Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Jaribosi mwalimu wa kiswahili usagara usiombe akukute unamwita hivyo
 
KIKULACHO, mwalimu wa Chemistry alikua ana miwani kuuubwa kama yule jamaa wa kwenye wimbo wa Kikulacho wa Mr.Nice
 
Kwa wale wa Majengo p/s kulikuwa na Mwl sasa basi.Akifundisha utasikia sasa basi eheee wakoloni wakavamia nchi yetu eheee sasa basi tukafanyishwa kazi kwa niaba ya uchumi wa kikoloni.
 
Abatonga kibasila nasikia amefariki ni history alikua akifundisha na jitegemee advance
 
Nyamayao: mwalimu wa book-keeping st. anthony's mbagala huyu alikuwa anafanana na Nyamayao yule mwigizaji wa kaole enzi zile

Pipiro: Mwl. wa hesabu st. anthony alikuwa mfupi na mkorofi sana afu mbishi.

Desert Boy: mwl. wa history alijiita mwenyewe hilo jina akimaanisha yeye ni mgumu eti.
Bado yupo? na yule mzee mwenye kitambi kikubwa sana anafundisha GS.
 
Ilboru 1990's hadi 2000 mwanzoni...
Machakura...mwalimu Mkurya aliyekuwa hawezi kusema "mabaki ya chakula", ye anaita machakura
Chifu...mwalimu Mmasai aliyekuwa akicharaza fimbo kinyama huku kila mwanafunzi yeye akipenda kuwaita "chifu"
Michael Jackson...Madam mahiri mwalimu wa English aliyependa kuvaa miwani na kuweka nywele "curl" kipindi hicho
Mzulu...second master mmoja mrefu aliyependa kusumbuana sana na wanafunzi enzi hizo, mmoja wao Lazaro Nyalandu
 
Back
Top Bottom