwanza wakati Mh. Kikwete alipoibuka kidedea. Inasemekana kinyongo cha Malecela kukosa urais kwa safari mbili kiliendelea hadi kusababisha makundi ndani ya chama.

Kwa vile wakati ule alikuwa bado na cheo cha Makamu Mwenyekiti rais Kikwete kwa kuona hali ilivyo ndani ya chama ikabidi atafute mbinu ya kumtoa pale, akasema anataka asaidiwe kwenye kiti kile cha M/M/kiti na damu changa lakini matokeo yake mwaka 2007 akateuliwa Pius Msekwa kiasi kwamba watu wakajiuliza damu changa iko wapi. Kwa vile ilionekana Malecela bado ana nguvu ndani ya chama uongozi wa juu wa chama katika kumpunguza nguvu zaidi ukafanya juu chini ili Malecela asishinde kwenye kura za maoni za ubunge jimbo la Mtera.

Mimi binafsi ingawa sikuwa kwenye michakato hii toka 1995 enzi za Mwalimu hadi 2005 enzi za Mkapa/Kikwete lakini nafarijika kwamba huyu Mzee hakupata kutuongoza kwenye nafasi ya urais kwa vile kama alivyosema Mwalimu ni Mbinafsi,Muhuni, roho isiyo na utu’You Can Go to Hell’ alitaka kutuingiza OIC, kama si Nyerere kuliona hilo mapema tungejuta.

I say again thank God he is/was not a President of Tanzania.
Luteni umemaliza kabisa

Huyu mzee kwa story zake ninazozisikia nikilinganisha na dharau za watoto wake nasema kama angekuwa rais ningehama nchi hata Sudani ningeenda kuishi hadi nisikie hayupo madarakani. Najiuliza nyodo za watoto wake zingekuwaje kama angekuwa raisi hivi tu hana cheo chochote lakini wanavyoita watu mbuzi is beyond humanity thank God a billion for not allowing this man to be our president.
 
Mungu aliiepusha na balaa TZ kwani Malecela kwa hulka zake tu angetutesa sana
Nafikiri angetupiga mnada wote bora huyu anayeuza dhahabu kuliko ambaye angetuuza wazima, Nyerere namwinulia mikono hata Mkapa aliliona hilo he had no option akatupa Kikwete Mkapa alichangua kati ya mbegu zilizooza akapata angalau tuliye naye kuliko Malecela.
 
Ndugu Luteni,

Respect!

Naomba niulize maswali kadhaa:
>Why Malechela ?
>Why now ?

>Je huu ni mwendelezo wa Mzee MM wa kumleta Mwalimu ne wazee wengine kwenye mwangaza ?
>Je haya masula yantusaidia vipi kujikomboa kwenye majanga lukuki yanayotuangamiza ?
>Je sii haki kumwacha huyu mzee apone in peace ?
>Je lile suala kuu. suala la kufa au kupona, suala la katiba mpya linauhusiano gani na haya ?
>Je huoni ni muhimu kwa nyakati hizi kupeleka nguvu zetu, fikra zetu na raslimali zetu kudai katiba ya watu ?
>Je tutafanikisha nini kwa kumnanga Mzee Malechela ?

Maswali ni mengi tuu, ila kwa sasa ni hayo tuu mkuu !

Me nataka pia kumjua mzee mwenyewe ili nijue huyu mtoto wake
karithi kwake au vipi,....

Yaani jana katoa povu kwenye thread ya Dr.Slaa hadi imefungwa sijui alikua
kavuja ganja au vipi,....sikudhania ni mtu hovyo kiasi hiko,...labda karithi,...
kabla hatuja mlaumu mzee,ni vizuri tumjue kwanza vyema
 
Luteni umemaliza kabisa

Huyu mzee kwa story zake ninazozisikia nikilinganisha na dharau za watoto wake nasema kama angekuwa rais ningehama nchi hata Sudani ningeenda kuishi hadi nisikie hayupo madarakani. Najiuliza nyodo za watoto wake zingekuwaje kama angekuwa raisi hivi tu hana cheo chochote lakini wanavyoita watu mbuzi is beyond humanity thank God a billion for not allowing this man to be our president.
Mngemkoma @ New York, nadhani lazima angekuwa na yeye serikalini, kama mkilalamika tu angewaambia shida ya Watanzani mna vichwa vya mbuzi.
Ndio maana mimi nimeanza kumtaarifu mapema asahau kuhusu ubunge nchi hii, yeye aongeze bidii tu kwenye kubeba box huko NYC
 
Me nataka pia kumjua mzee mwenyewe ili nijue huyu mtoto wake
karithi kwake au vipi,....

Yaani jana katoa povu kwenye thread ya Dr.Slaa hadi imefungwa sijui alikua
kavuja ganja au vipi,....sikudhania ni mtu hovyo kiasi hiko,...labda karithi,...
kabla hatuja mlaumu mzee,ni vizuri tumjue kwanza vyema
@New York, lazima atakuwa anakula msuba tu, kwa kazi za ubaharia ile kitu ndio sigara yao kule deep sea.
 
Baba aliona mbali akamtolea mbali maana ni king'ang'anizi wa madaraka, JK naye hivi kamtosa au wananchi wamemtosa?
 
Mngemkoma @ New York, nadhani lazima angekuwa na yeye serikalini, kama mkilalamika tu angewaambia shida ya Watanzani mna vichwa vya mbuzi.
Ndio maana mimi nimeanza kumtaarifu mapema asahau kuhusu ubunge nchi hii, yeye aongeze bidii tu kwenye kubeba box huko NYC
Kwa hulka yake lazima angekuwa IGP ili mmkome wenye sura za mbuzi. Nafikiri watu wa Mtera walikuwa wamechoka sana na Mzee ila walikuwa hawana jinsi kila wakifanya jina la Cigwi linarudi mwisho wakaamua liwalo na liwe wakampa mbuge jina limenitoka ingawa na yeye ni bomu sijui kama atarudi.
 
Kikwete naye alishamchoka kama angetaka arudi angemrudisha lakini lilishakuwa zigo lile akaona isiwe tabu ni kujinyamazia.
 
Huyo ni mtoto wake William anayewaita watu mbuzi labda inawezekana wanashauriana na mzee kwa vile mzee yuko kwa @NYK sasa.

Hivi nyinyi mmegeza hili jukwaa kuwa sehemu ya vichekesho? Duh kweli ujana maji ya moto, ehee eti wanashauriana na Mzee, nyie kiboko kweli!
 
Kwa hulka yake lazima angekuwa IGP ili mmkome wenye sura za mbuzi. Nafikiri watu wa Mtera walikuwa wamechoka sana na Mzee ila walikuwa hawana jinsi kila wakifanya jina la Cigwi linarudi mwisho wakaamua liwalo na liwe wakampa mbuge jina limenitoka ingawa na yeye ni bomu sijui kama atarudi.
Lile jimbo la Mtera ni kama lina laana maana mbunge wao wa sasa anaitwa Livingstone kama sikosei huyu inaonekana yeye ndio anakula msuba ule wa kutoka Malawi maana pale kichwani ndio empty kabisa, au unaweza kumuita Half glass empty.
 
Ujinga wa waTZ ndiyo mtaji wa walanchi, kipindi kile Nyerere hakumkatalia Ngw'inyamisi pekee yake bali pia alimkatalia hata mzee wa Richmond na huyu daktari wetu wa siasa Kikwete. Wa kwanza aliuza nchi na akaambiwa ajitoe ili asaidiwe hela ya watu irudi, hawa wawili wengine waliambia muda wao bado sana, wenzetu wakatafsiri kuwa ngoja akifa tu huyu mzee tunaingia. hali ndiyo hii tunayoiona na tutaendelea kuteseka hadi tuseme tuiii!!! Tumewapa ulaji na hata wao wamesema sasa zamu yao wanatesa, tutakoma tukomae pia. Labda maumivu yakizidi tutaweza kuamua njia mbadala
 
Mnakumbuka alipokuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi; kulikuwa na shida ya Usafiri wa Reli kwenda Mwanza through Dodoma akaseme wasafiri wote "THEY CAN GO 2 HELL" na hakuomba Msamaha... baada ya Uchaguzi Nyerere akamyima Uwaziri... Matatizo ni Anaropoka ropoka kweli lakini nasikia ana akili ni alikuwa Mshauri Mzuri wa JK just asiongee mwenyewe ni Upupu... we can say PUMBA
 
Wasalaam JF,

Tumekuwa tukiamini na kuendelea kuamini na ukweli ndivyo ulivyo kuwa muasisi wa taifa hili la Tanzania, Baba wa Taifa Mwl J. K Nyerere ndiye aliyepata kuwa rais muadilifu na mwenye uchungu na umaskini wa watz wanyonge hivyo alipewa heshima zote ndani ya chama na Serikali.

Nimekuwa nikijiuliza sana kwanini Nyerere alimkataa Malecela asigombee nafasi ya kuwania Urais kupitia chama cha mapinduzi,ccm? mpaka alitishia kurudisha kadi yake ya uanachama endapo Malecela asingejitoa.

Anayefahamu atujuze
Malecela yupi?? Huyu huyu Jumanne?
 
Mngemkoma @ New York, nadhani lazima angekuwa na yeye serikalini, kama mkilalamika tu angewaambia shida ya Watanzani mna vichwa vya mbuzi.
Ndio maana mimi nimeanza kumtaarifu mapema asahau kuhusu ubunge nchi hii, yeye aongeze bidii tu kwenye kubeba box huko NYC
Sijawahi kuona jitu bogus duniani kama @NYC, USA
 
Hujui hali yake ni tete? Akivuta tu watu tayari tunakuwa hewan na masong yetu!

Nyimbo za Kapteni Komba zipo ni kiasi cha kutoa jina la Nyerere unaweka la Mzee Malece.

Usiumize kichwa kumtungia nyimbo huyu bwana
 
Back
Top Bottom