Tukumbuke enzi za 'debate' na 'morning speech' tulipokuwa shuleni

Debates na M. speech nilikua napenda kusikiliza Errors tu..
most of eraz nilizowah sikia ni..
  • Mmoja alisema "Characteristic ya Ground photography it show One only single. akimaanisha it show one side view
  • mwingine et " Types of Tourism are Animal tourism and Movement tourism
  • mwingine eti "Micro organism is smallest deseas
Noma sana kilikuwa kipindi kimoja matata
 
Nilikuwa form one na kihereher e changu.kulikuwa na mada inasema agriculture is better than business. Mi nkaibuka na points za kukalilishwa upande wa proposal!!! Dah so unajua point za kukalilishwa na wakubwa bwsna!! Nimefika pale zikayeyuka fyeeee.afu nkiangalia macho yote kwangu!! Nilijikuta najampa kile kijampo cha Bomu LA atomic.usiniulize nn kilitokea
 
Nilikuwa form one na kihereher e changu.kulikuwa na mada inasema agriculture is better than business. Mi nkaibuka na points za kukalilishwa upande wa proposal!!! Dah so unajua point za kukalilishwa na wakubwa bwsna!! Nimefika pale zikayeyuka fyeeee.afu nkiangalia macho yote kwangu!! Nilijikuta najampa kile kijampo cha Bomu LA atomic.usiniulize nn kilitokea

Noma sana
 
Kukariri vocabularies hata kama haziendani unalitia ndani, unachanganya na kilugha cha kwenu humohumo. I remember this word "vandalism"
 
Mkuu umesahau "School baraza"
Usiombe ukaongea pumba tutakupigia makofi mwanzo mwisho mpaka uachie mic mwenyewe
 
Kuna siku mwalimu wa somo la General Studies alitoa kazi kwamba watu wajiandae, wakaekatika vikundi vya watu wanne mpaka watano, kipindi kijacho kila kikundi kitatoa presentation mbele ya darasa, halafu watu wataruhusiwa kuuliza maswali.

Ilikuwa nisehemu ya kutujenga katika "public speaking".

Basi, darasani kwetu mimi na wahuni wangu tulikuwa tunadharau kipindi cha General Studies, hatuingii.Tunakwenda kufanya mambo yetu.

Mwalimu alivyotoa assignment hiyo hatukuwepo.

Kibaya zaidi, hata tulivyorudi, hatukuuliza mwalimu kafundisha nini na kaacha assignment gani.

Basi baada ya siku chache mwalimu akarudi. Akawa kashajipanga na walimu wenzake kawaomba vipindi vyao ili apate muda mrefu, akawa ana vipindi kama vitatu.

Mwalimu akaingia darasani, tukamuamkia, akasema haya tujipange kwa vikundi tayari kwa presentation kama nilivyoagiza kipindi cha mwisho.

Basi kila mtu akawa anajipanga katika kikundi chake.

Tukabaki sisi ambao hatukuwepo wote, na sisi tumebaki "natural group". Group halijuikinachoendelea na wala tutajiandaa vipi.

Basi ikawa watu wanaenda mbele pale wanaongelea mambo ya uchumi, inflation, mara geography mara statistics. Mambo ambayo watu wanayajua. Maswalikibao ya kutoana jasho. Watu wanaumbuka.

Ikafikazamu ya kundi langu, washkaji wote wananiangalia mimi. Wanasema wewe ndiye kiongozi wetu, wewe ndiye msemajisemaji, wewe ndiye unakimiliki Kiingereza kama umezaliwa nacho, hapa wala hakuna mjadala, hata usijisumbue kubisha, utakuwa unapoteza muda tu, bora uanze kwenda mbele kutuwakilisha.

Nikasimama kutoka kwenye dawati nyuma ya darasa, nasimama huku sijui nitaongea nini na wala sijaandaa chochote.

Napiga hatua ya kwanza kuelekea mbele kwa mwendo wangu wa kudundika ambao shule nzima iliujua, huku sijui nitaongea nini.

Nimefika katikati ya darasa, nakwenda mbelekuongea, sijui nitaongea nini.

Nimefika mbele ya darasa, sijui nitaongea nini.

Nageuka kuliangalia darasa, nianze kuongea. Sijui nitaongea nini.

Naanza kufungua maongezi yangu, sijui nitaongea nini.

Nasema "Today, I am going to talk about..." sijui nitaongelea nini na wala hakuna kitu nilichotayarisha.

In a split second, nikasema, niongelee kitu ninachokipenda, kitu ninachokielewa, kitu nilichokisoma na kitu ambacho kitakuwa kipya kiasi kwamba hakuna mtu yeyote katika hili darasa (kiukweli mwalimu aliyaunganisha madarasa mawili pamoja) atakuwa anakijua.

nikamalizia sentensi yangu ya kwanza na "... cosmogony".

Watu mmmmh? Cosmo whaaat?

Kama muongeaji mzuri, kitu cha kwanza nikatoa introduction. Cosmogony is the science that deals with the beginning of the universe. It is an important science because it gives us knowledge about how the universe began and a better understanding of how things work for knowledges sake as well as for practical applications. Nikacharaza Big Bang Theory, nikacharaza singularity at the "beginning" of the universe, nikacharaza inflation theory ya Alan Guth, nikacharaza formation of stars, nikacharaza formation of heavier elements in the stars, nikapeleka mpaka Laplaces theory of how the solar system was formed, nikaongelea black holes na Hawking radiation, nikaeleza Schwarzchild's blackholes, nikaongelea the arrow of time and the second law of thermodynamics, nikaelezea mpaka tulipofika hapo tulipokuwa.

Muda woote watu kiiimya, hamna hata mwenye swali, kitu ambachokilikuwa tofauti sana na waongeaji wengine kwaniwaliingiliwa sana kwa maswali.

Nilipomaliza nikauliza, maswali?

Watu kimya.

Mwalimuwa General Studies akasema "Kwa kweli hapo hata mimi mwenyewe nashindwa kuuliza swali, kwa sababu haya mambo ndiyo kwanza nayasikia leo!"

Nikaona kumbe zile siku zote nilivyokuwa nasoma vitabu vya cosmology na cosmogony USIS pale Peugeot House haikuwa kusoma bure tu.

Nimetumia ile elimu leokujiondoa katika aibu ya kutokuwa na cha kusema katikadarasa ambalo sijajiandaa.
 
Nakumbuka niliwahi perform morning talk nlipokuwa njuka yaan form one, since hapo sijawahi perfom tena, debate ndio sijawahi kabisaa
 
nachokumbuka tu ni kwamba siku nimefika form one kama wiki hivi nashuhudia watu wanachofanya pale mbele in assembly ..Ndani ya wiki moja tu nikiwa form one niliona hiyo kazi sitoweza kufanya mimi ..Tangu hapo sikukaa assembly mpaka namaliza shule. MWISHO
 
nilisimama mbele natoa bonge la morning speech nikasifiwa na walimu jinsi nilivyopendeza nipo kat kat ya speech ukaja upepo tai ikapeperushwa kumbe shati lina kifungo kimoja tumbo lote nje, ndan kaboka nchiz( si unajua ukivaa kaptula ndani inapanda juu kuizd ya nje) kanaonekana, paled nzima hoi mpk walimu, nilichomoka kwa wenge baadala ya kuingia hata darasan nikaingia jikon nako nikakanyaga figa sufuria la uji bwaaaa, huko nako nikaacha wapish hoi nikakimbilia chooni, nashukuru sikuingia cha kike(ila ilibakia kdg tu) mana ingekua kali ya mwaka.
 
Back
Top Bottom