Anytime buddyN.B Thanks Mods
Shabaan Dede alihamia Sikinde akitokea Juwata Msondo ngoma ambapo hadithi ni kuwa alinyang'anywa unifomu wakiwa wanapiga mziki.
Mchongoma
) kuwa kama wao ni Ogelea Piga Mbizi basi yeye ni chunusi na wasithubutu kuchezea majini tena. Nyimbo zake zilikuwa heavy sana kuliko za hao Marquiz. Hebu chukua nafasi usikilize wimbo kama Marashi ya Pemba au Kesi ya Kanga ndipo ujue kuwa Freddie(RIP) kweli alikuwa Supreme
WildCard,
Kuna Empire kubwa sana East and Central Africa, inaitwa Bahima kama sikukosea ambayo ni shina ya makabila kadhaa yaliyoko Rwanda, Congo, Burundi, Tanzania, Uganda mpaka Kenya.
Katika ugomvi wa sasa kati ya Museveni na Kagame, chimbuko lake ni hilo la wao wawili kutoka shina moja na ndio maana Museveni anautaka sana ukuu wa EAC!
Sasa kabila la Nyerere Zanaki, inasemekana ni Bahima Empire.
Kwikwikwiiiiiii.....Ndivyo Tulivyo!!!
Wengine tulikuwa tunaenda pale posta ya zamani kuangalia meli......
1. Unajua Tanzania, pamoja na siasa zetu enzi zile, lakini bado tulikuwa na nafasi ya ku-socialize hasa kwenye ma-Disco na muziki wa Dance, kwenye hili ni lazima tuwe fair kuwa Mwalimu hakuwa na tatizo kabisaa.
2. Ni kweli kwamba ex- DJ Gerard, au kama alivyokuwa akifahamika kwa jina la "Jerry Kotto", alitokea kuwa mmoja wa the best DJs mjini Dar, na ni kweli kwamba alikuwa na matatizo ya kusoma, lakini Jerry alikuwa na tabia moja nayo ni akipata Album au Tape hukaa chini na kuisikiliza mwanzo mpaka mwisho, akisikia ngoma anayoamini kuwa ni safi basi husimamisha na kuweka alama kwanza kwenye Tape/Album na pia kwenye namba ya ile song, sasa akingia kupiga Disco huzikumbuka nyimbo zote zilipo na ni zipi, tena bila ya tatizo.
3. Kwa kadri ninavyokumbuka tumewahi kuwa na Ma-DJ waliokuwa waburudishaji na wakali, kwa sababu pamoja na kwamba wao yaani ma-DJ walikuwa sio wapigaji hasa wa zile nyimbo, lakini siku zote mchele ni ule ule, ila mapishi ndio hubadili matokeo, hata ma-DJ nao ilikuwa ni hivyo hivyo, kwa kweli ningeomba kuwakumbuka tena kwa nafasi zao, wale wote yaani ma-DJ waliowahi kutuburudisha mjini Dar kama ninavyowakumbuka na pia msaada unakubalika iwapo kuna niliowasahau au kuwaweka kwenye nafasi wasizofaa:-
1. DJ Justin Kusaga - Clouds (Morogoro).
2. DJ Kali Kali (Kalikawe) - YMCA/Mbowe.
3. DJ Ebbo Night Woo Jack! (Bob Rich Mazula) - Msasani Beach.
4. DJ Chris Phaby "The Lover" - Mbowe/Margott.
5. DJ Choggy Sly (Choggo Salum) & DJ JPP (John Peter Pantalakis) - Msasani Beach/Rungwe Beach
6. DJ Roma Pop Juice (RIP) - Mwanayamala.
7. DJ Jerry Kotto (Gerard) - Mbowe RSVP Club.
8. DJ Nigger Jay - YMCA.
9. DJ DC Washington (RIP) - Rungwe Beach.
10. DJ Lucas
11. DJ Tito Jackosn (Tito Kalumanga) - Rungwe Beach.
12. DJ John Bure
13. DJ Joe Kusaga (Joseph Kusaga) & DJ Stewart (Sterwart Chiduo) - Clouds.
14. DJ Kim (Kim) - Rungwe Beach.
15. DJ Kessy (Kessi) - Blue Sky Disco.
16. DJ Eddy - Magomeni.
17. DJ Super Deo (Deo) - YMCA/Margott.
4. Kwa upande wa muziki wa Dance, pia tilkuwa na bendi za wazawa na wageni, hasa kutoka Zaire na wao pia kulingana na nafasi zao kimuziki as I remmember, na time pia lakini pia msaaada unakubalika:-
1. End of The 60s:-
1. Orch. Morogoro Jazz - Mbaraka Mwinshehe (RIP).
2. Orch. Cuban Marimba - Salum Abdallah (RIP).
3. Orch. Nova Success - Baba Gaston (Nairobi).
4. Orch. Nuta Jazz - Muhidini Gurumo (Ilala - Msondo Ngoma).
5. Orch. Tabora Jazz - Wema Abdalalh/Shem Karenga (Tabora).
6. Orch. Western Jazz - Wema Abdallah (Sikukuu street Kariakoo, Dar).
7. Orch. Dar Jazz - Dar.
8. Orch. Unyanyembe Jazz - (Nyanyembe Tabora.)
9. Orch. Kilwa Jazz - Ahmed Kipande/Juma Mrisho (Kilwa).
10. Orch. Police Jazz - Dar.
11. Orch. Atomic Jazz - John Kijiko (Tanga).
12. Orch. Kilombero Jazz - (Kiwanda cha Sukari Kilombero).
13. Orch. Butiama Jazz - Ifakara.
14. Orch. Boma Liwanza - (Zaire/DSM).
15. Orch. Banangenge - Fataki Masumbuko Ya Dunia (Zaire/DSM).
2. In the 70s. to 80s:-
1. Orch. Super Volcano - Mbaraka Mwinshehe (Morogoro).
2. Orch. TK Lumpopo - Juma kilaza (Morogoro).
3. Orch. Afro 70 - Patric Balisidya (DSM).
4. Orch. Urafiki Jazz - Juma Mrisho (DSM).
5. Orch. Nuta Jazz - Muhidini Gurumo (DSM).
6. Orch. Marquiz du Zaire - Chinyama chiyanzi (Zaire/DSM).
7. Orch. Vijana Jazz - Andoro/Maneti (DSM).
8. Orch. Safari Trippers - Marijani Rajabu (DSM).
9. Orch. Mwenge Jazz - George Mpupua (JWTZ- DSM).
10. Orch. JKT Kimbunga - Mzee Zakaria (DSM).
11. Orch. Kimuli muli - Zahiri Zoro (JKT Mafinga/DSM)
12. Orch. Simba Wa Nyika - Wilson & George Peter (Arusha/Nairobi).
14. Orch. Dar International - Abel Baltazari/Marijani Rajabu (DSM).
15. Orch. Police Jazz - Moshi William (DSM).
16. Orch. BarKeys - George Mhando (DSM).
17. Orch. Sola TV - (Temeke - DSM).
18. Orch. Makassy - Mzee Makassy (Zaire/DSM)
19. Orch. Nkashama Nkoi - Ndala Kasheba (RIP) (Zaire/DSM).
20. Orch. Matimila - Remmy Ongalla (Songea/DSM).
21. Orch. Sunburst - Kassim Magati (DSM).
22. Orch. Tanzanite - Nembo (DSM).
23. Orch. Toma Toma - Thomas (DSM).
24. Orch. Mpakani Kyauri Voice - Mzee Khatibu Itei Tei (DSM).
25. Orch. Mlimani Park - Abel Baltazari/Gurumo (DSM).
26. Orch. Doble O - King Kiki (Zaire/DSM).
27. Orch Safari Sound - Mbombo wa Mbombo-Ka/King Kiki/Ndala Kasheba (Zaire/DSM).
28. Orch. Mk Group - Kossongo Mpinda/shem Karenga (DSM).
Huenda kuna niliowaacha, lakini ninaamini kuwa ma-DJ tulionao sasa na bendi za muziki, ni kuanzia in 90s hadi leo ni almost wale wale na bendi ni zile zile ingawa cha kusikitisha sana ni kwamba kama ni bendi zilizopo leo labda hazizidi nne, zingine zote zilikufa kifo cha mende, lakini ni vyema kukumbuka kuwa katika enzi zile za 70s, 80, na mwanzoni mwa 90s pamoja na msiha kuwa magumu kidogo siku zote tulikuwa na burudani kabambe ambazo some of us zilitusaidia sana kuendelea kuyakabili maisha, knowing kwamba kuna weeek end kwenda kula mangoma na kuku za kibongo bongo.
Heshima Mbele Wakuu.
enzi za raha nje ya mki ikifika jioni magari ya bendi yanapita ,,,basi la sikinde linapeleka watu DDC MLIMANI PARK...........OSS WANASOMBA WATU HADI KIMARA RESORT.....JUWATA AMANA KAMA KAWAIDA....WATOTO WA MARQUEE PALE PALE LANGATA SOCIAL HALL.......RAHA TU HADI ASUBUHI...
,..BAADAYE DR KHALID ALIKUJA KUIGA HII STAILI YA KUSOMBA WATU WAKALE RAHA MAKONDEKO [PEPONI]AKAFILISIKA....I DONT KNOW WHERE HE WENT WRONG.....
HAPO WAZEE HAMJAWAKUMBUKA......MAKASSY ORIGINAL;...NA MJOMBA WAKE ..DR REMMY ONGALA...[ACHA BWANA HUYU BWANA NAMPENDA SANA ..KAMA BOB MARLEY KWA TUNGO ZAKE..SIO NYIMBO ZA LEO KUTAJANA MAJINA BILA UJUMBE]]..
]
nawakumbuka pia familia ya akina kapinga (george, amato na abraham) ambao wote walikuwa katika timu ya waanzilishi wa bendi ya the barkeys.
Mkuu Kishoka,
Heshima mbele, uliyosenma ni sawa kabisa lakini kidogo tu unajua nilifikiri alitoka Msondo Ngoma na kuingia Bima Lee ndio akaenda Sikinde, ambako wimbo wake wa kwanza akiwa Bima Lee ulikuwa "Samaki Baharini Huishi Vipi" akaanzisha na mtindo mpya wa "Magneti Tingisha", hakukaa sana akenda Sikinde, na baadaye kurudi tena Msondo Ngoma,
Anyways ni zamani sana kwa hiyo ninaweza kuwa nimepitiwa mkuu, ila respect kwa kipande chako cha historia.
Ngoja niwarudishe kwenye mpira wa miaka ya sabini tena, kwani wakati huo tulikuwa na kandanada la hali ya juu sana haijapata kutokea. Inawezakana baadhi ya picha zimeshawekwa hapa ila nadhani hakuna tatizo kama nitazirudia, kwani wahenga walitufundisha kuwa jambao jema linastahili kurudiwa tena na tena.
Pan African
Najua una rekodi kubwa sana ya mambo ya wakati huo, ila nakuomba tena upitie kumbukumbu zako vizuri na kwa makini. Ukweli ni kuwa mtindo alioanza nao Marehemu Maneti pale Vijana Jazz ulikuwa ni Koka Koka. Wimbo wa Kamata Sukuma ulitolewa kipindi kimoja na Niliruka Ukuta, na ulipigwa pia katika mtindo wa Koka Koka, ila kutokana na umaarufu ulioambatana na wimbo ule wa Kamata Sukuma, Maneti akapromote wimbo wa "Kamata Sukuma" kuwa mtindo uliorithi Koka Koka mwaka 1976 hivi, na ulidumu muda mfupi sana kabla hajaanzisha Heka Heka.
Kumbukumbu yangu kuhusu wimbo wa "Niliruka Ukuta" ambamo sauti ya Marehemu Maneti ilikuwa haitofautiani na ile ya Marahemu Mbaraka inakuja vizuri sana. Vile vile chini ya mtindo wa Koka Koka, Maneti alipiga wimbo wa "Zuhura Ninaondoka" ambao binafsi nilikuwa nauhusisha sana na mpenzi wangu wa wakati huo Marehemu Zuhura (RIP). Nilikuwa nina T-Shirt moja ya Sunflag iliyokuwa na picha ya kichwa cha tembo kifuani; mgongoni nikaandika pale maneno matatu kwa style ya aina yake: maneno hayo yalikuwa ni Masika, Sokomoko na Koka Koka, ambayo ilikuwa mitindo ya muziki niliyokuwa naizimia sana wakati ule. Marafiki zangu wa wakati huo wa ujingani wakisoma post hii watakumbuka sana ninayosema. Wakati Maneti anatoa wimbo wa "Niliruka Ukuta," Mbaraka naye alitoa wimbo wa "Mshenga" ambapo Marijani naye alikuwa ametoa wimbo uliokuwa unasema "Wapangaji mnawaacha watoto wenu wanavunjavunja milango na madirisha ndani ya nyumba yangu, hivyo ni afadhali muondoke kwani mnaleta sokomoko ndani ya nyumba yangu": jina halisi la wimbo huu silikumbuki tena. Nyimbo hizi zilikuwa kiboko sana wakati huo ndiyo maana kwangu mimi muziki ukawa ni Masika, Koka Koka na Sokomoko.
Kuna watu wengine wanaweza pia kuthibitisha hili. Hebu soma hapa:
Marehemu Maneti alipochukua uongozi wa bendi ya Vijana Jazz alianza nao na mtindo wa Kokakoka. Vibao maarufu vya mwanzo mwanzo vya bendi hiyo vilikuwa "Nimeruka Ukuta" uliofahamika na wengi, "Sabina" na Magdalena". Kwenye wimbo wa Sabina alimuomba mpenzi wake Sabina arudi kwani siku nyingi zilikuwa zimepita tangu aondoke na kwenye wimbo "Magdalena" alikuwa analalamika kuzuiwa na wazazi wake kumuoa Magdalena kwa sababu alikuwa na ulemavu wa jicho wakati yeye alikuwa akimpenda sana.
Pamoja na nyimbo hizo, nyimbo nyingine za mwanzo mwanzo za bendi hiyo zilikuwa, "Zuhura Naondoka", "Kamata Sukuma" waliotumia kujitaja majina, "Salima", "Nimeruka Ukuta Namba Mbili" na "Magdalena Namba Mbili" ambamo Maneti alifurahi baada ya wazazi wake kukubali amuoe Magdalena.
Dede kabla ya kwenda Sikinde alikuwa msondo. Ni mpenzi mkubwa wa Simba, siku hiyo Simba ilikuwa inacheza na Coastal. Dede akakacha onyesho la Msondo akaenda mpirani. Alivyorudi ukumbini baada ya mechi akatimuliwa na kunyang'anywa uniform. Hapo ndio akarudi Mlimani na kutunga nyimbo ya 'Talaka Rejea' yenye kuelezea masahibu yaliyomkuta. Alidai msondo kuna 'msondo-NUTA' na 'msondo-JUWATA'.
Alienda BIMALEE kwa kuwachukua Abdallah Gama (mchawi wa rhythm), Mwanyiro (kompyuta - Bass), na Mulenga (String master - solo) kutoka Mlimani. Kisha Jerry Nashon 'Dudumizi' kutoka Vijana.
Msimsahau DJ Mzee wa Mji Eddy Saly!
Ngoja niwarudishe kwenye mpira wa miaka ya sabini tena, kwani wakati huo tulikuwa na kandanada la hali ya juu sana haijapata kutokea. Inawezakana baadhi ya picha zimeshawekwa hapa ila nadhani hakuna tatizo kama nitazirudia, kwani wahenga walitufundisha kuwa jambao jema linastahili kurudiwa tena na tena. Simba
Cosmo: Sijaelewa jina hili la Cosmo lilikuwa lina maana gani